Member of EVRS

Wednesday 29 December 2010

Vacation!

Umh! I am on Christmas and New Year Vacation.

Visiting blog is altered due to here and there travelling.
I will keep posting whenever I get time.

I wish you a Happy New Year 2011

Friday 24 December 2010

Tanesco! Bado Kabisa!


Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kwa hivi karibuni limeanza kututumka na kutaka kuonyesha kuwa linawajali na kuwaheshimu wateja wake na kuthamini malipo yao kuwa ndio uha wa Tanesco (kwani ndio linawafanya watendaji waweze kwenda haja).
Kumekuwa na vipindi vingi vya kwenye radio na runinga wakijielezea mikakati yao, kujibu maswali ya wasikilizaji na watazamaji na pia kutoa ushauri kwa wenye malalamiko wapi wataweza kusikilizwa.
Hata siku ya tarehe 23 Desemba 2010, waziri wa nishati na madini Mh. Ngeleja akiwa na watendaji wa Tanesco, alikuwa akitoa maelezo na kujibu maswali ya wasikilizaji/watazamaji moja kwa moja (live bila chenga).
Mbali ya juhudi za uongozi wa juu kujaribu kulisafisha shirika hili la ugavi wa umeme, bado watendaji wa ngazi za chini yao, wana roho zilizosheheni kutu, utukutu wa akili au makusudi na kutowajibika.

Kuna sehemu fulani huko manispaa ya Ilala kuna nguzo imeoza na kuegeme ukuta nyumba kwa zaidi ya miaka 3 sasa. Wenye nyumba walishapiga kelele weee mpaka wakamwachia Mungu awalinde hizo nyaya zisijeangukia watu hususan watoto, basi ndio ikawa mauti tena.



Mpita njia waweza kuona nguzo hiyo ikiwa imeegemea ukuta, na kwa hapo chini utaona ule waya unaoshikilia nguzo ikae wima ukiwa umelegea kabisa, kuashiria ya kuwa hauna kazi tena kama ilivyokusudiwa!

Picha hii chini inaonyesha nguzo ikiwa imekwisha kabisa na kugeuka mahali pa ndege kujikinga na jua la Dar es salaam!
Na hii picha juu ndio hali halisi ya nyaya za umeme zikiwa zimeshuka chini kabisa chini ya usawa wa mabati ya nyumba! 

Kinachoshangaza, wiki chache zilizopita, watu wa Tanesco walikuja kumuunganishia umeme mteja mpya, na wakaweka waya kutoka kwenye nguzo hiyo hiyo iliyooza, na walipotaarifiwa kuhusu ubovu wa mlingoti huo, waliuangalia na kusema wanaenda kutoa taarifa ofisini, na kwa sasa inakaribia miezi 2 na hakuna taarifa wala mtu aliyekuja kuona.

Watendaji wa kweli walipotaarifiwa, wakawapa maelekezo walalamikaji mahali pa kwenda na namba za simu, sasa sijui nicheke au... mhusika alipopatikana kwa simu, alisema yupo likizo na akatoa namba nyingine ya mtu ambaye kwa zaidi ya wiki amefunga simu, na watu wakamshauri mlalamikaji ati asubiri sikukuu zipite ndipo akaulizie tena!!!!!

Hivi hizo nyaya za umeme na nguzo zinajua sikukuuu hizo ambazo Tanesco wanasubiri ziishe kwanza!
Na hao wafanyakazi watafungaje line mpya kwenye nguzo wanayoiona imeoza?!
Likitokea janga ... ni nani wa kulaumiwa.
Hakika watendaji wabovu wa Tanesco wanastahili kuongozwa  na mtu kama Stalin :-(

Tuesday 21 December 2010

Hukumu ya BAE SYSTEMS Kutolewa Leo

Hukumu kesi ya shirika kubwa la kuuza silaha la Uingereza (BAE Systems) itatolewa kesho na Jaji Bean anayesikiliza madai ya kampuni hiyo kujihusisha na rushwa kubwa kwa kuiuzia Tanzania radar ya kijeshi ambayo iliigharimu nchi maskini ya Tanzania zaidi pauni za Uingereza milioni 28 ( Zaidi ya sh.billioni 70 za kitanzania)

Hakimu huyo aliihoji kampuni hiyo kuhusu madai ya kumlipa mfanyabiashara Sailesh Vithlani kiasi cha kama pauni millioni 7.7, katika kujitetea kampuni hiyo ilidai ilitoa pesa kumpa Vithlani kwani walimtumia kama papa mdogo kupenyeza ili waweze kushinda zabuni ya kuiuzia Tanzania rada hiyo kwa bei ya kuruka.
Kampuni ilikiri kuwa na kosa dogo la kuweka vizuri kumbukumbu za mahesabu kwa kudai walimlipa Vithlani kama mshauri wa kiufundi wakati Vithlani mwenyewe hakuwa na ujuzi wowote katika masuala hayo ya ununuzi wa rada.

Jaji hakuridhika na maelezo hayo, na akaendelea kusisistiza kuna kila dalili ya rushwa kwani alihoji kwa nini zaidi ya 97% ya malipo ilipitia  kwenye mikono ya Vithlani!, kiasi kwamba alitaka kutoa uamuzi wa kuita mashahidi kueleza ni vipi pesa alizopewa Vithlani zilivyotumika kabla ya kutoa hukumu yake, lakini baadaye alibadili mawazo yake na kuahidi kutoa ya hukumu dhidi ya BAE System leo siku ya Jumanne.
 
Hapo awali, kampuni hii ilikiri kuwa na makosa ya kuweka vibaya kumbukumbu za pesa, na ilikubali kulipa pauni milioni 3 kama fidia kwa Tanzania na pesa hizo kutumika nchini Tanzania kwa ajili ya shughuli za maendeleo. Lakini ikawa inasisitiza haikutoa mlungula wowote.

Pata maelezo zaidi kwa mwanzilishi wa mjadala huu wa uuzwaji wa rada hii kwa bei isiyo na tija

Monday 20 December 2010

WikiLeaks Cable Hit Tanzania

Today I was reading Subi's Wavuti and came accross this astonishing news about radar scam!

Quoted ......The Tanzanian prosecutor, Edward Hoseah, investigating worldwide misconduct by BAE, Britain's biggest arms company, confided to US diplomats that "his life may be in danger"...

Hoseah met a US diplomat, Purnell Delly, in Dar es Salaam in July 2007, and claimed (unrealistically it turned out) he would be able to prosecute guilty individuals in the BAE case. The US cable reports: "He called the deal 'dirty' and said it involved officials from the Ministry of Defence and at least one or two senior level military officers."

Hoseah spoke gloomily about the prospects for Tanzania's anti-corruption struggle and his original hopes to prosecute the "big fish" of corruption.

"He told us point blank... that cases against the prime minister or the president were off the table ..." The cable then details allegations against former leaders and their inner circles, saying they would be "untouchable".................

Today, is the beginning of the case related to BAE fraud on radar scam. More terrible news are going to be revealed out ....

The Guardian (UK) has more astonishing news

Friday 17 December 2010

Enjoy your Weekend!

Hi Guys, I am still with you.
  
But, I wish christmas will be ten weeks ahead, so that this working under pressure to beat the deadlines will be kept out of our mind and order.  
  
I wish you the nice weekend for those who will have the really weekend.

Wednesday 15 December 2010

Homa ya Harusi ya Prince William Yazidi Kupanda

Baadhi ya makampuni ya kutengeneza zawadi yameanza kuchangamkia tenda ya kutengeneza zawadi ya Harusi ya mjukuu wa malkia wa Uingereza Prince William ambaye anatarajjia kufunga ndoa na Kate Midleton mwishoni mwa mwezi Aprili 2011.

Kampuni hizo zipo Uingereza na China.
Wamiliki wameanza kutengeneza vito vya thamani kama pete na vyombo vingine vikiwa na picha ya mtoto huyo wa kifalme na mchumba wake, kwani wanatarajia soko litakuwa kubwa sana hapo harusi itakapokuwa inakaribia.

Kampuni moja ya China imeanza kutengeneza pete mfano wa ile ya uchumba ambayo Kate amejipatia. Pete hiyo ambayo imetengenezwa kwa almasi za rangi tofauti tofauti ikizunguka kito cha rangi ya sapphire ilikuwa ya Diana. William alisema hakutaka kabisa marehemu Mama yake apitwe na tukio lolote la harusi hiyo, ndio maana alikubali mchumba wake avikwe pete ambayo ilikuwa ya uchumba ya mama yake.

Wachina wamepata haki ya kutengeneza mfano wa pete hiyo, na kwa yeyote anayetaka kununua, Soko lipo wazi sasa.

Harusi hiyo ambayo itaonyeswa moja kwa moja na vyombo vya runinga mbalimbali inatarajiwa kuvunja rekodi ya harusi kuangaliwa na watu wengi duniani.

Gonga hapa kupata habari zaidi

Monday 13 December 2010

Gwiji la Muziki Remmy Mtoro Ongala Afariki Dunia

Mwananmziki mkongwe na maarufu nchini Tanzania, Ramadhani Mtoro Ongala au maarufu kama Dokta Remmy amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.  
  
Remmy alikuwa akisumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kisukari ambao ulisababishwa alazwe mara kadhaa hospitalini ikiwa ni pamoja na hospitali ya taifa ya Muhimbili. Inasemekana amefariki kwa matatizo hayo hayo ya kisukari.  
   
Remmy atakumbukwa kwa mengi ikiwa ni pamoja na kuwa mshindi wa pili kwa sura mbaya Tanzania japo alilalamika ya kuwa kaonewa kwani aliamini ya kuwa yeye ana sura mbaya kuliko watu wote waliokuwa wanaishi Tanzania wakati huo!!!!!  
  
Pia kuna nyimbo kadhaa alizoimba ambazo watu watatzikumbuka ikiwa ni pamoja na wimbo wa KIFO. 
 
Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi

Saturday 11 December 2010

Tanzania Bara Yaingia Fainali ya CECAFA Tusker Challenge Cup 2010

Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) hapo juu wakishangilia ushindi, jana ilifanikiwa kuingia fainali ya kombe la CECAFA baada ya kuwafunga timu ya Uganda (The Cranes) kwa mikwaju ya penati 5 - 4


Kipa namba moja wa Kilimanjaro Stars, Juma Kaseja kama anavyoonekana hapo juu akiiokoa penati moja ya waganda na hivyo kuifanya Tanzania Bara kuingia fainali.

Fainali itakuwa kesho, ambapo Tanzania Bara itapambana na timu ya Ivory Coast. Hata hivyo ni lazima kombe libaki Tanzania hata kama Ivory Coast itashinda, kwani timu hii ya Afrika Magharibi ilialikwa tu kupasha moto mashindano, na sheria za CECAFA timu mualikwa huwa haipewi kikombe, isipokuwa inapewa zawadi iliyopangwa kwa mshindi wa kwanza, na kikombe huchukuliwa na nchi mwanachama aliyeshika nafasi ya juu.

Kwa maana hiyo, Kilimanjaro Stars ndiyo itakayopewa kombe hilo kwa matokeo ya aina yoyote.

Tuna imani Tanzania Bara itashinda na kuchukua kombe hilo.

Picha kutoka kwa michuzi

Friday 10 December 2010

Nobel Peace Price 2010 Received by a Ghost


The family of Liu Xiaobo who is the Nobel Peace prize winner for 2010 has been banned to attend the prize giving ceremony in Oslo - Norway today.

They were not granted permission to leave China for not clearly known reasons, but every one in the world can guess the main reason.  
  
Xiaobo has been sentenced to jail for 11 years on charges for trying to "westernises" China. 
The wife of Xiaobo has been in house arrest for 2 months now since annoncement of the winner for Nobel Prize. Yesterday the security was even more tighter at the front of her apartment in Beijing with both plain and uniformed security officers.

For another time since 1936, this year ceremony will be conducted without the laureatte or representative to be in Oslo to receive the award.

More info at TVS

Thursday 9 December 2010

Unaelewa Nini Kuhusu Uhuru wa Tanganyika

Leo, watanganyika (hata kama huupendi huu ukweli), wamesheherekea miaka 49 tangu wapate uhuru wao kutoka kwa mkoloni (Uingereza). 
  
Asilimia kubwa ya watu wanaofuatilia uhuru huu, wanaukandia na kuubomoa, na kuona hauna maana kubwa kwa hali halisi ya kiuongozi tulionao na watendaji wengine. 
  
Mkulima wa kijijini, ndio kwanza haelewi hata maana ya uhuru wenyewe.
Kwa wale wanaokenua meno na kushangilia siku ya uhuru, wanapaswa kujiuliza kwa nini watnganyika wengine hawaelewi kabisa maana ya siku na uhuru wenyewe.  
  
Nina hakika uhuru wenye maana kwa wananchi, kila mtu huwa anaguswa na siku hii, lakini kwa watanganyika, naona huwa wanajua kwa kuwa siku hiyo hawatakiwi kwenda kazini, na pia kushuhudia gwaride la kijeshi, baada ya hapo hawajui chochote.

Mchambuzi Fadhy Mtanga, kaeleza mtazamo wake kuhusu uhuru wa Tanganyika, soma makala yake hapa

Wednesday 8 December 2010

Mstaafu ateuliwa kushika Nyadhifa ya Mstaafu

Rais Jakaya Kikwete amemteua Jaji Mstaafu Salome Suzette Kaganda kuwa Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma. Uteuzi huo ulianza tangu tarehe 4 Desemba 2010. 
  
Jaji mstaafu Salome amechukua nafasi ya jaji mstaafu Stephen Ihema ambaye amemaliza muda wake.  
Taarifa hizi zimetolewa na Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu.
   
Tukumbuke pia kuwa tume ya uchaguzi inaongozwa na Jaji Mstaafu Lewis Makame.  
  
Sielewi vizuri hii dhana ya kuchagua wastaafu kuwarithi wastaafu.
Ningependa kusikia watyu wenye uwezo ambao hawajastaafu wakishikilia nyadhifa hizo na watu wengine wanaochipukia wakibana nafasi za wenzao wanaopanda nyadhifa, na sio kila siku wastaafu ndio wanashika hatamu.
Suala hili lingeenda pia na kwa wakuu wa vyuo vikuu, weneyviti wa bodi mbalimbali kwani wengine wako hoi sana kwa uzee na sioni sababu ya wao kuendelea kukamata nyadhifa hizo.

Tuesday 7 December 2010

Tuwe Waangalifu na Mwisho wa Matumizi ya Bidhaa

Mimi bado nina imani vitu vinavyotengenezwa Bongo, vina uzuri fulani, na kwa kiasi fulani huwa vina ubora unaoridhisha hususan mambo ya vyakula.
Ninaogopa kuvamia hasa vile vinavyotoka Uchina, kwani vingi huwa ni bandia. 
 
Lakini wabongo wanaudhi pale wanapokuwa si makini katika kuangalia mazao yao wanayouza au kununua kama yana vigezo vyote vinavyofaa kwa mlaji kupata taarifa sahihi ya vyakula vyenyewe, kama paketi au gunia limefungwa vizuri, bidhaa iliyomo ndani haijaharibika, na kama lebo inaendana na bidhaa iliyopo. Na cha muhimu zaidi tarehe ya mwisho ya matumizi ya bidhaa yenyewe. Hapo mii ndio hutoa jicho la nguvu. 
  
Nikiwa mitaa yangu ya huku, nikisikia mtu aja kutoka Bongo, ni kawaida yangu kuagiza chochote ali-mradi nafsi yangu itafurahia matunda ya mamaland, hata kama ni vitumbua, wee leta tuu.

Kwa mara nyingine tena nilikutana na lebo hii hapo juu, tarehe ya mwisho wa matumizi, nimeitafuta kwenye kalenda zooooooote sijaipata. 
  
Hivi hao watengenezaji wa vyakula hivyo, huwa hawana elimu ya tarehe za kwenye kalenda, na hao wanaonunua kuuza vyakula kwenye masoko haya ya kisasa hawana wataalamu wa vyakula kukagua kama kila kitu kiko sawa.  
   
Ukisiskia mtu anasema bidhaa za wabongo ni feki sijui utamjia juu au uta.... 
  
Tunahitaji kuwafahamisha wajasiriamali wetu kuwa makini na bidhaa zao kama wanataka mafanikio ya kweli.

Monday 6 December 2010

Nawaza tu


Aina mbali mbali za vimiminika ambavyo kamwe haviozi hata kama vitakaa kwa zaidi ya miaka kumi.

Mimi nimeshapata 6, lakini nataka mpaka idadi ifikie kumi.
Jaribu kufikiria nami na unipe mawazo

Duh! Jumatatu njema

Image from CGA

Saturday 4 December 2010

Vituko vya Marais wa Afrika: Ivory Coast Presidential Results Controversy

I hate people who thinks they were created to be leaders for life, look this man from Ivory Coast!
  
Marais wengi wa Afrika wana kasumba ya kujiona kuwa wao ndio pekee wanaofaa kuongoza nchi kama wafalme, yaani kifo tu ndicho kinaweza kuwaondoa madarakani.

Mifano michache ya ving'ang'anizi ni kama Museveni (Uganda), Mugabe (Zimbabwe), Mubarak (Misri), na hata huyu jamaa wa Angola ambaye kaamua kuwa rais anachaguliwa na wabunge walioshinda katika uchaguzi na sio wananchi tena.

Nguli mwingine ni Laurent Gbagbo wa Ivory Coast (pichani juu) ambaye ametia mpya hivi karibuni ktika uchaguzi huru uliofanyika nchini Ivory Coast. Katika raundi ya mwisho alipokuwa anashindana na mpinzani wake mkuu Allasane Ouattara (pichani chini), alihisi kuelemewa na hivyo kuamuru matokeo yasitishwe kutangazwa, na sehemu iliyokuwa bado kumaliza kutolewa matokeo ilikuwa ni ngome ya mpinzani wake
Hii ilisababisha kuchelewa kutolewa matokeo kwa siku mmoja, hata hivyo tume ya uchaguzi ilimtangaza Ouattara kama mshindi  kwa kupata  54%, na miongoni mwa watu wa kwanza kumpongeza alikuwa Rais Obama wa Marekani.
    
Cha kushangaza, baraza la katiba ambalo ndicho chombo kikuu cha mwisho kuidhinisha matokeo kilipinga matokeo ya tume na kusema tume ilichelewesha kutoa matokeo, na hivyo baraza hili likachakachua matokeo na kumtangaza Gbagbo kuwa kashinda kwa 51.45%.

Kwa sasa jeshi limefunga mipaka yote ya Ivory Coast, na kuzuia vyombo vya habari vya kimataifa kuchukua na kurusha habari zozote za uchaguzi huo.

Ufaransa na Umoja wa Mataifa umekataa kutambua matokeo ya pili ambayo yalimwengua Ouattara kwenye nafasi ya ushindi.

Ndugu yangu, utajiju na maswali yatakayokujaa kichwani mwako!!

Friday 3 December 2010

Kenyan Football: Sad Story

Kenya National football team (Harambee Stars) for this year is almost out of competition for CECAFA Challenge cup in Dar es Salaam, Tanzania.  

  
They lost all their games so far after being beaten by Malawi by 3-2, and then by Ethiopia by 2-1. Now they will have to face tough opponents, the defending champions, The Uganda Cranes who have gained 4 points out of 2 games they have played.

It is so sad to see our neighbour Kenya is going out of competition so easily while last year they were runner-up after being beaten in the final by Ugandan team.

Kenya has been tough opponents in these competitions which are the oldest regional tournaments in Africa.

The problems probably are not related to the coach Jacob “Ghost” Mulee or players, but rather poor preparations. I am sure lack of appropriate football governing body in Kenya is the major factor for poor preparations.  
 
Probably FIFA which has now turn to have many corruptions scandals has a major role in distorting football programmes in Kenya, by deliberating ignore the elected football association and supporting the company to run the national league and international competitions. This has created big chaos, since the governing body recognised by Kenyan government is the one FIFA doesn’t want to hear. 
  
We all know Government has a role in improving National football team by supporting in various ways including some advice. But with the current situation in Kenya, it is practically impossible to run the intended programs.  
  
FIFA is not that clean to dictate what Kenyans they should do. This remind me what FIFA they did to our Tanzania when they stand firm to support corrupt leaders who were accused by our Government for financial misuse of the same FIFA money. They only gave up when the secretary general of football association of Tanzania was jailed for the same fraud charges and the chair was asked to return what he took illegally from the office. It was then, the proper elections were done and all corrupt leaders were axed out. Since then Tanzania has a steady football development, also football had grand support from the Government and of course the corrupt FIFA. 
  
I think FIFA should repent its decision on Kenya, and leave Kenya to manage her internal football activities which will help the region to have stiff competitions and see Eastern Africa roars into world cup!  
   
Huu ni mtazamo wangu tu!!

Thursday 2 December 2010

Tanesco Yaanzisha Blogu


Kwa wale wanaotaka kujua ratiba za mgao wa umeme, kutoa maoni kuhusu namna ya kuijenga na kuimarisha Tanesco na kadhalika, basi habari nzuri ni kuwa Tanesco wameanzisha baraza la mawasiliano wakitegemea msaada mkubwa kutoka kwenu wananchi mnaoishi Tanzania ili muwasaidie waendelee kuwaangazia maisha

Wanatoa rai ya kuwasaidia na sio kuwatukana kwani matusi si ustaarabu.

Nimeiona kwa Subi na pia link yao ni hii hapa

Wednesday 1 December 2010

Nimebanwa Mbavu

It appears as if I have abndoned my blog!!!!  
  
La hasha, I am occupied with activities for the end of the year.
I expect to take a vacation, therefore, lazima kila kitu kieleweke kabla sijaondoka.  
  
Just keep on visiting my blog, I appreciate and enjoy even on your silent tracking over.
You are all great, thank you!

See you soon

Monday 29 November 2010

Matumaini Mapya Wizara ya Ujenzi

Nilikuwa nikiangalia runinga leo asubuhi, nikapokea habari nzuri zinazohusu ujenzi wa barabara Tanzania. 
  
Waziri wa ujenzi, Mhesh Pombe Magufuri akiwa na naibu waziri wake Prof Harrison Mwakyembe, jana walipokuwa wakiongea na watendaji wa wizara ya Ujenzi, alitoa muda wa mwezi mmoja kwa watendaji hao kujipanga na kumletea taarifa ya matarajio (projections) ya utendaji wao wa kazi kwa kipindi kijacho. 
   
Magufuri aliyeonyesha ukali katika kauli zake, alikemea tabia ya usimamizi mbovu wa miradi ya serikali, na pia kutowajibika. 
Mbali ya yote hayo, alielekea kushangaa ni kitu gani kinachoshindikana kujenga daraja la Kigamboni, akatolea mfano wa huko Uchina ambako aliona daraja lenye urefu wa km 26 likijengwa kwa miezi 14 tu. Alitoa rai kwa NSSF kujenga daraja hilo haraka iwezekanavyo, vinginevyo ataiomba benki kuu ya Tanzania kuidhinisha na kutoa pesa za ujenzi wa daraja hilo ili serikali isimamie. Kwa hapa naona ni neema kwa wakazi na wageni wanaotembelea Kigamboni ambao wamekuwa wana kilio hiki kwa muda mrefu sasa.  
   
Cha kufurahisha zaidi, na iwapo kitakuwa cha vitendo, ni pale Magufuri aliposema uanze mpango na ujenzi wa madaraja ya juu ya kupitia magari (flyovers), kwani hakuna kinachoshindikana. Pia kuwaeleza wazi kutakuwa na ziara za kushtukiza kukagua kazi na miradi mbalimbali ya ujenzi, pale itakapokutwa kazi ya ujenzi inalegalega, basi mhandisi anayesimamia ajijue ya kuwa kibarua kimekwisha ota nyasi (Keshafutwa ajira).  
  
Na mwisho aliwagawia watendaji wote ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 - 2015 ili waweze kufahamu ni nini serikali ya CCM inakusudia kutekeleza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kutoka sasa. Na ilani hizo walizigawa yeye mwenyewe na Mwakyembe kwa mikono yao wakimpa kila mtendaji pale alipokuwa amekaa, na sio watendaji kuzifuata kwenye meza kuu.  
  
Mimi nasema, mwanzo huu unatia moyo, kwani tunawafahamu Magufuri na Mwakyembe ni watendaji wazuri na wasimamizi katika maslahi ya Taifa. Nawatakia kila la heri.

Friday 26 November 2010

Have a nice weekend

I am running short of words...... 
 
This week was hectic ... busy.... whatever you call it..
  
Tomorrow, there is a community work here, no shop, market, bank, hotel, transport etc will be available from morning till mid day. 
  
If you are going to airport, you..either go before 7.00 am or after mid day! I am very serious.

Wishing you a lovely weekend!! :-x

Thursday 25 November 2010

Womb Fight!!!!



What kind of persons they are gonna be!

Enjoy your thursday!

Wednesday 24 November 2010

Baraza la Mawaziri na Naibu Mawaziri Novemba 2010

Ofisi ya Rais:
  • Utawala Bora - Mathias Chikawe
  • Mahusiano na Uratibu - Stephen Wassira
  • Menejimenti ya Utumishi wa Umma - Hawa Ghasia

Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Muungano - Samia Suluhu
  • Mazingira - Dr. Terezya Luoga Hovisa
Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi
  • Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  George Mkuchika
            Naibu (TAMISEMI) - Aggrey Mwanri na Kassim Majaliwa

Wizara ya Fedha - Mustapha Mkulo
Naibu Gregory Teu na Pereira Ame Silima

Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Shamsi Vuai Nahodha
Naibu - Balozi Khamis Suedi Kagasheki 
 
Wizara ya Katiba na Sheria - Celina Kombani
 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa - Bernard Membe
Naibu Mahadhi Juma Mahadhi
 
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Dk Hussein Ali Mwinyi
 
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi - Dr. Mathayo David Mathayo
Naibu - Benedict Ole Nangoro
  
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia - Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

 Naibu - Charles Kitwanga
 

  
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Prof. Anna Tibaijuka

 Naibu - Goodluck Ole Madeye
  
Wizara ya Maliasili na Utalii - Ezekiel Maige
  
Wizara ya Nishati na Madini - William Mganga Ngeleja
Naibu - Adam Kigoma Malima
  
Wizara ya Ujenzi - Dr. John Pombe Magufuli
 Naibu - Dr. Harrison Mwakyembe
   
Wizara ya Uchukuzi - Omari Nundu
 Naibu - Athumani Mfutakamba

  
Wizara ya Viwanda na Biashara - Dr. Cyril Chami
 Naibu - Lazaro Nyalandu
  
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi - Dr. Shukuru Kawambwa
 Naibu - Philipo Mulugo
 

 
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii - Dr. Haji Hussein Mpanda
 Naibu - Dr. Lucy Nkya
  
Wizara ya Kazi na Ajira - Gaudensia Kabaka
 Naibu - Makongoro Mahanga
  
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Sophia Simba
 Naibu - Umi Ali Mwalimu
  
Wizara ya Habari, Vijana na Michezo - Emmanuel John Nchimbi
 Naibu - Dr. Fenella Mukangara
  
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Samuel John Sitta
 Naibu - Dr. Abdallah Juma Abdallah
  
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika - Prof. Jumanne Maghembe
 Naibu - Christopher Chiza
  
Wizara ya Maji  - Prof. Mark James Mwandosya

 Naibu - Eng. Gerson Lwinge

  
 
Habari kutoka Ikulu Mawasiliano

Naomba Ushauri

Sehemu ninayoishi hapa Kigali, ina usalama wa hali ya juu, na patrol za polisi usiku zipo karibu muda wote! 
   
Tarehe kama ya leo, yaani 24 Mei 2010, mfanyakazi wangu wa nyumbani (house boy) alirudi kutoka "kijijini" alipoenda kusalimia famlia yake, na aliporudi usiku nilishtukia tu yumo ndani ya ua, bila kufunguliwa geti.
Nilipomuuliza kaingia vipi, akasema alifungua mlango kwa ndani kupitia kidirisha cha ulinzi (Security window), kwa ujumla sikuamini amini. Siku iliyofuata niliporudi kutoka kazini nilikuta katoweka, baadaye niligundua upotevu wa fedha kutoka chumbani kwangu.  
Habari ilifikishwa polisi, na hakuna kilichofanyika.  
   
Kijana huyo alikuwa naaminiwa sana na kila mtu, lakini mimi tangu siku ya kwanza roho yangu ilimkataa. Japo familia yangu walielekea kumwamini na kumpenda. Sasa naona wamebadilika kuliko hata mimi!

Leo tarehe 24 Novemba( Sielewi kwa nini ni hii tarehe), miezi sita imetimia, wakati naingia gereji kujiandaa kuondoka kwenda kazini, niliona nyendo zisizo za kawaida kwenye kona ya gereji, nilipokaza macho zaidi nikaona macho ya blink hapo kwenye kona huku yakiwa yamefunikwa na mlango mbovu na viti chakavu. Nilipokamua macho zaidi, mara akaibuka kijana yule yule aliyekuwa mfanyakazi wangu. Akadai aliruka ukuta usiku kupata mahali pa kulala na kisha alikuwa anasubiri nikienda kazini, naye ajiondokee zake!  
   
Kwa sababu kwa sasa naishi mwenyewe, nilitoka nje kuomba msaada wa mlinzi ili nimdhibiti, lakini alifanikiwa kwa muda kuchomoka na kukimbia, lakini weeee, watu wanajua kupiga mitama ama ngwara, hakufika mbali ndo hivyo tena akaibusu ardhi.  
  
Baada ya kumfkisha polisi, akakiri alikwiba siku za nyuma. Na ni kweli aliruka ukuta kuingia ndani ya nyumba bila idhini yangu.  
HUWEZI AMINI ALIHUKUMIWA KIFUNGO HAPO HAPO, na kwa sasa amekwisha anza kutumikia kifungo jela.  
Hakuna kesi mahakamani wala kuhangaishana na kuleta ushahidi. kwani kila kitu kilikuwa hadharani.  
   
Upekuzi wangu pale alipokuwa amejificha, nilikuta sanamu ya plastiki ya mnyama mwenye pembe 2 ambazo zipo sharp. Hiyo sanamu nilishawahi kuiona ndani ya nyumba miezi mingi wakati naingia, nikaitupilia jalalani. Pia sanamu hiyo nilipoikuta, siku za nyuma nilishawahi kukuta sanamu ya mtu aliyevishwa hirizi ya mbao!  
   
Mimi ni mtu wa imani kidini na huwa sitetereki, kawaida yangu ni kuzichoma moto takataka kama hizo.  
  
Bado najiuliza, kama nikimwona tena baada ya kifungo ndani ya himaya yangu nimfanye nini.  

Sunday 21 November 2010

Jumapili Njema

Jana modem yangu ya internet ilinigomea kabisa, nikashindwa kupata habari mpya.
Leo nimeshtukizwa na kuingia kazini tangu asubuhi mpakaaaa......

Hivyo nawatakia jumapili njema, na pia tuwaombee hao wanaume ambao wamezuka sasa na mtindo wa kuua familia zao kwa visu.  
  
Kwani hivi karibuni huko Kilimanjaro mtu kaua mama yake mzazi na watoto wake wawili, juzi tu, huko Kenya kuna mtu kaua mke wake mjamzito na watoto wawili kwa visu tena, mmoja tu wa miaka 3 ndio alikimbia. Halafu tena wiki kadhaa zilizopita jamaa mmoja tena huko Marekani mwenye asili ya Afrika, aliua mke na watoto wake wawili kwa mtindo huo huo. 
  
Bahati mbaya au nzuri kama utakavyochukulia wewe, wanaume hao wote nao walikufa aidha kwa kujiua au watu wenye hasira kali kuwamaliza!
 
Aaaah, nilishasahau, nilikuwa nataka kuwatakia jumapili njema tu!

Friday 19 November 2010

USA 2012 Elections Fever start Rising Now

Sarah Palin, who was runner mate for 2008 Republican presidential candidate, has shown some interest for Republican presidential nomination for 2012 to challenge Democrats likely presidential candidate, Barack Obama.  
  
The matter for running for presidential race is still under Palin family's discussion, but Palin's fans have started canvancing for her. 
 
So far, Barack Obama has upper hand where still 55% have a positive minds towards him despite the hard economic challenges affecting the globe and his Government, while for Sarah Palin only 47% gave her chances that might win the 2010 elections, while 53% unfavour her.

Thursday 18 November 2010

CHADEMA Wamsusa Rais Kikwete na Kuondoka Bungeni

Katika hali isiyokuwa ya kutarajiwa, Wabunge wa CHADEMA leo wameondoka ndani ya ukumbi wa Bunge mara tu Rais Jakaya Kikwete alipokuwa anataka kuanza kuhutubia bunge la 10. 

Kwa muda wote wakati rais anaingia na muda wa kusoma dua, wabunge wote walikuwa wametulia. Lakini mara tu rais Kikwete alipoanza kuongea, wabunge wa CHADEMA wakaamka ghafla na kutoka nje huku kukiwa na kelele za mzomeo na wabunge wa CCM wakiwaonyesha mikono kwa kupunga wakimaanisha waondoke tu! 
 
Bado sababu halisi ya kumsusa Rais Kikwete haijawekwa hadharani, japo ilikuwa inajulikana ya kuwa uongozi wa CHADEMA ulikuwa unadai rais Kikwete hakushinda kihalali kutokana na ubovu wa uendeshaji wa tume ya uchaguzi ya taifa, huku wakiwa wanaituhumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya uchakachuaji wa kura kutoka kwa baadhi ya maofisa wake na kuipendelea CCM huku wakiihujumu CHADEMA. 
  
Majuzi, spika wa bunge la Tanzania, Anne Makinda, aliwaita viongozi wawili wa kambi ya upinzani kutoka CHADEMA na kuwasihi wakubali kumtambua Rais Kikwete kama kiongozi halali wa Tanzania vinginevyo wanaweza kupoteza haki zao za msingi za kuwawakilisha vyema wananchi waliowachagua. Hatima ya kikao hiki cha faragha hazikujulikana wazi.

Tuesday 16 November 2010

Pinda athibitishwa kuwa Waziri Mkuu Tanzania


Mhesh Kayanza Mizengo Peter Pinda leo jioni amethibitishwa na Bunge kuwa waziri mkuu wa Tanzania baada ya kupata kura za ndiyo 277 sawa na asilimia 84.5 ya kura halali zilizopigwa, na pia kura 49 za hapana sawa na asilimia 14.9
  
Mhesh Pinda anatarajiwa kuapishwa kesho ikulu ndogo ya Chamwino iliyopo Dodoma. Na hapo baadaye yeye kwa kushirikiana na Rais Kikwete na pia makamu wa Rais, Dk Bilal wataandaa baraza jipya la mawaziri.  
  
Watu wengi walikuwa wanatarajia uteuzi wa Pinda kuwa waziri mkuu wa Tanzania.  
   
Hatuna budi kumpongeza, tukitumaini ya kuwa atatenda majukumu yake kama kiongozi wa serikali bungeni vyema na kupigania haki ya watanzania wote na sio maslahi ya chama chake.  
 
Mungu ibariki Tanzania.

Monday 15 November 2010

Wapinzani Wanaelekea Kuungana Bungeni

Kuna dalili ya kuwa wapinzani ndani ya Bunge la Tanzania wataungana mara pale Aliyekuwa kiongozi wa upinzani katika bunge lililopita Mhesh. Hamad Rashid Mohamed kutamka ya kuwa wapo tayari kushirikiana na vyama vyote vya upinzani kuunda umoja ndani ya bunge na hasa kwa kutoa mawaziri vivuli.  
  
Na pia alisema ya kuwa hawana nia ya kuwania uongozi katika kambi ya upinzani, bali kushirikiana kwa pamoja katika harakati za kukuza demokrasia ndani ya bunge na pia kuendelea kuikosoa Serikali kama walivyokuwa wanafanya katika bunge la 9. 
  
Mwanzoni, kulielekea kama kuna mfarakano ambao chanzo chake hakikujulikana, na watu walihisi zilikuwa ni zile kauli za Lipumba kujiona kuwa ni bora zaidi kufuikia hatua ya kujifananisha na mlima kilimanjaro, na kumfananisha mgombe aurai wa Chadema Mhesh Willbirod Slaa kama kichuguu.  
  
Tuna imani ya kuwa CCM nao wanalitambua hilo, na hivyo watakuwa makini sana katika shughuli za kuendesha mijadala na uwajibikaji ndani ya bunge, vinginevyo 2015 wataendelea kupoteza nguvu yao bungeni na mwisho kitakachofuata wanakijua.

Friday 12 November 2010

Anne Makinda: Mwanamke wa Kwanza Kuwa Spika wa Bunge la Tanzania


Mh. Anne Makinda (Pichani) amechaguliwa kuwa spika wa bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuchaguliwa na wabunge wa Tanzania kwa kura 265 na kumshinda mpinzani wake, Mh. Mabere Nyaucho Marando aliyepata kura 53.  
  
Ushindi huu ulitarajiwa ukizingatia idadi ya wabunge wa chama cha mapinduzi (CCM) anakotoka Anne Makinda kuwa wengi kwa zaidi ya 75% ya wabunge wote.  
 
Mh. Anne Makinda alikuwa naibu spika kwa miaka mitano iliyopita chini ya Mh. Samuel Sitta ambaye mwaka huu hakupitishwa kugombea kiti hicho na chama chake.   
  
Anne Makinda anaweka historia mpya ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo katika bunge la Tanzania.  

Katika hatua za mwanzo za mchakato wa uchaguzi, wakati Mh Marando anajieleza, ulipowadia wakati wa maswali, kulitokea tafrani ndogo ya mbunge mmoja mzoefu wa CCM kutaka kukiuka maagizo ya mwenyekiti aliyesimamia uchaguzi huo Mh. Anna Abdallah wa kutaka kuuliza swali kwa kutumia kipaza sauti ambacho mgombea ndio alikuwa anakitumia, na hivyo kupandisha munkari kidogo wa baadhi ya wabunge.  
  
Aliporuhusiwa kuuliza swali kupitia kipaza sauti kingine, ilibidi akatishwe kwani lilionekana halikuwa swali bali maelezo kinyume na yaliyotarajiwa, hata alipoambiwa kunyamaza, yeye aliendelea tu kuongea na kuonyesha ya kuwa hakuwa makini katika kutekeleza maelezo ya mwenyekiti wa kikao hicho.   
   
Tunasubiri changamoto nyingi katika bunge hili lililosheheni vijana wengi kuliko bunge lililopita wakiwamo vijana wa miaka 24 walioingia hivi karibuni.  
  
Hata hivyo, Stephen Wasira wa CCM, bado anashikiria rekodi ya kuingia bungeni akiwa kijana zaidi wakati huo akiwa na miaka 23 tu. na kwa sasa yupo bungeni kwa zaidi ya miaka 40.

Wednesday 10 November 2010

Barack Obama wins Indonesian Hearts

Barack Obama's visits to Indonesia was cheered by this largest moslem country in particular at his short speech which he expressed his Indonesian life memories when he was a young boy at Indonesia (aged 6 - 10 years popularly known as Barry by then).   
  
He won the hearts of Indonesian people when he spoke some phrases of local language. He added that he was had great affection with Indonesia people in particular by having an Indonesian half sister (Indonesian-American).  
  
Obama, also applause Indonesia for extraordinary democratic transformation and refer it as an example in the world.  
   
He also focus on Indonesia economic growth and high degree of tolerance between reliogions while the country is dominated by moslems. He, further, was keen to strengthen the economic ties USA has reached with Indonesia.  
  
The overwhelmed Indonesian was evidenced through twiter messages to congratulates Obama, considering that Indonesia is the second largest Twiter user in the world.  
  
Photo from B B C

Sunday 7 November 2010

Kenya: Polisi aua watu 10 Kwa Kinachodhaniwa ni Wivu wa Mapenzi

Jumamosi usiku, Mji wa Siakago ambao upo kama km 150 kutoka Nairobi uligeuka kwa muda kuwa uwanja wa kumwaga risasi mara baada ya afisa wa polisi mmoja kwenda kwenye baa moja ikisemekana alikuwa na nia ya kumfuata rafiki yake wa kike ambaye alidhani atakuwa kwenye baa hiyo.  
   
Baada ya kumkosa alifyatua risasi humo na kuua mtu mmoja, baadaye akaenda baa ya pili na kufyatua tena risasi ambapo aliua tena mtu mmoja. Na mwisho alienda baa ya tatu, alipomkosa akafyatua tena risasi na kuua watu wanane hapo.   
    
Habari ambazo hazijathibitishwa rasmi, zinasema kati ya waliouawa, wawili ni polisi.
Chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana, ila inasemekana muuaji huyo alijisalimisha mwenyewe kituo cha polisi, na alidai alifanya hivyo baada ya kuishiwa risasi.  
  
Polisi walikuwa wamemuweka chini ya ulinzi mkali katika kituo kikuu cha polisi, Embu. 
   
Ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao walikuwa katika taharuki na gadhabu kubwa kwa tukio hilo, kiasi kwamba usalama wa mtuhumiwa na kituo alichohifadhiwa kilikuwa hatarini kushambuliwa.  
   
Polisi bado wanaendelea na uchunguzi, huku habari za rafiki wa kike wa muuaji hazijulikani, kwani katorokea mahali pasipojulikana.  
  
Watu wengi hawakuwa na habari kuhusiana na kilichokuwa kinaendelea, huku wakidhani ni sherehe za wahindu kusheherekea sikukuu ya Diwali zikiendelea, ambazo huambatana na urushaji wa fataki na milipuko.

Friday 5 November 2010

JK Mshindi wa Urais Tanzania kwa 61%

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemtangaza Jakaya Kikwete kuwa mshindi kwa kupata jumla ya alama 61.1% ya kura zote akifuatiwa na Slaa wa CHADEMA aliyepata 26.3% na wa tatu ni Lipumba ambaye safari hii kaporomoka na kupata 8%.  
  
Ushindi uliopungua wa JK haukutarajiwa na wana CCM wengi, kwani walikuwa wana imani atapata ushindi wa kimbunga wa zaidi ya 90%, lakini mambo yamebadilika kabisa.   Ikumbukwe kuwa uchaguzi wa 2005, JK alipata zaidi ya 87% ya kura zote  
   
Slaa hakuhudhuria kwenye ukumbi wa matokeo, lakini wagombea wengine wote walikuwapo.  
  
Wapiga kura Uchaguzi wa mwaka huu walikuwa 42.6% tu ya wale wote waliokuwa wamejiandikisha.

Thursday 4 November 2010

Rwandair !!!

Hivi utasijiakiaje pale shirika la ndege linapokupatia tiketi ambayo unalazimika kutumia ndege nyingine kabla ya kuunganisha na ndege yao. Halafu tarehe ya ndege yao, wanakupa siku na saa ambayo hawana safari ya kwenda huko uendako.

Shirika jingine wanapokueleza ya kuwa connection yako haiwezekani, kwani shirika waliokupa tiketi hiyo,   hawana safari muda huo!!    
Unapowarudia ofisini kwao na kuwaambia wakupe ratiba ya safari zao, wanakuambia hapo customer care, kuwa hawana ratiba ofisini, na wakati huo huo wana mtandao wanaotumia kufanya booking!! Yaani hawatanii, ndio wanakwambia ukweli.... 
  
Ukiwa bado umeduwaa, wanakuja abiria wengine wawili, tayari wametahayari na kulalalama, ya kuwa walipofika uwanja wa ndege siku 3 zilizopita, waliambiwa safari ya ndege yao imefutwa, na hivyo wakaambiwa waje leo saa 4 asubuhi, kwani ndege itaondoka saa 8 mchana. Na wakawaandikia kwenye tiketi KABISA kwa elektroniki. Alipofika saa 4 asubuhi wakafika kwa bashasha, ndio wakakuta ndege inakaribia kugusa mawingu, yaani ilipaa kama dakika 1 hivi tangu wafike. Huwezi kuamini safari zote hizo ni za kimataifa.  
  
Mimi ambaye nilikuwa nasubiri kukata tiketi, nayo ya safari ya kimataifa nikabaki mdomo wazi. Mwisho wa yote, nilipomaliza kulipa, nikapewa karatasi yangu niliyokuwa nimewapa ya maelezo yote ya abiria, na wao walikuwa wameandika kwa mkono nyuma ya maelezo yangu wakiwa wameweka na namba ya elektroniki ya tiketi yangu, wakadai printer haifanyi kazi, kwa hiyo nije uwanjani na kikaratasi hicho!!!!!!!!!!  
  
Nikaomba nitumiwe kwa barua pepe, maana niliona hicho ni kiini macho.....sasa saa 8 zimekwisha pita, bado sijapokea barua pepe yoyote, na namba za simu zetu wanazo!!!

Upo hapo, kumbe sio Bongo tu kwenye mitkas viza ..............

Wednesday 3 November 2010

Tume ya Uchaguzi Tanzania Imechoka?

Kwa mtazamo wangu, naona Tume ya uchaguzi Tanzania ndiyo inaelekea kuwa chanzo cha vurugu zote zilizotokea baada ya kupiga kura.  
  
Yote hii inatokana na kutokuwa makini kwa tume yenyewe, na kufanya kazi kwa kujiamini ya kuwa hakuna mtu yeyote atakayeweza kuwatenda kwa chochote pale watakapovuruga. Hii ni imani ya kizee, kwani ni kawaida kwetu Mzee anaposhindwa kutekeleza jambo fulani, tunamsamehe kwa misingi ya kuwa ni mzee.
  
Mapungufu yote yaliyojitokeza kwangu hayana utetezi wa msingi, suala la kusema kila siku wanajifunza halina nafasi tena, imeshatimiza zaidi ya miaka 15 tangu tume hii iundwe, na bado ati wanajifunza.   Nahisi umri wa kujifunza umeshapita kwa sasa. 
  
Walikuwa na miaka 5 ya kuandaa uchaguzi wa mwaka huu, lakini tumeshuhudia vituko na mapungufu mengi tu. 
   
  • Watu kukosekana kwenye orodha ya wapiga kura, na hivyo kunyimwa  haki yao ya kuchagua viongozi wanaowafaa
  • Kuchanganya majina na picha za wagombea
  • Kuchanganya namba za kadi za wapiga kura
  • Kuwahamisha wapiga kura kwenye vituo walivyojiandikisha bila ridhaa yao na wala bila sababu yoyote ya maana
  • Kupeleka karatasi za kupigia kura mahali pasipotakiwa
  • Kuwacheleweshea posho wasimamizi wa uchaguzi na walinzi wa vituo vya kupigia kura
  • Kuchelewesha kutoa matokeo, kwa kisingizio cha mfumo wa kurekodi matokeo, na ati miundombinu.

Ni wazi ya kuwa tume hii ina watendaji wabovu au waliochoka.
Wanapaswa kuwajibika kwa matokeo ya vurugu.
Kwa heshima yao binafsi, wanapaswa au inawabidi wapumzike sasa, kwani baadhi yao ni wazee sana kwa kazi kama hii ambayo inahitaji uangalifu mkubwa na uwezo wa kufanya kazi nyingi na kwa muda mrefu.  
  
Nina imani Filbert Bayi na Suleiman Nyambui walikuwa ni wanariadha wazuri sana wa Tanzania, lakini kwa sifa hiyo ya zamani huwezi kuwapeleka kwenye mashindano ya mbio kwa sasa, ni wazi hawatafurukuta kama utawashindanisha na wakina Kenenisa Bekele.  Labda kama unataka kupata aibu.  
  
Nina matumaini, huu ndio utakuwa mwisho wa tume hii ya Wazee wastaafu.

Monday 1 November 2010

Habari Mpya: Dk Ali Mohamed Shein Rais Mpya wa Zanzibar, Aahidi Seif Kuwa Makamu Wake

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imemtangaza Dr Ali Mohamed Shein wa CCM kuwa mshindi wa Urais wa Zanzibar kwa kupata jumla ya 50.1% akifuatiwa kwa karibu na Sheif Sharif Hamad wa CUF aliyepata jumla ya 49.1%, na vyama vingine viligawana 0.8%.

Seif Shariff Hamad alimpongeza Shein kwa kuchaguliwa kuwa rais mteule wa Zanzibar, na kumuomba atakapoanza kazi azingatie marekebisho katika timu ya tume ya uchaguzi, akitolea mfano kwa baadhi ya watendaji wa tume ambao walikuwa wakiharibu kwa makusudi shahada za kupiga kura hasa za watu waliokuwa wanahoji ukiukwaji wa maadili na sheria za uchaguzi zilizokuwa zinafanywa na watendaji hao. Na pia alimuomba rais mteule atambue kuwa hakuna msindi wala mshindwa, kwani ushindi ni wa Wazanzibari wote, na kumuomba rais mteule aongee na wenzake awasihi kuacha kubezana hasa baada ya utangazaji wa matokeo haya, kwani yanaweza kuleta mtafaruku.  
   
Na mwisho, alimwombea heri Rais mteule kwa Mungu ili amwongoze katika kazi zake, na kisha alikwenda kumpa mkono.   
Kusema ukweli, huu ni mfano mzuri wa kizalendo na kiungwana kwa mshindwa kukubali matokeo na kumpongeza aliyeteuliwa.   

Shein naye katika hotuba yake, baada ya kuishukuru tume na wagombea wenzake, amekiri kuwa kazi ya kuwania urais haikuwa rahisi, na ushindi wake anajua ya kuwa una changamoto za juu zinazomsubiri, na inahitaji busara kubwa katika kutekeleza uongozi mpya.  
   
Pia alijigamba kuwa hakubahatisha kugombea nafasi ya uongozi wa Zanzibar, kwani alikuwa anajiamini na alijua kuwa kazi hii angeiweza japo ni alitambua kuwa ni ngumu.  
  
Pia alimshukuru sana Maalim Saif Shariff Hamad kwa hotuba yake fupi na nzito, na amefarijika sana kutokana ana changamoto aliyoitoa Maalim, naye ameahidi kushirikiana na wazanzibari wote katika serikali mpya ya umoja wa kitaifa. Na Dk Shein, ameahidi kuisimamia serikali ya umoja wa kitaifa akishirikiana na Maalim Seif kama makamu wake.  
   
Shein ameahidi kuhakikisha kutakuwa na utulivu kama ulivyokuwa kabla ya uchaguzi, na kuwataka wazanzibari wafurahi wote kwa pamoja na kuijenga Zanzibar.

Cheo cha waziri kiongozi sasa ni kwa heri....

Mimi Nasubiri ya huku Tanganyika!!!

Sunday 31 October 2010

Miss World 2010: Miss USA, First Runner: Miss Botswana, Second Runner: Miss Venezuela

Mashindano ya Mrembo wa Dunia yaliyofanyika jana Sanya, nchini China yamemalizika kwa Mrembo wa Marekani, Alexandra Mills kuibuka mshindi, na kufuatiwa na Mrembo wa Botswana, Emma Wareus na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Mrembo wa Venezuela, Adriana Vasini.  
  
Warembo wengine waliofanya vizuri katika mashindano hayo ni pamoja na Mrembo wa Kenya na wa Namibia  
   
Mrembo wa Tanzania alikwenda kushiriki katika mashindano hayo. Ila amepata cheti cha ushiriki kama walivyopata warembo wengine wote walioshiriki.  
    
Photo from missworld

Saturday 30 October 2010

Yemen: Seems to be the New Head-quarter of Al-Qaeda Now

Two parcels originating from Yemen were intercepted at Britain and Dubai while they were on their way to Chicago.  These bombs were targeted to the Jewish authorities.  
  
At Dubai, a bomb was found hidden in a printer and professionally, a closed circuit was connected to a mobile phone chip inside that printer.  
   
The parcels were sent using different internation carriers, UPS and FeDex companies. 

Read more details at this link

Friday 29 October 2010

Tafakari, Halafu Toa Jibu

Jamani, nilisema sitoi tena mambo ya uchaguzi, lakini kuna mtu amenichokoza na picha hii.

Natamani ningemjua aliyepiga au aliyeitoa hewani picha hii ili nimnukuu na kufuatilia wavuti au tovuti yake. 

Nahitimisha Habari za Kampeni za Uchaguzi 2010 Tanzania

Siku za kampeni za kisiasa Tanzania zinaelekea ukingoni.
Wasikilizaji tumefaidika sana katika kusikiliza sera mbalimbali za vyama vya kisiasa vinavyowania nafasi za kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao. Sera nyingi zimekolezwa chumvi kupita kiasi.
Ahadi zisizo na kifani na zenye matumaini ya maendeleo kwa wananchi wote!
Yaani, kama mtoto aliyezaliwa leo angekuwa na ufahamu wa kutambua maneno yote yanayozungumzwa kwenye majukwaa ya kisiasa wakati huu, hakika angejiona ana bahati kubwa ya kuzaliwa kwenye nchi yenye neema sana. Ninafikiri angemshukuru sana aliyemleta katika dunia hii ya Tanzania!
Mbali ya ahadi nyingi ambazo zimeshindwa kutekelezwa kwa miaka 49 iliyopita ya uhuru wetu wa Tanganyika. Tumeshuhudia watu wakijigamba ya kuwa watazitekeleza kwa miaka 5 ijayo, hakika wengi wetu tumegundua kuwa kuna ka-ujuha Fulani vichwani mwa………
Kinachonishangaza ni mkanganyiko wa mawazo na sera za vyama vyetu, utakuta kuna chama hapo awali kilisema hakiwezi kutoa elimu ya bure, kwamba hiyo ni ndoto, wiki hii, mzito mmoja wa chama hicho hicho kaja na mpya ya kuwa watatoa elimu ya lazima, yaani ya bure hadi kidato cha nne!! Wanaoambiwa ni wananchi walewale, na makofi walipiga tena.
Wengine wanajiona ni bora kuliko wengine, na hata kujifananisha sijui na mawe au milima huku wenzao wakiwaita ni udongo au mfano wake!!!!
Wengine wanaanza kutuhumu kuibiwa kura, hata uchaguzi haujafika, na kuweka imani kwa watu kuwa kuna mpango wa wizi wa kura….
Wengine wanatoa picha kwenye vyombo vya habari kuonyesha kampeni zao za uchaguzi zinahudhuriwa na watu wengi, ukichunguza picha hizo, unakuta zimesanifiwa kwa kutumia mtindo wa kielektroniki… ha ha haaaa
Wengine wameibuka na kudai fidia za mabilioni wakidai wamekashfiwa katika mikutano ya kampeni za uchaguzi za vyama vingine….
Nina hakika baada ya tarehe 31 oktoba 2010, kuna watu hawataamini kitakachokuwa kimetokea.

Tuesday 26 October 2010

Women Tooth-Gap: Making People Crazy Now!

Photo above from msn specials
It is amazing how the world changes, it seems each feature in human body at one time become the point of attraction!

Long time ago, smiling with gaped tooth was considered a taboo, but now it is different, the beauty industry had just turned into different perceptions. Having a tooth-gap signify beauty!

Last month, on “America’s Next Top Model,” host Tyra Banks sent a 22-year-old contestant from Boise, Idaho, to the dentist to widen her gap.The beauty blogosphere has been buzzing ever since. (according to this source)


In some African countries, the tooth gap had high credibility for beauty and fertility. Some of the women had attempted to widen the gap just to attract their destinies according to the same source.

I am sure, very soon, dentists will turn their usual work into beauty-commercial services.

Read more in this link

Sunday 24 October 2010

Uchaguzi Tanzania 2010: Ni Heri au Kiama

Imebakia wiki moja tu kabla ya watanzania watumie haki yao ya kikatiba kuwachagua viongozi watakaoona wanawafaa. Ingawa sina hakika kama wengi wa wapiga kura huwa wanatafakari usemi huu.. wa kumchagua kiongozi atakayefaa, kwa maana nyingine ambaye atatimiza ndoto za jamii anayotaka kuiwakilisha.  
  
Sanduku la kura, ndio huwa linabeba siri yote ya nani kamchagua huyu, na yupi ana kura nyingi.
Kwa sisi watazamaji tunaona kijisanduku cheusi ambacho ni kama giza tu, tunasubiri kuja kutangaziwa ati kijicho bin Tamaa kashinda, na tunapiga makofi na kushangilia, yaani hatujui kwa nini tulimchagua zaidi ya kufuata upepo tu na kumeza ahadi chungu nzima bila kuangalia kama zina maslahi kwa wapiga kura.  
  
Watanzania wengi wamekuwa na hulka ya kuacha kupiga kura ati kwa kudai ni kupoteza wakati!!! Halafu wale wanaowaita ngumbaru wakipiga kura za kingumbaru na kuwashinda werevu wachache waliojitokeza kupiga kura, wale werevu ngumbaru wanakuja juu na kudai sio haki, hakushinda nk, ukiwauliza nyie mlimchagua nani, watadai kivuli (hawakupiga kura) sasa walitaka kiongozi awe hewa? Tena utakuta ambao hawakupiga kura ni wengi kuliko waliojitokeza.   Kwa nini wasiende kumuuliza huyo kivuli kwa nini hakushinda? Maana ndio chaguo lao.....   
   
Pia kuna ujinga fulani ambao watu husema .. ati ni heri ukutane na zimwi likujualo, ha ha haaa, yaani wanajua kuwa wanayemchagua kuwa ni boga tu, lakini wanaogopa kumchagua mtu mpya hata kama anaonekana yu safi kabisa. Ati wanaogopa mtafuno wake sijui utakuwaje!!  
 
Utakuta mgombea anahaidi kujenga daraja chini ya mto, na watu wanapiga makofi. Hata mgombea mwenyewe anacheka kuona haya majitu pambaf kabisa, daraja chini ya mto!!!!, yaani uchimbe chini ya mto uweke daraja, hata ukichukulia maana ya daraja haiji!  
  
Dhana ya watanzania kuogopa mabadiliko, haipo katika siasa tu, bali hata katika kufanya kazi za kimataifa, utakuta ukiwaambia njoo ujiendeleze hapa uje ujenge nchi yako baadaye kwa maarifa utakayoyapata huku, jamaa anaogopa, ati huko atapoteza kacheo kake, hata kama ni uchwara, atasingizia usalama, au hawezi kuwa mbali na mbuyu ulio jirani ya nyumba yake... yote hii ni kuogopa mabadiliko, na hivyo kila siku kukubali kuendelea kutafunwa na kazimwi kake.  
   
Ninafikiri watanzania wameweza kuwasikiliza wagombea mbalimbali wakimwaga sera zao, japo wanasiasa wajanja, wengi wamekwepa kuweka muda wa kuulizwa maswali kuhusiana na ahadi zao, ambapo nyingine ni za kufikirika tu.  
   
Mimi natoa ushauri kwa watanzania kuwa
  • Watambue kuwa kura ni siri ya mpigaji, na hakuna mtu yeyote atakayejua walimchagua nani
  • Wasiogope mabadiliko pale wanapoona yatawasaidia
  • Wawe na hulka ya kuwapima wagombea kwa yale wanayoahidi, na kama walikuwa wana nafasi hiyo kabla, wapimwe kwa yale waliyoyafanya na kama wataweza kutekeleza wanayo ahidi tena.
  • Wamchague mtu wanayefikiri ataleta maendeleo yanayoendana na eneo walilopo, sio mtu anasema atawajengea meli hapo, wakati eneo lipo kwenye sehemu ambayo hata maji ya vijito hakuna.
  • Waangalie rekodi ya uadilifu wa wagombea.
  • Watumie akili zao kutoa maamuzi na sio kuendeshwa kama punda na kubebeshwa mzigo usio na manufaa hata kidogo kwao, jaribu kufikiria punda anapobebeshwa mifuko ya sement au chumvi, unafikiri ina manufaa yoyote kwake?  
Nawatakia uchaguzi mwema hapo Jumapili ijayo. Msituangushe sisi ambao katiba yetu imetunyima uhuru wa kupiga kura.

Wednesday 20 October 2010

Here and There, Chicago

Eye Industry exhibition booths


This week, we had a meeting attended by more than 30,000 eye care teams from all over the world at Chicago, IL. It was an interesting experience! Something terrible to us was cold. ...
Green market at the heart of Chicago, masoko haya ni kama magulio ya huko kwetu nyumbani, kwani wakulima wanaleta mazao yao na kuyauza, wanayakuza bila kutumia mbolea wala virutubisho vya bandia. Lakini ... nyumbani si ndio muda wote tunatumia mbolea asili.....

Mihangaiko ya mitaani tu, usishangae mitaa kuwa mitupu, kibaridi si mchezo.


 Nilipita pita maeneo ya Cook County, ambapo Barack Obama alikuwa anaishi, na mtaa katika picha hii ya chini unaoitwa Ellis, kwa mbele kidogo, ndio kuna nyumba aliyokuwa anaishi Obama, kuna ulinzi mkali japo hauna mtu anayeishi katika nyumba hiyo, ilikuwa imepambwa na masanamu ya haloween!!
Sehemu hii ndio pekee nilipokuta walinzi wa jadi, au ukipenda community security, ambao walikuwa wapo wengi mtaa wa 51 ambako ndipo kuna nyumba ya Obama. Maeneo haya wanaishi watu wengi wenye asili ya Uafrika, ila .. duh, kuna sehemu nyingine, watu kaustaraabu wamekasahau.....
Bustani ya kupumzika Cook County, nje kidogo ya katikati ya jiji la Chicago, IL.

Sunday 17 October 2010

Will Come out Soon.

I have extreme busy schedule here at Chicago, IL, Scarse time to sleep, too many nyama choma and roast, too much desert receptions. Enormous sweet cookies, raw fish!!!, ma-salad, kama kambuzi ati..., kahawa ya barafu huku mmewasha heater ndani!!! Nyie watu wa huku mnapenda sana kumimina chakula ndani ya tumbo..... ''' He! halafu mnadai kunywa diet Coke, wakati cookies zina sukari kama asali!!... hii ni ..... n'bangue, kwa wale wanaojua hapo mmenipata!

I am optimistic, once I settle, I will be able to have fun with my posts. Let me enjoy Chicago first.

Being retina physian.... interesting.
Hey! Gotta many interested parties, scholarship available..., assisted programmes and funds on hand... any one interested pse!! Just have masters in ophthalmology first, then contact me, I mean for Rwanda and Tanzania. ASAP, expiring date just at the tip of my fingers. Hope it will not fall on damn deaf ears and blind eyes!!

Friday 15 October 2010

Bado nipo nipo!

Huu ndio usafiri wangu wa kila siku wakati nikielekea mitaani na sehemu nilizopangiwa kufanya kazi za abunuwasi.
Nilikuwa nikihisi wenzetu wanatoa huduma za hali ya juu, na hakuna kuchapia uongo kwa wagonjwa wao... lakini wapi bwana, wakichemsha wanapiga fiksi hizo...., halafu mgonjwa akitoka, wanakuambia, hapo kazi ilitushinda... alas!
Nilichogundua wana tumajungu, na kusagiana!
Wagonjwa wa macho, nilikuwa naona nyumbani wanapiga foleni ya mwaka, lakini na huku, watu wasubiri masaa 2-3 kumaliza, wagonjwa wakiombwa msamaha, wanadai hakuna shida, wenyeji wakitoka, utaona mtu anakuambia ati hao madokta ni bull-shit nk, duh.. kuwa mgeni mahali, unakuwa rafiki wa kila mtu




Nilipata wasaa wa kufika Staten Island, na pia kufika kwenye statue of Liberty, japo giza lilikuwa limeanza kuingia..... well, well, it was a greaqt experience to visit these sites  across Hudson  river
Picha hiyo hapo juu sio Shanghai au mji wowote wa China, bali mji huu upo New York, na unaitwa "China Town", Karibu 90% ya wafanyabiashara hapa ni wachina, bei za vitu zipo kwa yuan, na kuna kila kitu kinachopatikana China kuanzia vyakula, mavazi, hata na watu hapo karibu wote ni wachina, na kuna wengine hata kiingereza hawajui, lakini wapo na wanafanya biashara.......!!




Duka kubwa la apple ambalo liko chini ya ardhi, watu hapo....... kila mtu ananunua i-phone, i-pod, i-pad nk. Kununua unajipanga foleni kama nusu saa, mind you, that there sales people like 20 and they are very fast...


Kama kawaida, unapofanyia kazi au kupitisha muda wako mwingi, hukosi marafiki, wengine utadhani mlikuwa mnafahamiana siku nyingi....., hapa ni katika hospitali moja ya macho maarufu kwa tiba ya wagonjwa wenye shida ya retina katikati ya jiji la New York. Well, these were my colleagues, they are residents, on the left is from Montana state- US, Middle - from Portugal. We went along very well.....

Monday 11 October 2010

New York Slices


Time square at night

Museum near the Park - NY

Jumba la Makumbusho - NY

12 - 13th Century Chinese products

Below: Grand station for subway trains in NY

Wednesday 6 October 2010

At times....Out of Network. Kumradhi Wakuu

I am on the cruise to nearly extreme north and then to the extreme west. Accessing inernet and other communications is frequently interrupted or prohibited. But, whenever I get time...

Nipo kwenye harakati za safari, kwa muda nitakuwa kwenye mazingira ya kuzima simu, ati jamaa wanadai wakati wanaendesha vyombo vyao au ungo wa kizungu, hawataki abiria wawe wanawasiliana kwa simu.
Wanadai kelele za simu zinaingilia mitambo yao.

Nikiweka kituo mahali popote, nikaweza kuwasiliana nanyi marafiki zangu, nitakuwa nikikohoa.
Kwa sasa nasikiliza hotuba ya Odinga!!