Member of EVRS

Friday, 30 October 2009

Mtafaruku wa Kubandika


Wapitiao njia hii mtaniwia radhi mkiona mambo hayaendi vyema.

Nimekuja kugundua unapoitwa kuwa msimamizi wa mitihani (external examiner) na kupewa jukumu la kutamka kwamba mtahiniwa huyu ameridhisha baraza la watahini na hivyo anastahili kufaulu mtihani ili asubiri graduation.. Ni adhabu kubwa.

Kwani inabidi na wewe urudi tena kwenye vitabu na kubukua ili mtahiniwa asije akakugonga nyundo ya kisogoni.

Kwa wiki mbili zijazo nitakuwa na kibarua cha kutoa maamuzi hayo. Mkiona blog imevaa suruali pwete, basi mjue vijana wamenitolea macho kweli kweli. Taabu lugha... kifaransa na kiingereza, lazima uvume kotekote ili wasikupige chenga.

Wikiendi njema

Wednesday, 28 October 2009

Norway: Wizi mwingine!! (Interesting smuggling)


Kijana wa miaka 22 kutoka Norway amekamatwa na polisi wa Norway akiwa anatokea Denmark baada ya kukutwa akiwa ameficha viumbe tambazi mbalimbali wakiwamo chatu wadogo 14 (royal pythons) kwenye mwili wake.

Polisi walikuwa katika upekuzi wa kawaida kwa kijana huyo na ndipo walipomuona buibui katika mizigo yake.

Kilichowashangaza zaidi, waliona mwili wa kijana huyo unachezacheza kila mahali muda wote ingawa yeye alikuwa ametulia, na ndipo walipomshtukia kuwa ni mwizi wa viumbe hai, na hivyo kuamua kumpekua mwili wote.
Walichokikuta kiliwaacha midomo wazi.
Kijana huyo amekubali kulipa faini ya pound 1380 ili aweze kuachiliwa
For more information in english, read here

Tuesday, 27 October 2009

Protects eyes of Less Privileged Children

Children born in many African countries do not receive more attention as far as eye care is concerned.

A good number of them are born in semi-furnished hospital or maternity units, and another big group are delivered at home with assistance from traditional birth attendants. Luckily many survives due to many factors. This doesnt mean that infant mortarity rate is low.

Among the commonest eye problem noted immediately after delivery, is neonatal conjunctivitis which can be caused by germs mostly from the mother's birth canal, however, some of them can acquire the infection during the delivery process or shortly after delivery if level of eye hygiene is poor.
Serious complications can come from diseases like gonorrhoea and chlamydia.

Typically the child presents with eye discharge which can be copious and eyes may be swollen sometimes grossly. The child might cry like ringing bell.
If no treatment is given, the child might suffer severe complications including perforation of the eyes and blindness is a life long painful end result.

It is unfortunate that in many African rural hospitals they do not provide eye treatment immediate after birth which can help to reduce incidences of neonatal eye infections.

It has been recommended to give antibiotics eye drops immediately after delivery. Drugs such as rifamycine eye drops are effective for both chlamydia and gonococcal conjunctivitis, therefore it is wise to give this treatment as prophylaxis (protection) immediately after delivery. The major problem is availability of such drugs in the rural communities where more than 70% of children are born there.

Let's improve the eye health of the less privileged children. Let's help them.
P'se, send to me your concern at this post or via my email: chi.bue@gmail.com

Omba omba anapokuwa kero


Jaribu kufikiria ya kwamba upo kwenye gari la kuazima, na mfukoni mwako umewakiwa jua kali sana. Na kwa wakati huo uko kwenye mzongo wa mawazo maana mshahara wa mwezi umechelewa kutoka, na wakati huohuo unadaiwa kodi na mwenye nyumba.

Halafu anakuja ombaomba, tena mama mtu mzima na kukuomba kwa heshima zote. Na kwa sababu huna unamjibu kwa heshima pia kuwa siku hiyo hali yako kifedha sio nzuri.

Kinachofuatia hapo ni huyo ombaomba kusema maneno ya kukulaani ati kwamba usipompa basi utapata mkosi, na wala hutafanikiwa, na kama haitoshi anakutukana kabisa na kuongeza kwa kukuita wewe ni bahili wa kutupwa.

Ukipenda kupata utamu wa habari hii, jaribu kuwa unaenda kivuko cha feri upande wa Kigamboni, na sharti uwe na gari hata la mtumba uliloliazima kwa mtu... ila nakushauri usiwe na hasira.

Saturday, 24 October 2009

Uingereza: Mgomo Katika Shirika la Posta


Wafanyakazi wa shirika la posta la Uingereza (Royal Mail) walikuwa wametangaza mgomo wa siku 3 ili kushinikiza serikali yao kuwaongezea malipo ya mishahara.

Inasemekana serikali ilitangaza nafasi za kazi za muda zipatazo 30,000 kwenye posta hizo. Bila kutarajiwa na wengi, walijitokeza watu zaidi ya 100,000 kuomba nafasi za kazi hizo za muda.

Mpaka sasa inadaiwa ya kuwa shirika hilo lina barua na mizigo ya wateja ipatayo milioni 30 iliyokwama na wanajitahidi kuifikisha kwa wateja haraka kabla ya mgomo mwingine haujaja. Hii ni kutokana na msemaji wa shirika hilo, lakini baadhi ya wafanyakazi wamedai taarifa hiyo si ya kweli, bali idadi inakadiriwa kufika milioni 65!

Sina hakika ingekuwaje kama ingetokea Bongo!

Thursday, 22 October 2009

Chaos in Brazil


Above: Remains of the police chopper after it was shot down by gang.

At least 32 people have been killed since last Saturday in Rio de Janeiro
The fighting erupted at the weekend when a police helicopter was shot down by suspected drug traffickers. Police interrupted the gun battles between drug gangs before this tragedy.

The violence comes just weeks after Rio was chosen to stage the 2016 Olympics.Feuding between rival drug gangs across several shantytowns (above the burning bus in one of the shanty towns) in the north of Rio that began on Saturday seems to have started a grim sequence of events that has yet to reach a conclusion, says the BBC's Brazil correspondent Gary Duffy.
This level of crimes......., it seems the 2016 olympic people have to go with bullet and grenades-proof vests!!

Bremen: Child Friendly Airport


When you arrive at Bremen Airport in Germany, you will always meet smiling faces ... from children.
They never become tired to enjoy their exclusive place for playing while waiting for their travel or visitors.
I congratulate Bremen airport authority for such considerations.

Wednesday, 21 October 2009

With a Light Touch

A man was just waking up from anaesthesia after surgery, and his wife was sitting by his side. His eyes fluttered open and he said,
Man: "You're beautiful." Then he fell asleep again.

His wife had never heard him say that, so she stayed by his side and thanking God that finally he has changed.
A few minutes later, his eyes fluttered open and he said,
Man: "You're cute!"

The wife was disappointed because instead of "beautiful," it was now "cute."

Woman: "What happened to 'beautiful'?"
Man: , "The drugs are wearing off!" then he fell asleep again.

Tuesday, 20 October 2009

Extended prunning!!


Last week I left my home in the morning for work... You know, I like gardens and trees, you can call me in any way, Nature conservator etc.
So... I left my growing garden like ... as you see above photo...
But, my gardener was too "clever", and he decided to "clean up" the environment...And that is what I found in the evening... My gardener was busy "prunning" at this level!!
I dont know.... But.. I could not believe my eyes .... right after I enter the gate.It will take some time before seeing my trees growing again.


Kama kawaida, onyo kali ni lazima utoe kwa ukataji wa miti wa namna hii.

Sunday, 18 October 2009

Mafua ya Nguruwe - Rwanda

Wiki iliyopita nilitoa taarifa ya ugonjwa wa mafua ya nguruwe kuingia hapa Rwanda baada ya kumpata waziri wa serikali.

Hali ilikuwa ya kuogofya kwa watu wengi, hasa ilipogundulika ya kuwa kuna watu 12 wamekwisha ambukizwa kwa muda mfupi sana ikiwemo na watoto wa waziri mwenyewe.
Mpaka sasa hakuna kifo kilichotokea na wagonjwa wote wanaendeelea vizuri.

Mwanzoni mwa wiki hii. Mkuu wa idara ya watoto katika hospitali alipolazwa mtoto wa waziri huyo aliyeleta mafua hayo Rwanda kwa siku 2 na kuruhisiwa baada ya kuendelea vizuri, alifukuzwa kazi wakisema idara yake ilifanya uzembe kwa kushindwa kugundua ugonjwa huo mapema. Hakupewa nafasi hata ya kujieleza na kitendo hicho kiliwaudhi wafanyakazi wenzake.

Hata hivyo, waziri wa afya ameingilia kati suala hilo na kuliangalia upya kwani inaonekana hatua iliyochukuliwa ilikiuka ngazi mbalimbali.

Wednesday, 14 October 2009

Biased Information Search in GoogleOver weekend I was looking for information about Barack Obama, someone iterrupted me and he asked me to find another word for smiling, out of my mind I type the word smiling without cancelling my previous search at the google search.

I was puzzled to see all those options which do not tie on what I was looking!! But it was an interesting results

I decide to try other way round


Then went back to my famous name, and well......, is my biased computer


So another trial with different name, well.....no confusion from web search, should....... Ithink it is your turn to try...

Nyerere: Akumbukwa Rwanda baada ya miaka 10 ya Kifo Chake


Wanyarwanda waliowahi kuishi Tanzania kama wakimbizi leo wanaadhimisha miaka 10 tangu kutokea kifo cha mwalimu Nyerere kwa shughuli kubwa ambayo wameiandaa kwa siku kadhaa.

Ili kufanukisha shughuli hiyo walikuwa wanapitia sehemu mbalimbali kukusanya michango na pia kufafanua umuhimu wa kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika ukombozi wa bara la Afrika na pia msimamo wake wa kukemea mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 hapa Rwanda.

Umoja wao ambao una jina la kiswahili, umekuwa na matukio mengi ya kuendeleza mshikamano kama walivyojifunza Tanzania, na kila mwaka huadhimisha siku ya Nyerere kuliko hata watanzania wanaoishi hapa Rwanda.

Tunashukuru juhudi za ubalozi wa Tanzania hapa Rwanda kwa kufanya juhudi za kuanzisha Umoja wa watanzania wanaoishi hapa Rwanda hasa baada ya kuzindua rasimu ya katiba ya umoja huo, ambao utaanzishwa rasmi kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Watanzania tudumishe mshikamano wetu, na kuenzi yale yote mema aliyotuachia hayatai Baba wa Taifa, hayati Julius Kambarage Nyerere.

Dalili za Ugonjwa wa mafua ya Nguruwe (Swine Flu)

Juzi nilizugumzia ujio wa mafua ya nguruwe hapa Rwanda.

Kuna baadhi ya wadau walitaka kufahamu zaidi habari ya mafua ya nguruwe, napenda kumshukuru mdau wa blogu hii Dr Faustine ambaye ni Mtanzania na pia mtaalamu halisi wa matatizo yanayosababishwa na vimelea ( Consultant Microbiologist) ambaye anafanya kazi Center of Disease Control (CDC), ambao Makao makuu yao yapo Atlanta, USA. Na ndiyo wasemaji wakuu wa magonjwa yote ya milipuko na yale yanayosababishwa na vimelea duniani kwa kutoa ufafanuzi huu hapa chini:

Dr Faustine: Dalili za H1N1 au mafua ya nguruwe zinafanana na dalili za mafua ya kawaida ikiwa ni pamoja na homa, koo kuwasha, maumivu ya viungo, kujisikia kuchoka na baadhi ya watu hujisikia kutapika au kuharisha.

Ugonjwa huu unasambaa kwa kasi sana na si hatari kama ugonjwa wa mafua ya ndege.
Wengi ya wagonjwa wanaofariki huwa wana magonjwa mengine yanayowakabili.

Ugonjwa huu husambazwa kwa njia ya hewa pale mtu mwenye ugonjwa huu anapopiga chafya au kukohoa.

Mgonjwa anashauriwa kuziba kwa kitambaa au "tissue" wakati wa kupiga chafya au kukohoa.
Mgonjwa anashauriwa kuosha mikono mara kwa mara kwa maji na sabuni. Unaweza kutumia pia Alcohol-based hands cleaners.
Kuna dawa zinazoweza kutolewa kwa mgonjwa kama atawahi kwenda hospitali ndani ya masaa 72 baada ya kupata ugonjwa huu.

Ukihisi una dalili kama hizi unashauriwa kuonana na Daktari.

Tuesday, 13 October 2009

Hotuba Za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere

Kwa wale wapenzi wa hotuba za Baba wa Taifa, blogu ya Subi imetoa hotuba hizo, waweza kuzipata kama utatembelea blog yake hapa.

Tusisahau kwamba kesho ndio kumbukumbu ya miaka 10 tangu atutoke, lakini busara zake bado zipo miongoni mwetu.

Tunawatakia kila la heri katika Nyerer day

Monday, 12 October 2009

Swine Flu in Rwanda

Rwanda has been hit by swine flu for the first time.

It was at the end of last week when the first case of swine flu was diagnosed at Kigali when the two children of a state minister was found to be positive, later the minister was tested positive too, however the spouse to minister was negative.

This follows a short illness of high fever and flu, apparently the minister has a mild flu. Some few days ago, the minister was on the trip to USA with two children, and on arrival back they all suffer from flu, but one child was a little bit more ill and necessitate admission.

So far, 3 doctors who attended the child of minister and another student at the hospital where the child was admitted have suffered mild flu and have been quarantined. One patient who was admitted at the hospital (a child of minister), has been discharged under quarantined, and the condition of child was described as good.

Total of 12 cases has been reported so far including a child from the same school where the minister’s children studies. The school has been ordered to be closed for one week.

All cases are mild and no death has been reported.
Rwandan Minister for Health is working hard on the issue and has given an assurance that all precautious measures have been taken and people should not worry.

Huraaah. Today is my BDTraditionally, birthday is celebrated by family and friends gatherings, and of course they enjoy drinks and BD cake together without forgetting the special BD songs and cheers.
What happen if you are outer there and there is no body to join the party ..... Any idea on how to celebrate?
I decide differently, to eat the most delicious food which my mother taught me .... many years back, cooked in a traditional way.
Well, this was against my odds, usually I don’t spend much time in kitchen, but because it is my special day, I decided to prepare my organic food, purely traditionally…… I used a clay pot where all the foods were steamed in it after being wrapped in the banana leaf.
Then I had to prepare the juice which I extract from the mango without using a blender, just simple pounding and then juice was squeezed, nothing added, I mean even water was not added.
All these preparations consumed my precious one hour! And the final result was as you see above on the photo.....But I enjoyed my art and BD!
Huraaaaaaaaaah!

Saturday, 10 October 2009

Rogers Mtagwa Ashinda pambano la Ndondi la Dunia


Bondia wa kitanzania Rogers Mtagwa, mkazi wa Philadelphia ameshinda pambano lake la mkanda wa uzito mwepesi a.k.a. unyoya (featherweight) kwa kumtwanga kwa KO bondia Tomas Villa wa Mexico kwenye raundi ya 10.
Pambano hilo linatambuliwa na WBO lilikuwa gumu sana na ilikuwa kama inaelekea Rogers anazidiwa hasa raundi ya 9. Lakini katika raundi ya mwisho alimchapa Villa konde takatifu ambalo lilimwangusha, baada ya hapo Villa alikuwa anaona nyota tu mpaka mwamuzi alipolikatiza. Kuna baadhi ya mashabiki wameliita pambano la mwaka kwa jinsi ambavyo mabondia walivyokuwa wanaoneshana ufundi kila raundi ambapo ilikuwa vigumu kujua nani atashinda.

Hongera sana Bondia Rogers Mtagwa.

Friday, 9 October 2009

Weekend Message


Waooow, TGIF!
I just want to wish you a lovely weekend!


For me. It is time to stretch my muscles, my bike will take me at least 10km this time. Charity starts at home, even bike race... starts at home. It is good for your health.

Well...... I am preparing for olympic!!

Obama: Apata Nishani ya Amani ya Nobel 2009

Rais wa Marekani, Barack Obama, ameshinda tuzo ya amani na Nobel 2009 baada ya kushika madaraka ya urais kwa miezi 9 tu!

Kuchaguliwa kwake kumekuja kwa mshangao wa wengi na bla kutarajiwa, kwani watu wengi hawakuwa wamemfikiria, na katika majina yaliyokuwa yanatajwa hapo awali, yeye hakuwemo. Mpaka sasa haijajulikana ni nani aliyempendekeza.

Pia ni kiongozi wa kipekee ambaye amepewa tuzo hiyo kwa juhudi za amani, hata kabla matunda ya juhudi zake hayajaonekana hasa huko mashariki ya kati.

Wasemaji wanasema hili ni pigo jingine kwa utawala wa rais aliyemtangulia George Walker Bush ambaye utawala wake ulichukuliwa kuwa wa mabavu kwa nchi za mashariki ya kati.

Binafsi, nampongeza rais Obama kwa mafanikio na ushindi huo.

Thursday, 8 October 2009

Children!!They are curious, imitating, creative, fearless and yet do dangerous actsThis is extremely dangerousAlways keep an eye on them!!!

Kenya: Bomu Linalosubiri Muda Muafaka

Kumekuwa na fununu kuwa baadhi ya wananchi Kenya wameanza kukusanya silaha za moto kama maandalizi ya kujihami na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 1012.
Na pia kumekuwa na ongezeko kubwa la uhalifu kwa sasa, na matukio yamekuwa yakiongezeka kila siku.

Uchunguzi uliofanywa na BBC umebaini ni kweli kuwa watu wameanza kununua silaha, na hasa kutoka Somalia, na hata baadhi yao walipo hojiwa walikiri kuwa wameshanunua kwa nia ya kujihami.

Serikali ya Kenya imekuwa inapinga ya kuwa matukio kama hayo hayapo, isipokuwa imekubali ya kuwa matukio ya uhalifu yameongezeka.

Swali kubwa ninalojiuliza, je, ni kweli serikali ya Kenya ipo makini na suala hilo, au watendaji wanafurahia hali ya vurugu wakati wa uchaguzi ili waweze kufanya "mambo yao"!

Ikumbukwe, wanaoumia siku zote ni watu wa kawaida na wasio na hatia, wakati viongozi na wachochezi wa vurugu huwa salama salimini. Hatupendi hizo kafara za uchaguzi EA.

Wednesday, 7 October 2009

Around Our Sphere


There are several domestic animals which can be kept somewhere in our sphere. While in another area.... people can put all sorts of things to keep them away. The old lady in India try to feed the ...... guess for what!!

Below: Train in Indonesia!!Thai child (below) washing the pet!!This can be seen only in AustraliaAlas! Enjoy more the sphere by clicking here

Tuesday, 6 October 2009

Kuanzishwa kwa Jumuiya ya watanzania - Jimbo la Gauteng, SA

HIGH COMMISSION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA


Telephone:012- 342 4371/93
Fax: 012 – 430 43 83
E-mail: tanzania@cis.co.za
thc@tanzania.org.za
Website: www.tanzania.org.za


822 GEORGE AVENUE,
P.O. BOX 56572,
ARCADIA 0007,
PRETORIAUBALOZI WA TANZANIA NCHINI AFRIKA KUSINI UNAPENDA KUWATANGAZIA WATANZANIA WANAOISHI KATIKA JIMBO LA GAUTENG KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO WA WATANZANIA WANAOISHI KATIKA JIMBO HILO UTAKAOFANYIKA TAREHE 24 OKTOBA, 2009 SAA NANE NA NUSU MCHANA HADI SAA KUMI NA MOJA JIONI KATIKA UKUMBI WA PRETORIA COUNTRY CLUB, NAMBA 241 MTAA WA SYDNEY, WATERKLOOF, PRETORIA.
MKUTANO HUO UNA LENGO LA KUANZISHA JUMUIYA YA WATANZANIA KATIKA JIMBO HILO.

TAFADHALI TUNAOMBA KUVAA NADHIFU NA KUZINGATIA MUDA.

KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NA WAFUATAO:

1. Jumanne Fhika 0762 909449
2. Faustine Ndugulile 0799 965120
3. Laurean Rugambwa 0835 566966
4. Lumbi na Ethel 012 344371/012 3425921IMETOLEWA TAREHE: 3.10.2009

UBALOZI WA TANZANIA- PRETORIA

Monday, 5 October 2009

Have a Nice WeekYesterday was .. sunday. For christians, is a worship day. May be for the others is either a working day or resting day. It is not bad if you decide to rest and enjoy the evening sun, like what I was doing, especially when you are far away from your family and country.

But sometimes you may be tired to stay idol when you are alone .....Or yes, you can work up you brain into fine tune..... and enjoy yourself. Who told you that you have to sing and play music before people!!
And when you get on board.... you can dance in front of your house even on your own... this is part of physical exercises.

But be aware if you have visible fence around your house, people may wonder if you are ok.....
I Wish you a blessed week!
The photos were taken by auto camera

Friday, 2 October 2009

Eye Care Services in Tanzania - Huduma za Macho TanzaniaLast week I visited CCBRT hospital in Dar es Salaam at paediatric eye unit to see how they do visual assessment in children.
I was impressed by friendly environment for children in such a way ..... children's fear for being in hospital is simply thrown away right at the entrance door.

Photo below shows that the child do not enjoy only the painting........, but she is assessed on her colour vision, crude vision, activity and level of intelligence according to age.
There are 3 dedicated trained staff for visual assessment, refraction and low vision assessment in children.

Kuna vifa vingi ambavyo huwafanya watoto kusahau kana kwamba wapo hospitali.
Mdau huyo hapo juu alikuwa amegoma kuingia kwenye chumba hicho, lakini jicho lilipochungulia ndani, baaaasi, akawa mwenyeji kuliko wenyeji halisi.

Thursday, 1 October 2009

Education or Add question?!!!

This pupils... The only thing they enjoy in this classroom is the outside view.....
And sitting very close to the writing board is unhealthy!!

Baada ya hapo tunategemea watoto wetu waweze kufanya vizuri kama wale ambao wana kila kitu cha kuwasaidia kupata elimu. Kinachonitisha zaidi ni jinsi walivyokaa karibu kabisa na ubao, maana yake wakitumia chaki kuandika halafu mtu afute... vumbi lote linaingia ndani ya macho na pua, baada ya hapo wanapotea darasani wakiwa wagonjwa.