Member of EVRS

Monday 29 November 2010

Matumaini Mapya Wizara ya Ujenzi

Nilikuwa nikiangalia runinga leo asubuhi, nikapokea habari nzuri zinazohusu ujenzi wa barabara Tanzania. 
  
Waziri wa ujenzi, Mhesh Pombe Magufuri akiwa na naibu waziri wake Prof Harrison Mwakyembe, jana walipokuwa wakiongea na watendaji wa wizara ya Ujenzi, alitoa muda wa mwezi mmoja kwa watendaji hao kujipanga na kumletea taarifa ya matarajio (projections) ya utendaji wao wa kazi kwa kipindi kijacho. 
   
Magufuri aliyeonyesha ukali katika kauli zake, alikemea tabia ya usimamizi mbovu wa miradi ya serikali, na pia kutowajibika. 
Mbali ya yote hayo, alielekea kushangaa ni kitu gani kinachoshindikana kujenga daraja la Kigamboni, akatolea mfano wa huko Uchina ambako aliona daraja lenye urefu wa km 26 likijengwa kwa miezi 14 tu. Alitoa rai kwa NSSF kujenga daraja hilo haraka iwezekanavyo, vinginevyo ataiomba benki kuu ya Tanzania kuidhinisha na kutoa pesa za ujenzi wa daraja hilo ili serikali isimamie. Kwa hapa naona ni neema kwa wakazi na wageni wanaotembelea Kigamboni ambao wamekuwa wana kilio hiki kwa muda mrefu sasa.  
   
Cha kufurahisha zaidi, na iwapo kitakuwa cha vitendo, ni pale Magufuri aliposema uanze mpango na ujenzi wa madaraja ya juu ya kupitia magari (flyovers), kwani hakuna kinachoshindikana. Pia kuwaeleza wazi kutakuwa na ziara za kushtukiza kukagua kazi na miradi mbalimbali ya ujenzi, pale itakapokutwa kazi ya ujenzi inalegalega, basi mhandisi anayesimamia ajijue ya kuwa kibarua kimekwisha ota nyasi (Keshafutwa ajira).  
  
Na mwisho aliwagawia watendaji wote ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 - 2015 ili waweze kufahamu ni nini serikali ya CCM inakusudia kutekeleza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kutoka sasa. Na ilani hizo walizigawa yeye mwenyewe na Mwakyembe kwa mikono yao wakimpa kila mtendaji pale alipokuwa amekaa, na sio watendaji kuzifuata kwenye meza kuu.  
  
Mimi nasema, mwanzo huu unatia moyo, kwani tunawafahamu Magufuri na Mwakyembe ni watendaji wazuri na wasimamizi katika maslahi ya Taifa. Nawatakia kila la heri.

Friday 26 November 2010

Have a nice weekend

I am running short of words...... 
 
This week was hectic ... busy.... whatever you call it..
  
Tomorrow, there is a community work here, no shop, market, bank, hotel, transport etc will be available from morning till mid day. 
  
If you are going to airport, you..either go before 7.00 am or after mid day! I am very serious.

Wishing you a lovely weekend!! :-x

Thursday 25 November 2010

Womb Fight!!!!



What kind of persons they are gonna be!

Enjoy your thursday!

Wednesday 24 November 2010

Baraza la Mawaziri na Naibu Mawaziri Novemba 2010

Ofisi ya Rais:
  • Utawala Bora - Mathias Chikawe
  • Mahusiano na Uratibu - Stephen Wassira
  • Menejimenti ya Utumishi wa Umma - Hawa Ghasia

Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Muungano - Samia Suluhu
  • Mazingira - Dr. Terezya Luoga Hovisa
Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi
  • Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  George Mkuchika
            Naibu (TAMISEMI) - Aggrey Mwanri na Kassim Majaliwa

Wizara ya Fedha - Mustapha Mkulo
Naibu Gregory Teu na Pereira Ame Silima

Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Shamsi Vuai Nahodha
Naibu - Balozi Khamis Suedi Kagasheki 
 
Wizara ya Katiba na Sheria - Celina Kombani
 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa - Bernard Membe
Naibu Mahadhi Juma Mahadhi
 
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Dk Hussein Ali Mwinyi
 
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi - Dr. Mathayo David Mathayo
Naibu - Benedict Ole Nangoro
  
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia - Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

 Naibu - Charles Kitwanga
 

  
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Prof. Anna Tibaijuka

 Naibu - Goodluck Ole Madeye
  
Wizara ya Maliasili na Utalii - Ezekiel Maige
  
Wizara ya Nishati na Madini - William Mganga Ngeleja
Naibu - Adam Kigoma Malima
  
Wizara ya Ujenzi - Dr. John Pombe Magufuli
 Naibu - Dr. Harrison Mwakyembe
   
Wizara ya Uchukuzi - Omari Nundu
 Naibu - Athumani Mfutakamba

  
Wizara ya Viwanda na Biashara - Dr. Cyril Chami
 Naibu - Lazaro Nyalandu
  
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi - Dr. Shukuru Kawambwa
 Naibu - Philipo Mulugo
 

 
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii - Dr. Haji Hussein Mpanda
 Naibu - Dr. Lucy Nkya
  
Wizara ya Kazi na Ajira - Gaudensia Kabaka
 Naibu - Makongoro Mahanga
  
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Sophia Simba
 Naibu - Umi Ali Mwalimu
  
Wizara ya Habari, Vijana na Michezo - Emmanuel John Nchimbi
 Naibu - Dr. Fenella Mukangara
  
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Samuel John Sitta
 Naibu - Dr. Abdallah Juma Abdallah
  
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika - Prof. Jumanne Maghembe
 Naibu - Christopher Chiza
  
Wizara ya Maji  - Prof. Mark James Mwandosya

 Naibu - Eng. Gerson Lwinge

  
 
Habari kutoka Ikulu Mawasiliano

Naomba Ushauri

Sehemu ninayoishi hapa Kigali, ina usalama wa hali ya juu, na patrol za polisi usiku zipo karibu muda wote! 
   
Tarehe kama ya leo, yaani 24 Mei 2010, mfanyakazi wangu wa nyumbani (house boy) alirudi kutoka "kijijini" alipoenda kusalimia famlia yake, na aliporudi usiku nilishtukia tu yumo ndani ya ua, bila kufunguliwa geti.
Nilipomuuliza kaingia vipi, akasema alifungua mlango kwa ndani kupitia kidirisha cha ulinzi (Security window), kwa ujumla sikuamini amini. Siku iliyofuata niliporudi kutoka kazini nilikuta katoweka, baadaye niligundua upotevu wa fedha kutoka chumbani kwangu.  
Habari ilifikishwa polisi, na hakuna kilichofanyika.  
   
Kijana huyo alikuwa naaminiwa sana na kila mtu, lakini mimi tangu siku ya kwanza roho yangu ilimkataa. Japo familia yangu walielekea kumwamini na kumpenda. Sasa naona wamebadilika kuliko hata mimi!

Leo tarehe 24 Novemba( Sielewi kwa nini ni hii tarehe), miezi sita imetimia, wakati naingia gereji kujiandaa kuondoka kwenda kazini, niliona nyendo zisizo za kawaida kwenye kona ya gereji, nilipokaza macho zaidi nikaona macho ya blink hapo kwenye kona huku yakiwa yamefunikwa na mlango mbovu na viti chakavu. Nilipokamua macho zaidi, mara akaibuka kijana yule yule aliyekuwa mfanyakazi wangu. Akadai aliruka ukuta usiku kupata mahali pa kulala na kisha alikuwa anasubiri nikienda kazini, naye ajiondokee zake!  
   
Kwa sababu kwa sasa naishi mwenyewe, nilitoka nje kuomba msaada wa mlinzi ili nimdhibiti, lakini alifanikiwa kwa muda kuchomoka na kukimbia, lakini weeee, watu wanajua kupiga mitama ama ngwara, hakufika mbali ndo hivyo tena akaibusu ardhi.  
  
Baada ya kumfkisha polisi, akakiri alikwiba siku za nyuma. Na ni kweli aliruka ukuta kuingia ndani ya nyumba bila idhini yangu.  
HUWEZI AMINI ALIHUKUMIWA KIFUNGO HAPO HAPO, na kwa sasa amekwisha anza kutumikia kifungo jela.  
Hakuna kesi mahakamani wala kuhangaishana na kuleta ushahidi. kwani kila kitu kilikuwa hadharani.  
   
Upekuzi wangu pale alipokuwa amejificha, nilikuta sanamu ya plastiki ya mnyama mwenye pembe 2 ambazo zipo sharp. Hiyo sanamu nilishawahi kuiona ndani ya nyumba miezi mingi wakati naingia, nikaitupilia jalalani. Pia sanamu hiyo nilipoikuta, siku za nyuma nilishawahi kukuta sanamu ya mtu aliyevishwa hirizi ya mbao!  
   
Mimi ni mtu wa imani kidini na huwa sitetereki, kawaida yangu ni kuzichoma moto takataka kama hizo.  
  
Bado najiuliza, kama nikimwona tena baada ya kifungo ndani ya himaya yangu nimfanye nini.  

Sunday 21 November 2010

Jumapili Njema

Jana modem yangu ya internet ilinigomea kabisa, nikashindwa kupata habari mpya.
Leo nimeshtukizwa na kuingia kazini tangu asubuhi mpakaaaa......

Hivyo nawatakia jumapili njema, na pia tuwaombee hao wanaume ambao wamezuka sasa na mtindo wa kuua familia zao kwa visu.  
  
Kwani hivi karibuni huko Kilimanjaro mtu kaua mama yake mzazi na watoto wake wawili, juzi tu, huko Kenya kuna mtu kaua mke wake mjamzito na watoto wawili kwa visu tena, mmoja tu wa miaka 3 ndio alikimbia. Halafu tena wiki kadhaa zilizopita jamaa mmoja tena huko Marekani mwenye asili ya Afrika, aliua mke na watoto wake wawili kwa mtindo huo huo. 
  
Bahati mbaya au nzuri kama utakavyochukulia wewe, wanaume hao wote nao walikufa aidha kwa kujiua au watu wenye hasira kali kuwamaliza!
 
Aaaah, nilishasahau, nilikuwa nataka kuwatakia jumapili njema tu!

Friday 19 November 2010

USA 2012 Elections Fever start Rising Now

Sarah Palin, who was runner mate for 2008 Republican presidential candidate, has shown some interest for Republican presidential nomination for 2012 to challenge Democrats likely presidential candidate, Barack Obama.  
  
The matter for running for presidential race is still under Palin family's discussion, but Palin's fans have started canvancing for her. 
 
So far, Barack Obama has upper hand where still 55% have a positive minds towards him despite the hard economic challenges affecting the globe and his Government, while for Sarah Palin only 47% gave her chances that might win the 2010 elections, while 53% unfavour her.

Thursday 18 November 2010

CHADEMA Wamsusa Rais Kikwete na Kuondoka Bungeni

Katika hali isiyokuwa ya kutarajiwa, Wabunge wa CHADEMA leo wameondoka ndani ya ukumbi wa Bunge mara tu Rais Jakaya Kikwete alipokuwa anataka kuanza kuhutubia bunge la 10. 

Kwa muda wote wakati rais anaingia na muda wa kusoma dua, wabunge wote walikuwa wametulia. Lakini mara tu rais Kikwete alipoanza kuongea, wabunge wa CHADEMA wakaamka ghafla na kutoka nje huku kukiwa na kelele za mzomeo na wabunge wa CCM wakiwaonyesha mikono kwa kupunga wakimaanisha waondoke tu! 
 
Bado sababu halisi ya kumsusa Rais Kikwete haijawekwa hadharani, japo ilikuwa inajulikana ya kuwa uongozi wa CHADEMA ulikuwa unadai rais Kikwete hakushinda kihalali kutokana na ubovu wa uendeshaji wa tume ya uchaguzi ya taifa, huku wakiwa wanaituhumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya uchakachuaji wa kura kutoka kwa baadhi ya maofisa wake na kuipendelea CCM huku wakiihujumu CHADEMA. 
  
Majuzi, spika wa bunge la Tanzania, Anne Makinda, aliwaita viongozi wawili wa kambi ya upinzani kutoka CHADEMA na kuwasihi wakubali kumtambua Rais Kikwete kama kiongozi halali wa Tanzania vinginevyo wanaweza kupoteza haki zao za msingi za kuwawakilisha vyema wananchi waliowachagua. Hatima ya kikao hiki cha faragha hazikujulikana wazi.

Tuesday 16 November 2010

Pinda athibitishwa kuwa Waziri Mkuu Tanzania


Mhesh Kayanza Mizengo Peter Pinda leo jioni amethibitishwa na Bunge kuwa waziri mkuu wa Tanzania baada ya kupata kura za ndiyo 277 sawa na asilimia 84.5 ya kura halali zilizopigwa, na pia kura 49 za hapana sawa na asilimia 14.9
  
Mhesh Pinda anatarajiwa kuapishwa kesho ikulu ndogo ya Chamwino iliyopo Dodoma. Na hapo baadaye yeye kwa kushirikiana na Rais Kikwete na pia makamu wa Rais, Dk Bilal wataandaa baraza jipya la mawaziri.  
  
Watu wengi walikuwa wanatarajia uteuzi wa Pinda kuwa waziri mkuu wa Tanzania.  
   
Hatuna budi kumpongeza, tukitumaini ya kuwa atatenda majukumu yake kama kiongozi wa serikali bungeni vyema na kupigania haki ya watanzania wote na sio maslahi ya chama chake.  
 
Mungu ibariki Tanzania.

Monday 15 November 2010

Wapinzani Wanaelekea Kuungana Bungeni

Kuna dalili ya kuwa wapinzani ndani ya Bunge la Tanzania wataungana mara pale Aliyekuwa kiongozi wa upinzani katika bunge lililopita Mhesh. Hamad Rashid Mohamed kutamka ya kuwa wapo tayari kushirikiana na vyama vyote vya upinzani kuunda umoja ndani ya bunge na hasa kwa kutoa mawaziri vivuli.  
  
Na pia alisema ya kuwa hawana nia ya kuwania uongozi katika kambi ya upinzani, bali kushirikiana kwa pamoja katika harakati za kukuza demokrasia ndani ya bunge na pia kuendelea kuikosoa Serikali kama walivyokuwa wanafanya katika bunge la 9. 
  
Mwanzoni, kulielekea kama kuna mfarakano ambao chanzo chake hakikujulikana, na watu walihisi zilikuwa ni zile kauli za Lipumba kujiona kuwa ni bora zaidi kufuikia hatua ya kujifananisha na mlima kilimanjaro, na kumfananisha mgombe aurai wa Chadema Mhesh Willbirod Slaa kama kichuguu.  
  
Tuna imani ya kuwa CCM nao wanalitambua hilo, na hivyo watakuwa makini sana katika shughuli za kuendesha mijadala na uwajibikaji ndani ya bunge, vinginevyo 2015 wataendelea kupoteza nguvu yao bungeni na mwisho kitakachofuata wanakijua.

Friday 12 November 2010

Anne Makinda: Mwanamke wa Kwanza Kuwa Spika wa Bunge la Tanzania


Mh. Anne Makinda (Pichani) amechaguliwa kuwa spika wa bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuchaguliwa na wabunge wa Tanzania kwa kura 265 na kumshinda mpinzani wake, Mh. Mabere Nyaucho Marando aliyepata kura 53.  
  
Ushindi huu ulitarajiwa ukizingatia idadi ya wabunge wa chama cha mapinduzi (CCM) anakotoka Anne Makinda kuwa wengi kwa zaidi ya 75% ya wabunge wote.  
 
Mh. Anne Makinda alikuwa naibu spika kwa miaka mitano iliyopita chini ya Mh. Samuel Sitta ambaye mwaka huu hakupitishwa kugombea kiti hicho na chama chake.   
  
Anne Makinda anaweka historia mpya ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo katika bunge la Tanzania.  

Katika hatua za mwanzo za mchakato wa uchaguzi, wakati Mh Marando anajieleza, ulipowadia wakati wa maswali, kulitokea tafrani ndogo ya mbunge mmoja mzoefu wa CCM kutaka kukiuka maagizo ya mwenyekiti aliyesimamia uchaguzi huo Mh. Anna Abdallah wa kutaka kuuliza swali kwa kutumia kipaza sauti ambacho mgombea ndio alikuwa anakitumia, na hivyo kupandisha munkari kidogo wa baadhi ya wabunge.  
  
Aliporuhusiwa kuuliza swali kupitia kipaza sauti kingine, ilibidi akatishwe kwani lilionekana halikuwa swali bali maelezo kinyume na yaliyotarajiwa, hata alipoambiwa kunyamaza, yeye aliendelea tu kuongea na kuonyesha ya kuwa hakuwa makini katika kutekeleza maelezo ya mwenyekiti wa kikao hicho.   
   
Tunasubiri changamoto nyingi katika bunge hili lililosheheni vijana wengi kuliko bunge lililopita wakiwamo vijana wa miaka 24 walioingia hivi karibuni.  
  
Hata hivyo, Stephen Wasira wa CCM, bado anashikiria rekodi ya kuingia bungeni akiwa kijana zaidi wakati huo akiwa na miaka 23 tu. na kwa sasa yupo bungeni kwa zaidi ya miaka 40.

Wednesday 10 November 2010

Barack Obama wins Indonesian Hearts

Barack Obama's visits to Indonesia was cheered by this largest moslem country in particular at his short speech which he expressed his Indonesian life memories when he was a young boy at Indonesia (aged 6 - 10 years popularly known as Barry by then).   
  
He won the hearts of Indonesian people when he spoke some phrases of local language. He added that he was had great affection with Indonesia people in particular by having an Indonesian half sister (Indonesian-American).  
  
Obama, also applause Indonesia for extraordinary democratic transformation and refer it as an example in the world.  
   
He also focus on Indonesia economic growth and high degree of tolerance between reliogions while the country is dominated by moslems. He, further, was keen to strengthen the economic ties USA has reached with Indonesia.  
  
The overwhelmed Indonesian was evidenced through twiter messages to congratulates Obama, considering that Indonesia is the second largest Twiter user in the world.  
  
Photo from B B C

Sunday 7 November 2010

Kenya: Polisi aua watu 10 Kwa Kinachodhaniwa ni Wivu wa Mapenzi

Jumamosi usiku, Mji wa Siakago ambao upo kama km 150 kutoka Nairobi uligeuka kwa muda kuwa uwanja wa kumwaga risasi mara baada ya afisa wa polisi mmoja kwenda kwenye baa moja ikisemekana alikuwa na nia ya kumfuata rafiki yake wa kike ambaye alidhani atakuwa kwenye baa hiyo.  
   
Baada ya kumkosa alifyatua risasi humo na kuua mtu mmoja, baadaye akaenda baa ya pili na kufyatua tena risasi ambapo aliua tena mtu mmoja. Na mwisho alienda baa ya tatu, alipomkosa akafyatua tena risasi na kuua watu wanane hapo.   
    
Habari ambazo hazijathibitishwa rasmi, zinasema kati ya waliouawa, wawili ni polisi.
Chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana, ila inasemekana muuaji huyo alijisalimisha mwenyewe kituo cha polisi, na alidai alifanya hivyo baada ya kuishiwa risasi.  
  
Polisi walikuwa wamemuweka chini ya ulinzi mkali katika kituo kikuu cha polisi, Embu. 
   
Ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao walikuwa katika taharuki na gadhabu kubwa kwa tukio hilo, kiasi kwamba usalama wa mtuhumiwa na kituo alichohifadhiwa kilikuwa hatarini kushambuliwa.  
   
Polisi bado wanaendelea na uchunguzi, huku habari za rafiki wa kike wa muuaji hazijulikani, kwani katorokea mahali pasipojulikana.  
  
Watu wengi hawakuwa na habari kuhusiana na kilichokuwa kinaendelea, huku wakidhani ni sherehe za wahindu kusheherekea sikukuu ya Diwali zikiendelea, ambazo huambatana na urushaji wa fataki na milipuko.

Friday 5 November 2010

JK Mshindi wa Urais Tanzania kwa 61%

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemtangaza Jakaya Kikwete kuwa mshindi kwa kupata jumla ya alama 61.1% ya kura zote akifuatiwa na Slaa wa CHADEMA aliyepata 26.3% na wa tatu ni Lipumba ambaye safari hii kaporomoka na kupata 8%.  
  
Ushindi uliopungua wa JK haukutarajiwa na wana CCM wengi, kwani walikuwa wana imani atapata ushindi wa kimbunga wa zaidi ya 90%, lakini mambo yamebadilika kabisa.   Ikumbukwe kuwa uchaguzi wa 2005, JK alipata zaidi ya 87% ya kura zote  
   
Slaa hakuhudhuria kwenye ukumbi wa matokeo, lakini wagombea wengine wote walikuwapo.  
  
Wapiga kura Uchaguzi wa mwaka huu walikuwa 42.6% tu ya wale wote waliokuwa wamejiandikisha.

Thursday 4 November 2010

Rwandair !!!

Hivi utasijiakiaje pale shirika la ndege linapokupatia tiketi ambayo unalazimika kutumia ndege nyingine kabla ya kuunganisha na ndege yao. Halafu tarehe ya ndege yao, wanakupa siku na saa ambayo hawana safari ya kwenda huko uendako.

Shirika jingine wanapokueleza ya kuwa connection yako haiwezekani, kwani shirika waliokupa tiketi hiyo,   hawana safari muda huo!!    
Unapowarudia ofisini kwao na kuwaambia wakupe ratiba ya safari zao, wanakuambia hapo customer care, kuwa hawana ratiba ofisini, na wakati huo huo wana mtandao wanaotumia kufanya booking!! Yaani hawatanii, ndio wanakwambia ukweli.... 
  
Ukiwa bado umeduwaa, wanakuja abiria wengine wawili, tayari wametahayari na kulalalama, ya kuwa walipofika uwanja wa ndege siku 3 zilizopita, waliambiwa safari ya ndege yao imefutwa, na hivyo wakaambiwa waje leo saa 4 asubuhi, kwani ndege itaondoka saa 8 mchana. Na wakawaandikia kwenye tiketi KABISA kwa elektroniki. Alipofika saa 4 asubuhi wakafika kwa bashasha, ndio wakakuta ndege inakaribia kugusa mawingu, yaani ilipaa kama dakika 1 hivi tangu wafike. Huwezi kuamini safari zote hizo ni za kimataifa.  
  
Mimi ambaye nilikuwa nasubiri kukata tiketi, nayo ya safari ya kimataifa nikabaki mdomo wazi. Mwisho wa yote, nilipomaliza kulipa, nikapewa karatasi yangu niliyokuwa nimewapa ya maelezo yote ya abiria, na wao walikuwa wameandika kwa mkono nyuma ya maelezo yangu wakiwa wameweka na namba ya elektroniki ya tiketi yangu, wakadai printer haifanyi kazi, kwa hiyo nije uwanjani na kikaratasi hicho!!!!!!!!!!  
  
Nikaomba nitumiwe kwa barua pepe, maana niliona hicho ni kiini macho.....sasa saa 8 zimekwisha pita, bado sijapokea barua pepe yoyote, na namba za simu zetu wanazo!!!

Upo hapo, kumbe sio Bongo tu kwenye mitkas viza ..............

Wednesday 3 November 2010

Tume ya Uchaguzi Tanzania Imechoka?

Kwa mtazamo wangu, naona Tume ya uchaguzi Tanzania ndiyo inaelekea kuwa chanzo cha vurugu zote zilizotokea baada ya kupiga kura.  
  
Yote hii inatokana na kutokuwa makini kwa tume yenyewe, na kufanya kazi kwa kujiamini ya kuwa hakuna mtu yeyote atakayeweza kuwatenda kwa chochote pale watakapovuruga. Hii ni imani ya kizee, kwani ni kawaida kwetu Mzee anaposhindwa kutekeleza jambo fulani, tunamsamehe kwa misingi ya kuwa ni mzee.
  
Mapungufu yote yaliyojitokeza kwangu hayana utetezi wa msingi, suala la kusema kila siku wanajifunza halina nafasi tena, imeshatimiza zaidi ya miaka 15 tangu tume hii iundwe, na bado ati wanajifunza.   Nahisi umri wa kujifunza umeshapita kwa sasa. 
  
Walikuwa na miaka 5 ya kuandaa uchaguzi wa mwaka huu, lakini tumeshuhudia vituko na mapungufu mengi tu. 
   
  • Watu kukosekana kwenye orodha ya wapiga kura, na hivyo kunyimwa  haki yao ya kuchagua viongozi wanaowafaa
  • Kuchanganya majina na picha za wagombea
  • Kuchanganya namba za kadi za wapiga kura
  • Kuwahamisha wapiga kura kwenye vituo walivyojiandikisha bila ridhaa yao na wala bila sababu yoyote ya maana
  • Kupeleka karatasi za kupigia kura mahali pasipotakiwa
  • Kuwacheleweshea posho wasimamizi wa uchaguzi na walinzi wa vituo vya kupigia kura
  • Kuchelewesha kutoa matokeo, kwa kisingizio cha mfumo wa kurekodi matokeo, na ati miundombinu.

Ni wazi ya kuwa tume hii ina watendaji wabovu au waliochoka.
Wanapaswa kuwajibika kwa matokeo ya vurugu.
Kwa heshima yao binafsi, wanapaswa au inawabidi wapumzike sasa, kwani baadhi yao ni wazee sana kwa kazi kama hii ambayo inahitaji uangalifu mkubwa na uwezo wa kufanya kazi nyingi na kwa muda mrefu.  
  
Nina imani Filbert Bayi na Suleiman Nyambui walikuwa ni wanariadha wazuri sana wa Tanzania, lakini kwa sifa hiyo ya zamani huwezi kuwapeleka kwenye mashindano ya mbio kwa sasa, ni wazi hawatafurukuta kama utawashindanisha na wakina Kenenisa Bekele.  Labda kama unataka kupata aibu.  
  
Nina matumaini, huu ndio utakuwa mwisho wa tume hii ya Wazee wastaafu.

Monday 1 November 2010

Habari Mpya: Dk Ali Mohamed Shein Rais Mpya wa Zanzibar, Aahidi Seif Kuwa Makamu Wake

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imemtangaza Dr Ali Mohamed Shein wa CCM kuwa mshindi wa Urais wa Zanzibar kwa kupata jumla ya 50.1% akifuatiwa kwa karibu na Sheif Sharif Hamad wa CUF aliyepata jumla ya 49.1%, na vyama vingine viligawana 0.8%.

Seif Shariff Hamad alimpongeza Shein kwa kuchaguliwa kuwa rais mteule wa Zanzibar, na kumuomba atakapoanza kazi azingatie marekebisho katika timu ya tume ya uchaguzi, akitolea mfano kwa baadhi ya watendaji wa tume ambao walikuwa wakiharibu kwa makusudi shahada za kupiga kura hasa za watu waliokuwa wanahoji ukiukwaji wa maadili na sheria za uchaguzi zilizokuwa zinafanywa na watendaji hao. Na pia alimuomba rais mteule atambue kuwa hakuna msindi wala mshindwa, kwani ushindi ni wa Wazanzibari wote, na kumuomba rais mteule aongee na wenzake awasihi kuacha kubezana hasa baada ya utangazaji wa matokeo haya, kwani yanaweza kuleta mtafaruku.  
   
Na mwisho, alimwombea heri Rais mteule kwa Mungu ili amwongoze katika kazi zake, na kisha alikwenda kumpa mkono.   
Kusema ukweli, huu ni mfano mzuri wa kizalendo na kiungwana kwa mshindwa kukubali matokeo na kumpongeza aliyeteuliwa.   

Shein naye katika hotuba yake, baada ya kuishukuru tume na wagombea wenzake, amekiri kuwa kazi ya kuwania urais haikuwa rahisi, na ushindi wake anajua ya kuwa una changamoto za juu zinazomsubiri, na inahitaji busara kubwa katika kutekeleza uongozi mpya.  
   
Pia alijigamba kuwa hakubahatisha kugombea nafasi ya uongozi wa Zanzibar, kwani alikuwa anajiamini na alijua kuwa kazi hii angeiweza japo ni alitambua kuwa ni ngumu.  
  
Pia alimshukuru sana Maalim Saif Shariff Hamad kwa hotuba yake fupi na nzito, na amefarijika sana kutokana ana changamoto aliyoitoa Maalim, naye ameahidi kushirikiana na wazanzibari wote katika serikali mpya ya umoja wa kitaifa. Na Dk Shein, ameahidi kuisimamia serikali ya umoja wa kitaifa akishirikiana na Maalim Seif kama makamu wake.  
   
Shein ameahidi kuhakikisha kutakuwa na utulivu kama ulivyokuwa kabla ya uchaguzi, na kuwataka wazanzibari wafurahi wote kwa pamoja na kuijenga Zanzibar.

Cheo cha waziri kiongozi sasa ni kwa heri....

Mimi Nasubiri ya huku Tanganyika!!!