Member of EVRS

Tuesday, 4 May 2010

JK Atangaza Azma ya Kugombea Tena Muhula Mwingine

Jamani natoka nje ya mada kidogo.

Jana nilikuwa nasikiliza hotuba ya Mh Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alipokuwa anaongea na ati wazee wa Darisalama.

Lakini cha ajabu watu wa tivii waliamua kututangazia hata na sie ambao sio wazee wa darisalama, achana mbali na umri wetu kama tuna sifa za kuitwa wazee au la.
Mbali ya kuwakanyaga kanyaga viongozi wa TUCTA kwa maneno yao na kuwaita ya kuwa ni waongo… err na kadhalika.

Lakini watu walikosa pointi aliyotaka kuiweka hadharani, pamoja na kuwa kazungumzia kidogo tuuuu, lakini wenye masikio walisikia.
Ni pale alipokuwa anasema ya kuwa viongozi hao wa TUCTA walikuwa na nia ya kumnyima kura uchaguzi utakapofika. Hizi zilikuwa salamu kwa wanachama wa chama tawala ya kuwa jamani eeeh, ninagombea tena kiti hikiiii, hi hi hiii. Wazeee hoyeee, hi hi hiii.
Sasa narudi katika mada……

Mheshimiwa Rais alionekana kuwa mkali na asiye na masihara katika kazi, mimi sina la kuchangia hapo, kwani hata nikipiga kelele nani anayenisikiaaaa…
Lakini ningependa kusikia sana Rais huyo huyo akikemea kwa ukali ule ule na kuchukua hatua kwa mafisadi ambao ushahidi upo wa jinsi walivyokomba mali za watanzania kwa manufaa yao binafsi, tena ni wachache sana ukilinganisha na hao sungusungu wanao omba kuongezewa kima mshahara.

Kisu kiwe na makali pande zote hapo utashinda na kukoga nyoyo za wengi. Mambo ya kusema asilimia 15% hata ufanyeje hawatakupenda mhhhhhhhh!!!!

6 comments:

John Mwaipopo said...

du, most of us have been busying ourselves challenging the rather tyrannising speech. little did we know he was letting the dar' stalwarts know that he is on the mark.

Anonymous said...

:-)

I never thought about that. Politicians bwana!!

Fadhy Mtanga said...

...mimi pia sikufikiria mbali hivyo. Kaka bora umenigutua. Lakini jana nilikuwa disappointed totally. Sisemi kwa nini.
Lakini uzuri wake keshasema hana shida na kura zetu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ameshiba kura zenu za kitoto hapendi.

subiri akianza kupita na bakuli la kura

chib said...

Kamala umesema ukweli, wakati wa kuomba kura, hata goti utapigiwa, na ikibidi kachozi kamwagike ili utoe huruma yako ha ha haaa

Bwaya said...

Kuna mechanism tusiyoijua iko kazini. Pamoja na yote haya bado utashangaa atalamba kura zote. Kuna kisichojulikana kwenye akili za wapiga kura