Sababu kubwa ni:
- Kutoa muda zaidi wa kamati hiyo kupitia muswada huo
- Kufanyia kazi mambo ambayo yameonyesha kuleta utata
- Kuwapa muda zaidi wanachi wa Tanzania kutoa maoni zaidi
- Kuandaa muswada kwa lugha ya kiswahili ili watu wauelewe zaidi kuliko kutafsiriwa na watu wachache
Spika Anne Makinda ameridhia, lakini ametoa tahadhari ya kuwa muswada huo haumilikiwa na chama chochote cha siasa, pia amewaasa watu wote kuupitia taratibu bila jazba wala kuleta fujo. Mwisho aliiagiza kamati kumpa ratiba ya shughuli za kurejea muswada huo, na kueleza lini watakuwa tayari kutoa muswada huo tena kwa lugha zote za kiswahili na kiingereza.
Hapo awali, muswada huu ulileta fadhaa na ghadhabu kwa baadhi ya watu wakiupinga kwani ulikuwa umekataza baadhi ya mambo kujadiliwa katika maoni ya marekebisho mapya yatakayopendekezwa.