Member of EVRS

Friday, 29 October 2010

Tafakari, Halafu Toa Jibu

Jamani, nilisema sitoi tena mambo ya uchaguzi, lakini kuna mtu amenichokoza na picha hii.

Natamani ningemjua aliyepiga au aliyeitoa hewani picha hii ili nimnukuu na kufuatilia wavuti au tovuti yake. 

8 comments:

Subi said...

Pengine kura yake ya Uraisi anampa Kikwete na kura ya Ubunge anampa Mnyika.

Ama pengine anavaa na kubeba bango kuchanganya watu, anawazuga, siri yake ipo ndani ya moyo wake.

Ama amedata na anadatisha wengine.

chib said...

Swali moja, majibu mengi, ha ha haa, natania hapo. Lakini Subi, nimekubali brain yako bado moto!

SIMON KITURURU said...

Subi katekenya nilichofikiria.

Au jamaa hiyo ni kazi tu kwahiyo kwenda Morogoro atapiga debe watu wapande Abood Basi na Abood likiondoka anageuza kibao na kupigia debe HOOD basi yote ikiwa ni katika kuhangaikia ngawira pesa ndani ya siku.

chib said...

Yup mtakatifu. Kumbe upo makini

Upepo Mwanana said...

Hii ni ya aina yake!
Mimi naona ni ajira tu, akimaliza hapo, chap chap anaenda kampeni za chama kingine na kukusanya kidogo kidogo

chib said...

@ Upepo...Yawezekana

Faustine said...

....Wanaitwa madalali wa kisiasa.....

Anonymous said...

Kumbe siasa nayo ina udalali?