Member of EVRS

Friday, 29 October 2010

Nahitimisha Habari za Kampeni za Uchaguzi 2010 Tanzania

Siku za kampeni za kisiasa Tanzania zinaelekea ukingoni.
Wasikilizaji tumefaidika sana katika kusikiliza sera mbalimbali za vyama vya kisiasa vinavyowania nafasi za kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao. Sera nyingi zimekolezwa chumvi kupita kiasi.
Ahadi zisizo na kifani na zenye matumaini ya maendeleo kwa wananchi wote!
Yaani, kama mtoto aliyezaliwa leo angekuwa na ufahamu wa kutambua maneno yote yanayozungumzwa kwenye majukwaa ya kisiasa wakati huu, hakika angejiona ana bahati kubwa ya kuzaliwa kwenye nchi yenye neema sana. Ninafikiri angemshukuru sana aliyemleta katika dunia hii ya Tanzania!
Mbali ya ahadi nyingi ambazo zimeshindwa kutekelezwa kwa miaka 49 iliyopita ya uhuru wetu wa Tanganyika. Tumeshuhudia watu wakijigamba ya kuwa watazitekeleza kwa miaka 5 ijayo, hakika wengi wetu tumegundua kuwa kuna ka-ujuha Fulani vichwani mwa………
Kinachonishangaza ni mkanganyiko wa mawazo na sera za vyama vyetu, utakuta kuna chama hapo awali kilisema hakiwezi kutoa elimu ya bure, kwamba hiyo ni ndoto, wiki hii, mzito mmoja wa chama hicho hicho kaja na mpya ya kuwa watatoa elimu ya lazima, yaani ya bure hadi kidato cha nne!! Wanaoambiwa ni wananchi walewale, na makofi walipiga tena.
Wengine wanajiona ni bora kuliko wengine, na hata kujifananisha sijui na mawe au milima huku wenzao wakiwaita ni udongo au mfano wake!!!!
Wengine wanaanza kutuhumu kuibiwa kura, hata uchaguzi haujafika, na kuweka imani kwa watu kuwa kuna mpango wa wizi wa kura….
Wengine wanatoa picha kwenye vyombo vya habari kuonyesha kampeni zao za uchaguzi zinahudhuriwa na watu wengi, ukichunguza picha hizo, unakuta zimesanifiwa kwa kutumia mtindo wa kielektroniki… ha ha haaaa
Wengine wameibuka na kudai fidia za mabilioni wakidai wamekashfiwa katika mikutano ya kampeni za uchaguzi za vyama vingine….
Nina hakika baada ya tarehe 31 oktoba 2010, kuna watu hawataamini kitakachokuwa kimetokea.

4 comments:

John Mwaipopo said...

... such a good recap.

John Mwaipopo said...

... such a good recap.

Upepo Mwanana said...

Shukrani, jumapili tupo vituoni tayari kabisa

mumyhery said...

Mungu Ibariki Tanzania