Member of EVRS

Tuesday, 25 May 2010

Umoja Wa Watanzania Wanaoishi Rwanda: UTARWA wapata Viongozi

Takribani wiki 2 zilizopita, Watanzania waishio Rwanda tumeweza kufanikisha kuunda umoja wetu ambao unajulikana kwa kifupi kama UTARWA.
Jumuiya hii iko chini ya ulezi wa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda. Jumuiya hii au umoja huu uko mbioni kusajiliwa na una madhumuni makuu ya kuwakutanisha Watanzania waishio Rwanda, na pia kupeana taarifa na kusaidiana pindi Mwanachama anapopata tatizo lolote.
Zoezi la kuandikisha wanachama likiendelea kabla ya kuanza mkutano


Wajumbe wakipitia rasimu ya katiba ya jumuiya kabla ya kuifanyia marekebisho ya mwisho na kuipitisha

Wajumbe wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Dr Matiko Chacha Marwa ambayo aliitoa baada ya kupata viongozi wa Jumuiya.
Katika mambo aliyoyasisitiza ni kuwasihi Watanzania kuchangamkia fursa ya kufanya biashara Rwanda ambako kuna soko kubwa la bidhaa za Tanzania kwani zina viwango vya ubora wa hali ya juu kuliko bidhaa nyingi hapa.
Balozi Marwa Alitoa ushauri kwa watu wajihamasishe na kusambaza taarifa za kuja Rwanda kufanya biashara, na pia alisisitiza ya kuwa Serikali ya Rwanda imefungua milango kwa wanajumuiya ya Afrika Mashariki kuingia Rwanda na kufanya shughuli halali bila kulipia viza.
Viongozi wa UTARWA chini ya mwenyekiti Josephine Marealle-Ulimwengu (wa sita kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na mhesh Balozi Marwa (Wa tano kutoka kushoto)


Mambo yakiendelea baada ya mkutano, wajumbe wakiendelea kukifumua kiswahili kwa furaha, kama aonekanavyo mdau mkuu wa blogu hii (mwenye kofia maalumu ya Tanzania) akiteta jambo kwa furaha :-)

11 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kusaidiana wakati wa matatizo!! mna matatizo sana huko ehe??

EDNA said...

Hongereni kwa kupata uongozi mpya.

chib said...

Kumradhi: Ni Kusaidiana kwa mambo yote..

Yasinta Ngonyani said...

Hongereni sana kusaidiana ni maja ya maisha hapa duniani na pia hongera kwa kupata uongozi mpya.

mumyhery said...

Hongereni sana kwa kuunda umoja na kupata viongozi, nawatakia kila yalio mema

SIMON KITURURU said...

Hivi kwa Makisio Rwanda kuna kama Watanzania wangapi?


Hongereni kwa kujipanga!

Maisara Wastara said...

mwanzo mzuri, tunwaombea kila la kheri

Maisara Wastara said...
This comment has been removed by the author.
kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mambo gani?? ngoja niishie hapa maana!! kuna mambo ambayo hamwezi kusaidiana tusidanganyanye!!

Upepo Mwanana said...

Hongereni sana.
Kamala tukuzoea.. Mr Controversial, he he hee

Faustine said...

Hongereni sana! Mama Ulimwengu ni kiongozi mahiri. Mpeni sapoti.