Member of EVRS

Wednesday 14 October 2009

Dalili za Ugonjwa wa mafua ya Nguruwe (Swine Flu)

Juzi nilizugumzia ujio wa mafua ya nguruwe hapa Rwanda.

Kuna baadhi ya wadau walitaka kufahamu zaidi habari ya mafua ya nguruwe, napenda kumshukuru mdau wa blogu hii Dr Faustine ambaye ni Mtanzania na pia mtaalamu halisi wa matatizo yanayosababishwa na vimelea ( Consultant Microbiologist) ambaye anafanya kazi Center of Disease Control (CDC), ambao Makao makuu yao yapo Atlanta, USA. Na ndiyo wasemaji wakuu wa magonjwa yote ya milipuko na yale yanayosababishwa na vimelea duniani kwa kutoa ufafanuzi huu hapa chini:

Dr Faustine: Dalili za H1N1 au mafua ya nguruwe zinafanana na dalili za mafua ya kawaida ikiwa ni pamoja na homa, koo kuwasha, maumivu ya viungo, kujisikia kuchoka na baadhi ya watu hujisikia kutapika au kuharisha.

Ugonjwa huu unasambaa kwa kasi sana na si hatari kama ugonjwa wa mafua ya ndege.
Wengi ya wagonjwa wanaofariki huwa wana magonjwa mengine yanayowakabili.

Ugonjwa huu husambazwa kwa njia ya hewa pale mtu mwenye ugonjwa huu anapopiga chafya au kukohoa.

Mgonjwa anashauriwa kuziba kwa kitambaa au "tissue" wakati wa kupiga chafya au kukohoa.
Mgonjwa anashauriwa kuosha mikono mara kwa mara kwa maji na sabuni. Unaweza kutumia pia Alcohol-based hands cleaners.
Kuna dawa zinazoweza kutolewa kwa mgonjwa kama atawahi kwenda hospitali ndani ya masaa 72 baada ya kupata ugonjwa huu.

Ukihisi una dalili kama hizi unashauriwa kuonana na Daktari.

1 comment: