Member of EVRS

Wednesday 20 April 2011

Look here: Kigamboni, New City Plan

Being a prospective Kigamboni resident in Dar es Salaam....
 I was attracted by this master city plan....

Click here at kitururu's blog to see the .... plans

Tuesday 19 April 2011

Jonathan Wins Nigerian Presidential Race


He is a winner, no doubts

Scoop more than 57% out of 20 contestants.

People from the North are angry for the South - South Corridor, because he was the president before, and now is tha president again ......

Friday 15 April 2011

Muswada wa Marejeo ya Katiba ya Tanzania 2011 Waondolewa Bungeni

Kamati ya Bunge inayohusiana na masuala ya uundwaji wa sheria, imetoa mapendekezo ya kuongeza muda wa kupitia muswada wa sheria utakaohusu mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Sababu kubwa ni:
  • Kutoa muda zaidi wa kamati hiyo kupitia muswada huo
  • Kufanyia kazi mambo ambayo yameonyesha kuleta utata
  • Kuwapa muda zaidi wanachi wa Tanzania kutoa maoni zaidi
  • Kuandaa muswada kwa lugha ya kiswahili ili watu wauelewe zaidi kuliko kutafsiriwa na watu wachache
 
Spika Anne Makinda ameridhia, lakini ametoa tahadhari ya kuwa muswada huo haumilikiwa na chama chochote cha siasa, pia amewaasa watu wote kuupitia taratibu bila jazba wala kuleta fujo. Mwisho aliiagiza kamati kumpa ratiba ya shughuli za kurejea muswada huo, na kueleza lini watakuwa tayari kutoa muswada huo tena kwa lugha zote za kiswahili na kiingereza.
    
Hapo awali, muswada huu ulileta fadhaa na ghadhabu kwa baadhi ya watu wakiupinga kwani ulikuwa umekataza baadhi ya mambo kujadiliwa katika maoni ya marekebisho mapya yatakayopendekezwa.

Thursday 14 April 2011

Anne Makinda: Bado Kanuni za Bunge Zinamkanganya

Kwa wale wanaofuatilia mijadala ya Binge la Tanzania kwenye runinga moja kwa moja, watakubaliana nami ya kuwa Bunge la sasa la Tanzania linaelekea kuyumba na kuendeshwa ndivyo sivyo. 
   
Chanzo kilichopo ni pamoja na Spika Anne Makinda kutokufahamu vizuri baadhi ya kanuni za uendeshaji wa Bunge la Tanzania, na wakati mwingine kuendesha mambo kwa "mazoea". 
Katika kikao cha Bunge kilichopita, kuna siku alikiri ya kuwa kuna baadhi ya kanuni hakuwa anazijua, hadi wabunge walipokuwa wananukuu vifungu fulani fulani, akajikuta kuwa naye alikuwa havijui.
Hayo ni matunda ya kuendesha Bunge kwa mazoea, ndio maana hata na yeye baada ya kukaa bungeni kwa zaidi ya miaka 30, bado hajui baadhi ya kanuni, achilia mbali ya kuwa alishawahi kuwa naibu spika! 
  
Jana wakati wa kikao cha Bunge aling'aka pale mbunge mmoja alipotaka mwongozo wa uteuzi wa wenyeviti wa Bunge, baada ya Bunge kukiuka uteuzi wa wagombea.
Mwishoni Spika ilibidi akubali kutengua kanuni hiyo iliyokiukwa ili wenyeviti hao waweze kuteuliwa na kufanya kazi baada ya kuonekana upungufu/ uvunjaji wa kanuni ya Bunge.

Pia kulikuwa na vurugu nyingine
Nisikumalizie uhondo, ingia hapa kwa Subi upate video ya vurugu Bungeni. Utabofya kwenye link aliyo onyesha, nina hakika utabaki mdomo wazi!!!

Monday 11 April 2011

Mukama ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Mpya wa CCM

Hatimaye jina la mrithi wa Yusuph Makamba kama katibu mkuu wa CCM limetangazwa na mwenyekiti wa CCM, naye si mwingine bali ni Wilson Mukama (Pichani juu)
Jina lake limepitishwa na Kikao cha halmashauri kuu ya CCM huko Dodoma, na muda mfupi uliopita ndio jina hili likatangazwa rasmi.   
   
Naibu wake kwa upande wa Bara ni John Chiligati na kwa upande wa Visiwani ni Ali Vuai Ali.

Sunday 10 April 2011

Yusuph Makamba Ajiuzulu Ukatibu Mkuu wa CCM

Habari zilizojiri hivi karibuni zinasema Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Bw. Yusuph Makamba amejiuzulu wadhifa wake. Sio yeye peke yake, bali hata sekretarieti yake yote nayo pia imejiuzulu. 
Mpaka sasa hivi bado haijajulikana nani atateuliwa kushika nafasi yake.
Mwenyekiti wa CCM Mh. Jakaya Kikwete inasemekana amewataka wanachama wa CCM wawe watulivu wakati wakisubiri uteuzi mpya. Ameyasema hayo katika kikao cha CCM kinachoendelea huko Dodoma.  
   
Kujiuzulu kwa Makamba kulikuwa kunatarajiwa kwani alikuwa katika shutuma na lawama nzito juu yake kuhusiana hasa na kuporomoka kwa CCM katika uchaguzi mkuu uliopita kwani alihusishwa na kuleta mkanganyiko na makundi. Kuna baadhi ya wagombea walimhusisha na tuhuma za rushwa na upendeleo hasa wa kidini ambapo tuhuma hizo bado hajizathibitishwa.  
  
Habari zaidi zitapatikana muda si mrefu.

Friday 8 April 2011

Hellow Museveni! This is insanity

President Yoweri Museveni of Uganda has tendered a bill before the selective members of Parliament for endorsement of US $ 750 Million supplementary budget to buy 6 jet fighters from Russia. He said, money will be obtained from the Central Bank of Uganda. However, nobody within the bank is aware of the huge transaction plan.
Rosoboronexport, is the company which have signed a contract with Uganda to supply Su-30MK2s jet fighters. 
  
According to the Monitor, the members of parliament called to endorse the supplementary budget, were not aware of the agenda prior to meet the president, and he kept on referring the transactions without their knowledge, ........

It is further said, that the aim of buying the jet fighters is to protect Ugandan territory which is in danger of an attack.....
Political analysts are convinced that Museveni has observed what is happening in Libya, and realised that the same might occurs to him since he has been in power for more than 25 years and at the end of his current term, he will be cerebrating his 30+ years as president, and he seems that he would love to beat Gaddafi's record of 40+ years in power.
They concluded this, after the leaking news that he had signed another contract to buy anti-riot equipments, which of course will never be used to protect Uganda from al-shabaab offences!! 
 
Uganda need more money to invest on human welbeings (who are anyway tax payers, and the money is theirs) and environment than jet fighters, which might be used to protect the "chosen few". 

Thursday 7 April 2011

Rwanda Leo Yaadhimisha Miaka 17 ya Mauaji ya Kimbari Dhidi ya Watutsi

Leo imetimia miaka 17 tangu mauaji ya Kimbari ya Rwanda kutokea.
Kwa miaka yote tangu mauaji hayo ya kikatili dhidi ya Watutsi yafanyike, tarehe kama ya leo watu hukumbuka matukio ya mwaka 1994 kwa hotuba na baadhi ya watu kutoa ushuhuda wa matukio ya wakati huo. Kwa ujumla huamsha hisia na uchungu kwa manusura, baadhi yao hupata mfadhaiko wa akili kiasi cha baadhi yao kulazimika kupelekwa hospitali kwa matibabu. 
  
Katika hotuba ya kitaifa siku ya leo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, katika machache aliyozungumza, hakuficha hisia zake na hasira kwa wale wanaoendelea kupinga mauaji hayo ya kimbari dhidi ya watutsi (Genocide against Tutsis), na pia aliyashutumu mataifa yanayoendelea kuwaficha watuhumiwa wakuu wa mauaji hayo ambao wamejificha katika baadhi ya nchi hususan za Ulaya, na kukataa kata kata kuwatoa kwa ajili ya kushitakiwa kisheria. Alitoa hisia yake ya kuwa nchi hizo zinaogopa kuwatoa kwa sababu zinaogopa ushahidi utakaotolewa na hao watuhumiwa, utadhihirisha ni jinsi gani nchi hizo zilishiriki katika kufanikisha mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi wa Rwanda.  
  
Siku kama ya leo huwa ni mapumziko ya kitaifa, na shughuli zote za kikazi husimamishwa ikiwa ni pamoja na maduka kufungwa na shughuli zote za kibiashara kusimamishwa.  
 
Jinsi nilivyoiona siku ya leo, sikuona tofauti na siku nyingine za maadhimisho ya mauaji hayo hasa nikilinganisha na maadhimisho ya miaka iliyopita, kwani jiji la Kigali limepooza sana, na watu wachache wanaotembea barabarani, sura zao zinaonyesha huzuni kubwa.

Nakubaliana na msemo wao NEVER, NEVER... IT WILL NEVER HAPPEN..... NEVER AGAIN

Wednesday 6 April 2011

Kampuni ya Simu Ya Ghaddafi Kufungwa Rasmi Rwanda

Kampuni ya mawasiliano ya simu za kiganjani ya Rwandatel inatarajiwa kusimamisha kutoa huduma za mawasiliano ifikapo usiku siku ya ijumaa tarehe 8 Aprili 2011.


Hii ni kutokana na kufutiwa leseni yake ya biashara ya mawasiliano ya simu za kiganjani hapa Rwanda baada ya kushindwa kukidhi vigezo vya biashara hiyo kwa taratibu za nchini Rwanda.
Mkuu wa tume inayodhibiti mawasiliano Rwanda (RURA) Regis Gatarayiha, amesema leseni hiyo imefungwa moja kwa moja.

Kampuni hii ya simu inamilikiwa na kiongozi mwanamapinduzi wa Libya Muhamar Ghaddafi ambaye utawala wake huko katika hatihati yakung’olewa na wapenda mabadiliko wa Libya wakisaidiwa kwa kiasi kikubwa na majeshi ya Ulaya na Marekani.

Wiki iliyopita, wakati Rais wa Rwanda Paul Kagame akiongea na waandishi wa vyombo vya habari vinavyofanya kazi Rwanda, aliulizwa msimamo wa Rwanda kuhusiana na agizo lililopitishwa na umoja wa Mataifa wa kumuwekea vikwazo vya kiuchumi Ghaddafi huku muuliza swali akilenga uwekezaji wa Ghaddafi hapa Rwanda kupitia njia ya mawasiliano. 
  
Rais Kagame alijibu kwa kueleza kuwa kampuni ya Ghaddafi tayari ilishakuwa na matatizo ya kiutendaji hata kabla ya vita ya Libya, na hivyo walikuwa wapo mbioni kuisimamisha kutoa huduma zake nchini, pia alisema anaunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa kwani nchi zote wanachama zinawajibika kufuata maagizo pale haki za binadamu zinapokiukwa.  
  
Tume inayodhibiti mawasiliano hapa Rwanda, imewashauri wateja na watumiaji wa huduma za simu wa Rwandatel kujiunga na kampuni nyingine za simu.
Wafanyakazi zaidi ya 300 watapoteza ajira zao ikijumuisha na raia wa Libya na makampuni yanayowakilisha Rwandatel nchini (Dealers).

Pia, kuna baadhi ya shule zilizokuwa zinafadhiliwa na serikali ya Libya, kwa sasa imebidi zipandishe ada kwa asilimia mia moja kukidhi upungufu wa fedha kutokana na kusimamishwa kwa malipo ya kila mwaka kutoka katika mfuko maalumu wa Libya kusaidia maendeleo ya elimu nchini Rwanda.

Friday 1 April 2011

Nawatakia Weekend Njema



Sina la zaidi kwa kuandika hapa.

Najua wengi mmelizwa na siku hii ya Wajinga!
Nawatakia burudani tosha mwisho wa wiki hii mpoze machungu ya kugeuzwa mafaaaala. Lakini ndio mambo hayo.

Dawa za "Vikombe" Si Lolote si Chochote

Wimbi la dawa za "vikombe" inasemekana si lolote si chochote, bali ni njia mojawapo za kujikwamua kimaisha na kukabiliana na ukata uliopo kwa sasa Bongo.

Watu werevu wametumia mbinu ya matatizo ya wananchi na ukomo wa fikra zao, na kutumia njia hiyo kuwahadaa ya kuwa wanatibu magonjwa sugu ambayo madaktari wamesema hayatibiki hadi kupona kabisa. 
  
Maneno haya yamebainishwa na mchungaji mstaafu wa Loliondo, na ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kwa kuacha kunywa dawa zao za hospitali baada ya "vikombe", amekuwa akisisitiza waendelee kunywa dawa zao hata baada ya "vikombe" 
  
Itakumbukwa ya kuwa siku zote huwa anawaambia wateja wake ya kuwa, kupona kwao ni kwa imani, na kama huna imani, basi hautapona.
Hii ni kama vile watu wanavyo amini ya kuwa Mungu yupo, japo hawajawahi kumuona wala kusikia sauti yake achana na harufu yake tu. Lakini watu kwa imani yao, inapotokea mtu akamkashifu huyo Mungu ambaye hawajamuona na wanayemuamini, kunaweza kukatokea vita na maangamizi! 
  
Tahadhari: Leo ni siku ya wajinga!