Member of EVRS

Friday, 27 July 2012

Gharama ya Kuunganishiwa Umeme Kushuka - Waziri wa Nishati na Madini

Waziri Sospeter Muhongo ambaye ana dhamana ya kuongoza wizara ya Nishati na Madini, leo akiwa anawasilisha makadirio na matumizi ya wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya bajeti ya mwaka 2012/13 ametangaza kusudio la serikali kupunguza gharama za kuunganisha umeme kwa maeneo ya mijini na vijijini likiwa na punguzo kati ya asilimia 25 na 70 kutegemea na mahitaji ya vijijini na mijini, huku akizungumzia zaidi kwa njia moja (Single phase). 
  
Hata hivyo, punguzo la gharama hizi litaanza kutumika kuanzia mwezi Januari mwaka 2013. 
  
Katika mambo mengine aliyozungumzia, ni pamoja na kukiri kuwa kuna baadhi ya watendaji wa Tanesco si waaminifu, na wamekuwa wakishiriki katika vitendo vya kulihujumu shirika la hilo la ugavi wa umeme. 
Waziri ameahidi kuwa kuna hatua madhubuti za kuhakikisha umeme utapatikana na polepole suala la mgawo wa umemem litakwisha. 
  
Serikali pia imewekeza katika kumiliki na kutumia njia za kusafirisha gesi asilia ambayo itatumika kuzalisha umeme, na pia kuhakikisha asilimia 0.5 ya faida ya kuzalisha gesi asilia inatumika katika kutoa umeme kwenye maeneo gesi asilia ainapozalishwa na kupitia.  
  
Cha muhimu alichoahidi, ni kuendesha wizara kwa uwazi na watu wote wanakaribishwa kutoa maoni yenye mtazamo chanya au hasi. 

No comments: