Member of EVRS

Wednesday, 28 October 2009

Norway: Wizi mwingine!! (Interesting smuggling)


Kijana wa miaka 22 kutoka Norway amekamatwa na polisi wa Norway akiwa anatokea Denmark baada ya kukutwa akiwa ameficha viumbe tambazi mbalimbali wakiwamo chatu wadogo 14 (royal pythons) kwenye mwili wake.

Polisi walikuwa katika upekuzi wa kawaida kwa kijana huyo na ndipo walipomuona buibui katika mizigo yake.

Kilichowashangaza zaidi, waliona mwili wa kijana huyo unachezacheza kila mahali muda wote ingawa yeye alikuwa ametulia, na ndipo walipomshtukia kuwa ni mwizi wa viumbe hai, na hivyo kuamua kumpekua mwili wote.
Walichokikuta kiliwaacha midomo wazi.
Kijana huyo amekubali kulipa faini ya pound 1380 ili aweze kuachiliwa
For more information in english, read here

7 comments:

viva afrika said...

huyu jamaa ni mbunifu sana, angetusaidia sana kule mbagala kulikotokea bahati mbaya.

John Mwaipopo said...

Viva afrika kweli huyu jamaa ni mbunifu ila nina swali kuwa angetusaidiaje kule mbagala? nadhani unaongelea mabomu sasa angeyaficha kama hao viumbe au ingekuwaje. hebu fafanua-po.

Anonymous said...

Duh. Kama maana ndiyo hiyo, basi huyo jamaa hastahili kuwa mbagala, labda kama ataenda kwenye maficho ya Osama akawatoe baruti huko

Candy1 said...

I feel like screaming...mmh...

Jade said...

I actually screamed!My imagination was horrible!

~PakKaramu~ said...

Pak Karamu visiting your blog

SIMON KITURURU said...

Binadamu KIBOKO!

Wengine wakiona nyoka na mabuibui wanawaua na kwa wengine ni bonge la mfugo!

Just fikiria jinsi watu wanavyoingia mpaka ubunifu namna hii kisa kusafirisha nyoka, mijusi na Mabuibui!:-)