Member of EVRS

Saturday, 10 October 2009

Rogers Mtagwa Ashinda pambano la Ndondi la Dunia


Bondia wa kitanzania Rogers Mtagwa, mkazi wa Philadelphia ameshinda pambano lake la mkanda wa uzito mwepesi a.k.a. unyoya (featherweight) kwa kumtwanga kwa KO bondia Tomas Villa wa Mexico kwenye raundi ya 10.
Pambano hilo linatambuliwa na WBO lilikuwa gumu sana na ilikuwa kama inaelekea Rogers anazidiwa hasa raundi ya 9. Lakini katika raundi ya mwisho alimchapa Villa konde takatifu ambalo lilimwangusha, baada ya hapo Villa alikuwa anaona nyota tu mpaka mwamuzi alipolikatiza. Kuna baadhi ya mashabiki wameliita pambano la mwaka kwa jinsi ambavyo mabondia walivyokuwa wanaoneshana ufundi kila raundi ambapo ilikuwa vigumu kujua nani atashinda.

Hongera sana Bondia Rogers Mtagwa.

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana. natumaini meno yote yapo salama maana mchezo huo mmmhhh!!!

John Mwaipopo said...

wakati kuna watu wanakesha kuichafua nchi hii kwa ufisadi, kumbe kuna watanzania wanaokesha kwa mazoezi na ushujaa kuitukuza na kuitakasa kwa ushindi katika nyanja mbalimbali, ikiwemo michezo.

hongera roggers mtagwa. hongera tena na tena.

John Mwaipopo said...

mbona bondia huyo huyo kapigwa kwa michuzi.

Halil Mnzava said...

Tunampahongera,Anatuwakilisha.