Member of EVRS

Monday, 30 July 2012

Watazamaji Wabadili Matokeo ya Waamuzi Kwenye Olimpiki

Kushoto Cho akishangilia alipotangazwa mshindi na picha ya Kulia akiwa na butwaa mara matokeo yalipobatilishwa
 Katika hali isiyo ya kawaida, waamuzi na majaji wa shindano la judo kati ya Cho Jun-Ho wa Korea Kusini na Ebinuma Masashi wa Japan, ilibidi wabadili maamuzi ya kutangaza mshindi pale hapo awali walipomtangaza Cho kuwa mshindi kwa kunyanyua bendera za rangi ya bluu ambayo ndio iliyokuwa inawakilisha mwenye mavazi ya bluu.
Lakini, mashabiki walizomea uamuzi huo, ikabidi majaji na waamuzi wakae tena na kujadili kabla hawajabatilisha matokeo na kumtangaza  Masashi wa Japan kuwa mshindi
Maamuzi yalipobadilishwa

Hali hii inatia wasiwasi ya kuwa majaji hawako makini, au kwa makusudi wanawatoa baadhi ya washindani. Katika angalia yangu, kuna maamuzi waliyotoa kwenye mchezo wa masumbwi hata na mimi yalinipa mashaka.

Habari huu kutoka Euro sport

Sunday, 29 July 2012

Yanga Bingwa Kombe la Kagame 2012


Timu ya Yanga ya Dar es Salaam, Tanzania imefanikiwa kutetea kombe lake la Klabu Bingwa Afrika Mashariki ambalo kwa sasa limepewa jina la Kombe la Kagame baada ya kuifunga timu ya Azam ya Dar es Salaam pia kwa jumla ya magoli 2 - 0. 
  
Magoli ya Yanga yalifungwa na Hamis Kiiza katika dakika ya 45 na Said Bahanuzi katika dakika ya 90.
  
Kwa sasa, Yanga imefanikiwa kulichukua kombe hili kwa mara ya tano. 
  
Hapo awali, Timu ya Vita Club, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilifanikiwa kuifunga timu ya APR ya Rwanda kwa magoli 2 - 1 na kujiwezesha kushika nafasi ya tatu.  
   
Binafsi, nazipongeza timu zote za Tanzania kufanikiwa kufika katika hatua za mbele na hatimaye fainali kuzikutanisha timu za Tanzania pekee

Friday, 27 July 2012

Gharama ya Kuunganishiwa Umeme Kushuka - Waziri wa Nishati na Madini

Waziri Sospeter Muhongo ambaye ana dhamana ya kuongoza wizara ya Nishati na Madini, leo akiwa anawasilisha makadirio na matumizi ya wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya bajeti ya mwaka 2012/13 ametangaza kusudio la serikali kupunguza gharama za kuunganisha umeme kwa maeneo ya mijini na vijijini likiwa na punguzo kati ya asilimia 25 na 70 kutegemea na mahitaji ya vijijini na mijini, huku akizungumzia zaidi kwa njia moja (Single phase). 
  
Hata hivyo, punguzo la gharama hizi litaanza kutumika kuanzia mwezi Januari mwaka 2013. 
  
Katika mambo mengine aliyozungumzia, ni pamoja na kukiri kuwa kuna baadhi ya watendaji wa Tanesco si waaminifu, na wamekuwa wakishiriki katika vitendo vya kulihujumu shirika la hilo la ugavi wa umeme. 
Waziri ameahidi kuwa kuna hatua madhubuti za kuhakikisha umeme utapatikana na polepole suala la mgawo wa umemem litakwisha. 
  
Serikali pia imewekeza katika kumiliki na kutumia njia za kusafirisha gesi asilia ambayo itatumika kuzalisha umeme, na pia kuhakikisha asilimia 0.5 ya faida ya kuzalisha gesi asilia inatumika katika kutoa umeme kwenye maeneo gesi asilia ainapozalishwa na kupitia.  
  
Cha muhimu alichoahidi, ni kuendesha wizara kwa uwazi na watu wote wanakaribishwa kutoa maoni yenye mtazamo chanya au hasi. 

Monday, 23 July 2012

War in Eastern DR Congo: Kagame Blasts International CommunityPresident of Rwanda, Paul Kagame today when addressing the Ambassadors, Internationa senior Military officers, Local senior and junior Military Officers and other invited guests to the inauguration of Rwanda Defence Forces Command and Staff College. He expressed his disatisfaction on remarks which has been made by powerful international community by condemning his Government to support Eastern Congo rebels.
He denied all accusations impounded on his Government's shoulders as baseless and infact intriguing more chaos in the region. 
  
He spent some time explaining how the current war started which was engineered by the same Internation community which he did not disclose their identities.  
  
Among the things he said, where his speech was broadcasted live by Rwanda Television, is that he was approached well in advance before the current havoc, that he should give help to the Internation Criminal Court (ICC) to facilitate arrest for some of the Congolese rebellions which were needed by Internation Criminal Court for justice trial regarding crimes against humanity (which he said this organisations-ICC, has been politicised and lost its meaning and intentions). According to him, he was shocked by this act, and he refused to interfere other autonomy state, he gave them clear answer if they want to do that in Congolese territory, let them proceed without involving Rwanda.  
  
He further said, he communicated to DR Congo president on this matter to warn him what has been cooked under the ground, which he realised his neighbour president was aware and actually wanted those rebellions to be handled to his Government rather than being sent to ICC. 
  
President Kagame was puzzled after he realised that the plan was going ahead despite that The Congolese Government had a meeting with rebellions and International community where there was an agreement of certain matters to be solved to maintain the peace. 
  
H. E. Kagame is irked to see the war is getting fiercer, and the International community have shut down their deaf ears to what they know exactly what is happening, while opening their mouth by shouting Rwanda stops ........... He added that, what is happening in Congo now, is what exactly happened during the Rwanda genocide in 1994 where same if not similar people shut down their deaf ears and eyes witnessing shed of innocent blood massively. He actually express that the ICTR which was established by UN to charge the genocide mastermind network, should also charge some members of International Community.

Friday, 13 July 2012

Mbunge wa Kigamboni Atolewa Bungeni kwa Kuwatetea Wananchi Wake


Mbunge wa Kigamboni Dr Faustine Ndugulile (CCM) jana tarehe 12 Julai 2012 alitolewa nje ya ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania baada ya kulazimishwa kuomba radhi na kufuta kauli ambayo aliitoa juzi kueleza wasiwasi wake wa mazingira ya baadhi ya madiwani wake kukaribishwa bungeni na waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi bila ya yeye kuwa na taarifa, na hasa ukizingatia alikuwa anajua madiwani wake walikuwa katika ziara ya mafunzo katika mkoa mwingine.

Dr Ndugulile ambaye yupo mstari wa mbele kutetea haki na stahiki za wananchi wake, amekuwa mwiba mkali kwa mawaziri ambao wamekuwa wanatumia nguvu na kuvunja sheria dhidi ya wananchi wake.
Nguvu alizonazo, zinasukumwa kwa ukubwa na matakwa ya wananchi wake ambao walimchagua kuwawakilisha katika kutatua matatizo yao mbalimbali.  
  
Mojawapo ya jambo walilomtuma kuwasemea bungeni ni pamoja na kuukataa mpango wa mji mpya wa Kigamboni kwani umegubikwa na utata mwingi na umekiuka sheria nyingi za ardhi pamoja na katiba inayotumika sasa.  
   
Wananchi hapo awali walitaka mpango huo uratibiwe upya kwa kuwashirikisha, lakini wizara husika ilikuwa inapiga chenga na kutoa taarifa ambazo hazikuwa sahihi kwenye baadhi ya vyombo vya habari na vya sheria. 
   
Inaonekana wizara na watendaji wake hawakuwa na habari ya kuwa wananchi walimwita mbunge wao katika kikao chao cha wazi na kumtuma nini akawasemee bungeni, na ndicho hicho alichokisema bungeni ambacho kinaonekana kiliwaudhi baadhi ya watendaji wa serikali na bunge na kuamua kumpa adhabu kali kwa kumkoseha siku 3 za kuhudhuria vikao halali vya bunge.  
   
Mwezi uliopita wananchi hawa hapa chini walitoa dukuduku zao na maazimio kuhusu mji wa Kigamboni

Baadhi ya wananchi wa Kigamboni walipomuita mbunge wao wamueleze dukuduku lao kuhusu mji mpya wa Kigamboni

Mwananchi akichangia mawazo kuhusu mji mpya wa Kigamboni

Mmoja wa wachangiaji aliyekuwa anawakilisha taasis ya kidini

Mwakilishi wa kamati ya wakazi wa Kigamboni akifafanua jambo kuhusu Mji Mpya unaotaka kuletwa

Viongozi wa wananchi wakisikiliza kwa makini

Mbunge akikabidhiwa ripoti ya kamati kuhusu juhudi walizozifuata na maazimio waliyoyapitisha
Katika kuonyesha kutahayari, naibu waziri wa wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi, alionekana kwa namna fulani kuwa na kigugumizi alipokuwa akijibu baadhi ya hoja za wabunge, kwani yeye ndiye aliyekuwa mchangiaji wa kwanza baada ya Dk Ndugulile kutolewa nje ya ukumbi wa bunge.  
  
Na kudhihirisha kuwa suala hili halikumpendeza waziri, alitumia karibu theluthi moja ya muda wake wa kujibu hoja za wabunge zaidi ya 150 waliochangia kuzungumzia suala la Kigamboni na mbunge wake. Na kuonyesha ya kuwa hakupendezwa na Mbunge huyo wa Kigamboni, alikataa kumtaja Mbunge wa Kigamboni kama mmoja wa watu waliochangia katika hotuba yake aliyoitoa hapo awali. 
  
Japo waziri Tibaijuka alianza kwa kuisifia demokrasia iliyopo kwa sasa na watu kusema bila uoga, na baadaye alitamka ya kuwa amemsamehe Dr Ndugulile kwa yale aliyoyasema, lakini haikuweza kuficha kutofurahishwa na kauli ya Dr. Ndugulile na wasiwasi wake kuhusu kutekelezwa kwa mradi huo.
Sio siri, Mama Tibaijuka amekuwa mstari wa mbele kwa kutekeleza mambo kisheria, lakini kwa Kigamboni, bado hajapata ufumbuzi wa mpango huu ambao hata yeye ameukuta ukiwa tayari njiani pamoja na kasoro zake nyingi tu.  
   
Kutolewa bungeni kwa Dr Faustine kuliwashtusha wapiga kura wake, na kwa ujumla wamemuona kama shujaa wao kwa kusimama kidete kutetea maazimio yao.  
 
Kama wananchi wa nchi huru na yenye ustaarabu, hatutapenda kuona kunatokea uvunjifu wa amani kwa wana Kigamboni. Tuna imani busara na hekima itatumika kwa kufuata sheria mama za nchi.  

Wednesday, 4 July 2012

Rwanda Yaadhimisha Miaka 18 Baada ya Mauaji ya Kimbari ya Mwaka 1994


Siku ya leo tarehe 4 Julai 2012, Rwanda imeadhimisha miaka 18 tangu mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi yalipomalizika. 
Tarehe kama hii ya leo hapo mwaka 1994, jiji la Kigali lilikombolewa na majeshi ya RPF na hivyo kukomesha mara moja mauaji yaliyokuwa yanaendelea amabyo yalilengwa haswa kwa watutsi, japo na wale wahutu wenye msimamo wa wastani nao walikuwa wakishambuliwa na hata kuuawa. 
  
Siku kama ya leo, watu huwa wanatoa ushuhuda wa matukio yalivyokuwa na kuendelea kutoa msamaha kwa wale waliofanya mauaji na kutesa watu waliokuwa hawana hatia. 
  
Tarehe 4 Julai huwa ni kilele cha maombolezo ambayo huanza tarehe ambayo ni sambamba na wakati mauaji yalipoanza mnamo mwezi wa Februari. 

Kwa mwaka huu wa 2012, wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka nchi za Kenya, Tanzania, Uganda na Burundi waliungana kwa pamoja kwenda kutoa heshima kwa wahanga wa mauaji hayo waliozikwa kwenye eneo la Gisozi wakisindikizwa na wanyarwanda ambao wengi wao walikuwa wakiishi Tanzania kama wakimbizi baada ya kukimbia vita na mauaji ya kikatili yaliyokuwa yakiendelea wakati huo nchini Rwanda. 

Tuesday, 3 July 2012

Choo na Mgawanyo wa Matumizi

Alaa, kumbe mgawanyo wa matumizi ya choo upo wa aina nyingi!

Nilishazoea kuona mgawanyo wa jinsia ........

Monday, 2 July 2012

Euro 2012 Final: Spain 4 - 0 ItalyItaliaaaaaa ...... Last minutes, I thinks their stockings were packed with gravels and stones, they could not fly!
Anyway, they were playing with the best team in the World!

Scorers
Silva - 14'
Jordi Alba - 41'
Torres - 84'
Mata - 88'

Ball possession 50 - 50

Sunday, 1 July 2012

Rwanda Yasheherekea Miaka 50 ya Uhuru Wake


Rwanda leo imeadhimisha miaka 50 tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa wabelgiji hapo mwaka 1962.
 
Hadi kufikia miaka 50 ya uhuru, nchi ya Rwanda imepitia mambo mengi, kubwa zaidi ni mauaji makubwa ya kimbari yaliyolengwa kuwaanagamiza watutsi wa Rwanda yaliyofanyika mwaka 1994. 
  
Mbali ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru, pia iliadhimisha miaka 18 tangu mauaji ya kimbari yalipomalizika.  
 
Katika hotuba ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame, amesema kwa sasa wanaangalia maisha ya baadaye na kusahau yaliyopita. 
 
Kesho Jumatatu itakuwa siku ya mapumziko, kwani leo watu watakesha wakisheherekea sikukuu hii.