Member of EVRS

Sunday, 30 May 2010

Kukosa Haki ya Msingi Kwenye Blogu

Ugonjwa wa blogu ya Mwananchi Mimi umehamia kwangu leo!!!!

Nimekwama kutoa mawazo yangu (my comments) kwenye blogu zote nilizotembelea, hata kujibu maswali yenu.... Nimenuna huyo :-(

Hakika nimekosa haki yangu ya msingi ya kuachia ujumbe wangu kwenu wasomaji
Natumaini punde itakuwa shwari.

Nawatakia jumapili njema, japo nimechelewa kidogo kwenu ninyi mnaoishi karibu na greenwich meridian.

Friday, 28 May 2010

The Perfect Thief

This friday.. I want to give you a funny tale, ha haaa haaa

I cant wait, but is a story of a parrot who guide the house from the thief.

Just visit this site to laugh, ha ha haaa

I suffered worthless theft from my house-keeper :-(

Sasa tuache utani, wiki hii yaani imenitia simanzi kabisa, nimeshindwa kuikalia blogu hii kwa sababu ya tukio la wizi, duh!! Polisi wa Afrika mashariki.. aaah wote wako sawa tu katika kuwajibika. Hata kama hawaombi rushwa, lakini kuzungusha na njoo kesho, njoo kesho :-( wanakuchelewesha kupata RB tuuuu wakati wewe unataka kuishia hapo
Ikitokea ukaibiwa na mtu unamfahamu na kumuamini, wakati mwingine inashangaza na kukaa unacheka tu, he he heee

Mwenzenu yamenikuta baada ya kukutana na mtu aliye na fani ya kuwa mwizi au mdokozi . Kijana aliyekuwa anaaminika kwa uaminifu na ushamba, ukimpa pesa kanunue kitu, anakurudishia mpaka senti tano. Ukimtuma kitu cha 5000 aka-bargain kwa 3000 anakurudishia chenji yote
Ukisahau coin kwenye mfuko anakuletea. Kwa miaka 8 hajawahi kubadili tabia.

Nimeachiwa kijana huyu miezi 10 iliyopita kwa sifa tele, na kweli alidhihirisha kuwa ni mtu safi kwa muda wote.

Lakini sijui kwa nini roho yangu ilikuwa inasita kufungua pazia la uaminifu wote kwa muda niliokuwa naye, na hivi karibuni niliamua kuwa muangalifu zaidi.
Lakini wapi bwana, jumanne wiki hii nikiwa kazini na nimefunga milango yote ya nje, ila ya ndani niliacha bila kufunga na funguo, na yeye akiwa kwenye servant qtr yake huko nje, kwa nini asinilize pesa zote nilizoacha chumbani, cha ajabu kakomba pesa za kitanzania, faranga za Rwanda na kuacha dola na shilingi za Kenya wakati zilikuwa pamoja!!
Kinacho niacha hoi zaidi, nusu ya faranga zote zilizokombwa zilikuwa sehemu ya mshahara wake!! ambao alikuwa hajachukua kwa maombi yake mwenyewe.

Mwisho wa siku, nimegundua sehemu alipopitia, kama huna ujuzi wa kuangalia hakika usingeweza kutambua, yaonekana hiyo kazi aliifanya kwa muda mrefu, na taratibu. Aliweza kutengeneza njia yake ambayo anaweza kuingia na kutokea ndani kisha kutoka nje tena, hakika sikudokezi ni wapi, maana mwingine anaweza kusoma hapa akaja akakuliza na wewe.....

Kwa ufupi, kijana mwenyewe hajulikani alipo kwa sasa...

Nimejifunza kufanya ukaguzi wa mara kwa mara.

Kinachoniudhi sasa! Kupata namba ya shauri. Ma- arufonsi wa huku hawajali time, sasa siku ya 3 eti bado niende kesho. Halafu kitu kidogo huku wala hawana habari kabisa. Hata kondoo wengine wakiambiwa subiri hapo wanakaaa masaaa yoote, mie nilikuwa sitoki mbali na mlango mpaka inabidi wanisikilize alaaaaaaaa!

I wish a lovely weekend. Usiseme pole, toa onyo ndugu weee, ili nikomae zaidi au vp?

Tuesday, 25 May 2010

Umoja Wa Watanzania Wanaoishi Rwanda: UTARWA wapata Viongozi

Takribani wiki 2 zilizopita, Watanzania waishio Rwanda tumeweza kufanikisha kuunda umoja wetu ambao unajulikana kwa kifupi kama UTARWA.
Jumuiya hii iko chini ya ulezi wa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda. Jumuiya hii au umoja huu uko mbioni kusajiliwa na una madhumuni makuu ya kuwakutanisha Watanzania waishio Rwanda, na pia kupeana taarifa na kusaidiana pindi Mwanachama anapopata tatizo lolote.
Zoezi la kuandikisha wanachama likiendelea kabla ya kuanza mkutano


Wajumbe wakipitia rasimu ya katiba ya jumuiya kabla ya kuifanyia marekebisho ya mwisho na kuipitisha

Wajumbe wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Dr Matiko Chacha Marwa ambayo aliitoa baada ya kupata viongozi wa Jumuiya.
Katika mambo aliyoyasisitiza ni kuwasihi Watanzania kuchangamkia fursa ya kufanya biashara Rwanda ambako kuna soko kubwa la bidhaa za Tanzania kwani zina viwango vya ubora wa hali ya juu kuliko bidhaa nyingi hapa.
Balozi Marwa Alitoa ushauri kwa watu wajihamasishe na kusambaza taarifa za kuja Rwanda kufanya biashara, na pia alisisitiza ya kuwa Serikali ya Rwanda imefungua milango kwa wanajumuiya ya Afrika Mashariki kuingia Rwanda na kufanya shughuli halali bila kulipia viza.
Viongozi wa UTARWA chini ya mwenyekiti Josephine Marealle-Ulimwengu (wa sita kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na mhesh Balozi Marwa (Wa tano kutoka kushoto)


Mambo yakiendelea baada ya mkutano, wajumbe wakiendelea kukifumua kiswahili kwa furaha, kama aonekanavyo mdau mkuu wa blogu hii (mwenye kofia maalumu ya Tanzania) akiteta jambo kwa furaha :-)

Sunday, 23 May 2010

Eritrea Women Football Team: German trip Was Helpful!!!

National football team for Eritrea (Women) had a shocking 8 – 1 defeat from their Tanzanians opponents.

This game was played in Dar es Salaam today.
The game was almost one sided, but at least Eritrea manage to get their lone goal during the injury time of the second half.

It should be remembered that Eritrean team was in Germany for about a month where they went there for training as preparations for this game. Probably this training had helped them at least to reduce the number of goals, otherwise they could have been beaten heavily.

The return leg will be held in Asmara two weeks from now by which Eritrea will have to score 7 – 0 if they want to qualify for the finals of African Women Football Championship in South Africa shortly after the world cup this year.

My advice to Eritrea, probably they should go to Italy now to learn how to defend their goal! :-(

Twiga Star Hoyeeee!

Saturday, 22 May 2010

Tangazo la Leo!

Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda(Pichani) inawakaribisha watanzania wote wanaotaka kufanya biashara Rwanda.

Wanatoa ushauri wa bure kwa wanaotaka kufahamu zaidi sehemu za kuwekeza au kufanya biashara hasa kwa bidhaa zinazotoka Tanzania.

Waweza kuipata ofisi hii kwa Simu namba +250 252505400

Wish you a nice Saturday!

Thursday, 20 May 2010

Wars and Alternative Dwellings

I have no comment!!
Thanks Mdau Wa London for Captions.

Tuesday, 18 May 2010

Always: Take a Closer Look

Watu tumezoea kuchukulia kitu au kuangalia kitu kijuujuu tu, na wala hatuchukui muda kuchunguza kwa ukaribu. Tunafikia kutoa maamuzi bila kuangalia kwa undani!!
Je, ulishawahi kutafakari kile ukionacho na kujua ya kuwa muonekano wake hautoshi bila kukichunguza na kujua kimebeba taswira gani


Kuvamia kitu kijuu juu tu kunaweza kukufanya uingie matatani.
Joto ya jiwe......... aijuaye......
Siku njema :-(

Monday, 17 May 2010

Tanesco: Life is not Cheap!


The word "Life" to Tanesco doesnt means that is a cheap stuff, but rather ... worthless.
These cables have been like this for many months.
Cha kushangaza ni kuwa zina umeme, jamaa wakipita mitaa hiyo, wanasisitiza watu wakate miti karibu na nyaya, lakini wao kurekebisha hili tatizo......
These creatures working at Tanzania No Electricity and Services Company... are the deadly crooks!!

Friday, 14 May 2010

Coming Back Soon

I am out and away from my network station.
Irregular posting Is innevitable.

Nina matumaini ya kurudi tena kwenye mmeng'enyuo wangu wa kawaida muda si mrefu.

Have a nice day

Monday, 10 May 2010

Hmhmm!!!! Tulikotoka?

When I was going through different blogs...... I came to realise that to acquire knowledge you don't need to go to the class.....
Blogging is more than going to the classes, at least that is what I can say......


Au wewe wasemaje
Kazi ya pitapita kwenye vibaraza vya watu, shule weeee..... za uswekennnnnn


Sunday, 9 May 2010

Chelsea Massive Roars as They Clinch Barclays Premier League Championship

They thrashed Wigan 8 - 0
The first team to score over 100 goals in premiership within one season, they scored 103 Didier Drogba emerges as top scorer with 29 goals
He scores a hat-trick on the second half
Big applaud from Ivory Coast and Kikwete!
Man U missed the championship by just one point only,
They just met this shield at the door!!

Probably bad day for Tottenham when they were beaten 4 - 2 by relegated Burnley. Burnley came from behind 0 - 2 and scored 4 times to win the match.
Congratulatios Chelsea despite that I am not a Chelsea fan!

Simba yapoteza Mechi Misri 5 - 1

Timu ya mpira wa Miguu ya Simba, ambayo ndio mabingwa wapya wa ligi kuu ya Tanzania Bara, kwa mara ya kwanza wikendi hii imeonja machungu...... baada ya muda mrefu wa kucheza mechi za ndani na za kimataifa bila kufungwa, wikendi ihii meweza kufungwa kwa idadi kubwa ya magoli kwa jumla ya 5 - 1 na Hodoud ya Misri kwenye michezo ya kuwania kombe la shirikisho barani Afrika.

Kipigo hiki kimeifanya itolewe kwenye mashindano hayo kwa jumla ya mabao 6 - 3, kwani Simba ilipata ushindi wa mabao 2 - 1 wakati wa mechi ya mkondo wa kwanza iliyochezwa Dar es salaam majuma mawili yaliyopita.

Hii ni mara ya kwanza kwa simba kufungwa mabao mengi kiasi hiki kwa mechi za kimataifa nchini Misri, kwani Simba imekuwa na rekodi nzuri kuliko Yanga kwenye mechi na timu za Misri.

Friday, 7 May 2010

England 2010 Elections: Conservative Emerges as Top Winner in Parliamentary Seats

David Cameron's Conservative Party has won the majority of votes and Parliamentary seats in UK 2010 elections.
Conservative won 307, followed by Labour Party with 258 seats and Liberal Democrats 57.

At this time seniour members of Conservative and Liberal Democrats (Not Parties Leaders) are under negotiations to form a coallition of their parties, which will enable them to form a minority government.

Labour Party Receives Another Big Blow

It is obvious now that Labour party of England has lost mandate to form a government from the results which are coming in.

So far Conservative has won 289 seats, Labour 245 and Liberal Democrats has 51 seats.

Few minutes ago, Nick Clegg, the leader of Liberal Democrats has announced that he believes that the Party which has majority of seats, should be given chance to form the government. He further, strengthen his speech by saying that he do believe Conservative will prove that is capable of joining hand with other parties to form a government for the benefit of all people in England.

This is a clear blow to Labour party, it is unlikely that Liberal Democrats will form a coallition Government with Labour, but rather ready to do so with Conservative.

The final results are expected later today.

Thursday, 6 May 2010

Today's Living Message: Water SecrecyHad you ever asked yourself the secret under the WATER?

Most of the time we see WATER just over its surface, but we rarely wonder what does actually WATER hide from our eyes.

WATER bodies constitute largest percentage of Earth surface.
Saline WATER constitute larger portion of water bodies
Even in human being, our bodies have larger proportion of WATER as compared to other elements.

Almost nearly all living creatures on our planet need WATER for survival and replication.
In most areas, WATER just comes to the surface of the planet at no human effort, and it flows around to nourish the living objects.
Larger WATER bodies have millions of species living within it, and without WATER, they will not survive for a longer time!

Human being needs WATER too, and without WATER, human beings will not survive long.
Without WATER, there is no life for human being, but also there is no life for human if they attempt to live under WATER.

Message to take: Almost everything has good and bad sides. Stick to the LIMITS, you will be the most successful person.

Wednesday, 5 May 2010

Kenya yasamehewa na Dubai!

Serikali ya Muungano wa Falme za Himarati (United Arab Emirates) umeondoa kizuizi kwa wakenya kwenda Dubai kwa sharti kuu la kuwa ni lazima wawe na angalau shahada moja.
Kizuizi hiki kiliwanyima wakenya wengi fursa ya kufanya biashara kati ya Kenya na Dubai hasa kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ambao huwa ni wengi.


Mzozo huu ulikuja kutokana na makosa ya maofisa wa uhamiaji wa Kenya kuwatimua watalii kutoka Dubai kwa tuhuma kwamba ni magaidi. Kati ya waliotimuliwa ni pamoja na watu wa jamii ya Kifalme ya Himarati.

Viongozi wa kiserikali wa Kenya walihaha sana hadi kufikia muafaka, kwani ilikuwa inahatarisha ajira za wakenya wengi walioajiriwa Dubai ikiwa ni pamoja na shirika la ndege la Falme hizo la EMIRATES ambalo limeajiri maelfu ya wafanyakazi amabao ni wakenya kuliko idadi ya wafanyakazi wote wa shirika la Kenya Airways.

Serikali ya Kenya ilikuwa na haki ya kuwajibika kutokana na uzembe na uamuzi mbovu wa maafisa wake.

Tuesday, 4 May 2010

JK Atangaza Azma ya Kugombea Tena Muhula Mwingine

Jamani natoka nje ya mada kidogo.

Jana nilikuwa nasikiliza hotuba ya Mh Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alipokuwa anaongea na ati wazee wa Darisalama.

Lakini cha ajabu watu wa tivii waliamua kututangazia hata na sie ambao sio wazee wa darisalama, achana mbali na umri wetu kama tuna sifa za kuitwa wazee au la.
Mbali ya kuwakanyaga kanyaga viongozi wa TUCTA kwa maneno yao na kuwaita ya kuwa ni waongo… err na kadhalika.

Lakini watu walikosa pointi aliyotaka kuiweka hadharani, pamoja na kuwa kazungumzia kidogo tuuuu, lakini wenye masikio walisikia.
Ni pale alipokuwa anasema ya kuwa viongozi hao wa TUCTA walikuwa na nia ya kumnyima kura uchaguzi utakapofika. Hizi zilikuwa salamu kwa wanachama wa chama tawala ya kuwa jamani eeeh, ninagombea tena kiti hikiiii, hi hi hiii. Wazeee hoyeee, hi hi hiii.
Sasa narudi katika mada……

Mheshimiwa Rais alionekana kuwa mkali na asiye na masihara katika kazi, mimi sina la kuchangia hapo, kwani hata nikipiga kelele nani anayenisikiaaaa…
Lakini ningependa kusikia sana Rais huyo huyo akikemea kwa ukali ule ule na kuchukua hatua kwa mafisadi ambao ushahidi upo wa jinsi walivyokomba mali za watanzania kwa manufaa yao binafsi, tena ni wachache sana ukilinganisha na hao sungusungu wanao omba kuongezewa kima mshahara.

Kisu kiwe na makali pande zote hapo utashinda na kukoga nyoyo za wengi. Mambo ya kusema asilimia 15% hata ufanyeje hawatakupenda mhhhhhhhh!!!!

Sunday, 2 May 2010

Jumapili Njema!

Siri ni ya mtu mmoja tu.

Epuka ushawishi wa kibonzo hiki. Just have fun

Jumapili njema, eerrr have a nice sunday!