Member of EVRS

Tuesday 27 October 2009

Omba omba anapokuwa kero


Jaribu kufikiria ya kwamba upo kwenye gari la kuazima, na mfukoni mwako umewakiwa jua kali sana. Na kwa wakati huo uko kwenye mzongo wa mawazo maana mshahara wa mwezi umechelewa kutoka, na wakati huohuo unadaiwa kodi na mwenye nyumba.

Halafu anakuja ombaomba, tena mama mtu mzima na kukuomba kwa heshima zote. Na kwa sababu huna unamjibu kwa heshima pia kuwa siku hiyo hali yako kifedha sio nzuri.

Kinachofuatia hapo ni huyo ombaomba kusema maneno ya kukulaani ati kwamba usipompa basi utapata mkosi, na wala hutafanikiwa, na kama haitoshi anakutukana kabisa na kuongeza kwa kukuita wewe ni bahili wa kutupwa.

Ukipenda kupata utamu wa habari hii, jaribu kuwa unaenda kivuko cha feri upande wa Kigamboni, na sharti uwe na gari hata la mtumba uliloliazima kwa mtu... ila nakushauri usiwe na hasira.

2 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yule mama namfahamu na si lazima uwe na gari. eti ndo ubarikiwe na sio Mungu ampe yeye direct kwa hiyo yupo kupewa sadaka ili Mungu abariki na kunyimwa basi mkosi ni kama dini hivi

Anonymous said...

Huyo mama nimeshakutana naye kama mara 4, namfahamu, huwa nikimuona nawahi kufunga vioo potelea mbali joto liniumize kipindi anachopita maana nimegundua ukifunga kioo anapita tu.