Member of EVRS

Sunday, 21 November 2010

Jumapili Njema

Jana modem yangu ya internet ilinigomea kabisa, nikashindwa kupata habari mpya.
Leo nimeshtukizwa na kuingia kazini tangu asubuhi mpakaaaa......

Hivyo nawatakia jumapili njema, na pia tuwaombee hao wanaume ambao wamezuka sasa na mtindo wa kuua familia zao kwa visu.  
  
Kwani hivi karibuni huko Kilimanjaro mtu kaua mama yake mzazi na watoto wake wawili, juzi tu, huko Kenya kuna mtu kaua mke wake mjamzito na watoto wawili kwa visu tena, mmoja tu wa miaka 3 ndio alikimbia. Halafu tena wiki kadhaa zilizopita jamaa mmoja tena huko Marekani mwenye asili ya Afrika, aliua mke na watoto wake wawili kwa mtindo huo huo. 
  
Bahati mbaya au nzuri kama utakavyochukulia wewe, wanaume hao wote nao walikufa aidha kwa kujiua au watu wenye hasira kali kuwamaliza!
 
Aaaah, nilishasahau, nilikuwa nataka kuwatakia jumapili njema tu!

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hao wanaume lazima watakuwa ahawana akili nzuri. Mungu amewahukumu.....Ahsante kwa habari hii ya kusikitisha!! Jumapili njema na wewe pia.

SIMON KITURURU said...

Jumapili njema kwako pia Mkuu!

emu-three said...

Mbona mimi sikusema, na wewe pia!