Member of EVRS

Friday, 12 November 2010

Anne Makinda: Mwanamke wa Kwanza Kuwa Spika wa Bunge la Tanzania


Mh. Anne Makinda (Pichani) amechaguliwa kuwa spika wa bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuchaguliwa na wabunge wa Tanzania kwa kura 265 na kumshinda mpinzani wake, Mh. Mabere Nyaucho Marando aliyepata kura 53.  
  
Ushindi huu ulitarajiwa ukizingatia idadi ya wabunge wa chama cha mapinduzi (CCM) anakotoka Anne Makinda kuwa wengi kwa zaidi ya 75% ya wabunge wote.  
 
Mh. Anne Makinda alikuwa naibu spika kwa miaka mitano iliyopita chini ya Mh. Samuel Sitta ambaye mwaka huu hakupitishwa kugombea kiti hicho na chama chake.   
  
Anne Makinda anaweka historia mpya ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo katika bunge la Tanzania.  

Katika hatua za mwanzo za mchakato wa uchaguzi, wakati Mh Marando anajieleza, ulipowadia wakati wa maswali, kulitokea tafrani ndogo ya mbunge mmoja mzoefu wa CCM kutaka kukiuka maagizo ya mwenyekiti aliyesimamia uchaguzi huo Mh. Anna Abdallah wa kutaka kuuliza swali kwa kutumia kipaza sauti ambacho mgombea ndio alikuwa anakitumia, na hivyo kupandisha munkari kidogo wa baadhi ya wabunge.  
  
Aliporuhusiwa kuuliza swali kupitia kipaza sauti kingine, ilibidi akatishwe kwani lilionekana halikuwa swali bali maelezo kinyume na yaliyotarajiwa, hata alipoambiwa kunyamaza, yeye aliendelea tu kuongea na kuonyesha ya kuwa hakuwa makini katika kutekeleza maelezo ya mwenyekiti wa kikao hicho.   
   
Tunasubiri changamoto nyingi katika bunge hili lililosheheni vijana wengi kuliko bunge lililopita wakiwamo vijana wa miaka 24 walioingia hivi karibuni.  
  
Hata hivyo, Stephen Wasira wa CCM, bado anashikiria rekodi ya kuingia bungeni akiwa kijana zaidi wakati huo akiwa na miaka 23 tu. na kwa sasa yupo bungeni kwa zaidi ya miaka 40.

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Safi kabisa huu ndio ule uanauke wa shoka ausemao da`Mija. Hongera sana Ana na nakutakia kazi njema na nzuri. Pamoja Daima. Wanawake oyeeeeee!!!!

SIMON KITURURU said...

Hongera Mwanamama!

Nje kidogo ya topiki:

Sijui kwanini kabla sijatoa pongezi hii nimejiuliza;

``Hivi tuwapongezapo watu huku kwenye mablogu hasa watu ambao labda hata BLOGU zenyewe hawazipitii sio kupoteza muda tu?

Ni kama ambavyo najiuliza kuhusu ile tabia ya kumwambia marehemu upumzike salama wakati hana uhai ambao labda ndio ungefanya astukie sifa zetu ,
Hivi hilo nalo sio kupoteza tu muda?


Nje zaidi ya topiki:

Naombea tu isije geuka kuwa fasheni kuwa JINSIA ya MTU ndio kigezo cha kupewa ofisi nasio UWEZO wa kazi,...

.... ili tusije jikuta hadi UMOJA wa WANAWAKE Tanzania unajikuta unalazimika katika kuhakikisha imo kwenye fasheni ya kisasa ya KUCHAGUA kwa kufuata JINSIA hata kama uwezo wa kazi haupo,...
...inabidi wamchague MWANAUME kuwa Kiongozi wao hata kama maswala ya WAMAMA /Wadada hayajui kihivyo.:-(

Nawaza tu kwa SAUTI!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ndio, simon, nini hasa maana halisi ya pongezi hata kama wangekuwa wanapitia blogu??

hivi mtu anapaswa kupongezwa kwa kutwishwa majukumu na lawama kibao?

lakini je, tunapaswa kuangalia jinsia ya mtu kama kigezo cha uongozi?

emu-three said...

TWAMTAKIA KAZI NJEMA

Fita Lutonja said...

tunamtakia ufanisi katika kuliongoza bunge make tumechoshwa na mafisadi