Member of EVRS

Friday, 30 July 2010

Wish you A nice Weekend of Prayers

Wale wote wanaotarajia mafanikio, basi mwishoni mwa wiki hii nimejitolea kuwaombea kwa dhati kabisa, na Mungu awatangulie ili wapate mafanikio yaliyotukuka kadri wanavyokusudia.

Na shetani ashindwe.

God bless You!

Wednesday, 28 July 2010

Un-expected Caption

This photo..... well, I call it un expected snap.

It was taken by a 5 years old child... no preps at all, This gentleman was busy arranging stuffs in the shopping bag.

Just a simple call.. hey, look up here..... I insit, that was a gentle yell from the child that could be picked by this man...

what was seen ... was just a flash of light, and laughter kwi kwi kwiii.

Hey Child... You Gonna be great photographer umh! That is what the man said

Sunday, 25 July 2010

Mkutano wa Watanzania waishio Rwanda

Jana tarehe 24 julai 2010, umoja wa Watanzania waishio Rwanda tulikutana kama kalenda yetu ilivyokuwa imepanga, ulikuwa ni mkutano wa kwanza baada ya kuanzisha rasmi umoja huu ambao kwa ufupi unaitwa UTARWA na ulifanyika katika eneo la ubalozi wa Tanzania, Rwanda.

Uongozi mpya wa umoja huu chini ya Mwenyekiti wetu Mama Josephine Marealle-Ulimwengu (Katikati katika picha hii chini) ulipanga mikakati mbalimbali ya kuuendeleza umoja huu katika mpangilio maalumu wenye viambatanisho na ufuatiliaji wa matukio mbalimbali ya umoja, ikiwa ni pamoja na malengo yanayokusudiwa kwa muda maalumu. Katika masuala muhimu yaliyojadiliwa ilikuwa ni pamoja na kuwa na ofisi ya kudumu ikiwa pamoja na samani, tovuti, na pia kuanzisha klabu kwa ajili ya kubadilishana mawazo na pia kuandaa matamasha ya michezo hasa ya kujenga afya.


Watanzania kwa umoja wao, waliweza kuchanga papo hapo pesa ambazo zilitosha kununulia mashine ya kudurufu karatasi.


Uongozi wa UTARWA, pia uliweka wazi kwa majadiliano mti wa mawasiliano waliouandaa, ambao utaweza kuunda mtandao wa Watanzania wote wanaoishi Rwanda. Njia hii itawezesha mawasiliano kuwa ya haraka.

Pichani juu, maelezo kuhusu mti wa mawasiliano yakitolewa kwa wajumbe wote ndani ya ofisi ya ubalozi wa Tanzania, Rwanda.
Shughuli nyingine ambayo uongozi umekuwa ukifanya, ni kuandaa tovuti ambayo itakuwa na taarifa za wanachama wote, ikiwa ni pamoja na familia zao kadri mwanachama atakavyojaza kwenye fomu maalumu ya kuingia uwanachama. Na hii data base itakuwa inaweza kuonwa na viongozi tu, iwapo mwanachama atataka taarifa zake, basi ataweza kuzipata.

Pichani juu, wakati wa utambulisho wa tovuti ya UTARWA, ambayo itakuwa na taarifa nyingi za nyumbani, hapa Rwanda, habari za magazeti na blogu mbalimbali.


Pichani juu, baadhi ya wajumbe wa UTARWA wakisikiliza kwa makini maelezo yanayohusiana na tovuti.
Katika shughuli zilizopangwa baadaye, ni kuchangisha pesa ili kutunisha mfuko wa jumuiya ya akina Mama wa Kitanzania waishio Rwanda, na vitaandaliwa vyakula maalumu vya kitanzania hapo tarehe 3 oktoba 2010.Friday, 23 July 2010

Rwanda: Kampeni za Uchaguzi wa Rais 2010

Rwanda inatarajia kufanya uchaguzi wa rais mwezi ujao katikati.
Kampeni zimeanza rasmi wiki hii na itachukua majuma sita tu kumaliza kampeni na wananchi kuchagua Kiongozi atakayewafaa kwa miaka mingione saba (7).

Rais wa sasa, Paul Kagame anatarajiwa kushinda uchaguzi huo kwa kuwa wananchi wengi bado wanamkubali sana, japo wapo wachache wasiomkubali, ndio demokrasia hiyo.

Kampeni zinaendeshwa kwa amani na utulivu, hakuna fujo, na wala sijaona polisi wakikimbizana na watu au kuvuruga mikutano.

Sijasikia madai ya rushwa wala hisia ya rushwa, japo yapo manung'uniko kidogo kwa wale walioshindwa kusajiri vyama vyao vya siasa kabla ya uchaguzi.

Pichani chini ni kampeni za chama kinachotawala cha Paul Kagame katika jimbo la Kaskazini, unaweza kushuhudia umatu wa watu unaokiunga mkono chama hiki ambao ulijitokeza kutoa mshikamano kwa mgombea wao Na hawa wa kijani chini ni wanachama na wapenzi wa Liberal Party wakiwa katika kampeni zao pia. Nao wana matumaini ya kushinda na kuweka historia kwa kuwa na rais wa kwanza kutoka katika chama chao.


Na wao wanatumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua kiongozi wanayeona atawafaa
Linganisha tena hapa, yaani siasa inataka moyo bwana...Thursday, 22 July 2010

Hurricane Alex: Gulf of Mexico Devastated

Just see the effect of Alex... before and after...


Wind was travelling at a speed of 160km/hr, heavy downpours followed shortly later. 8 lives were claimed.

1.


2.

after

3.

after
4.

after


Thanks mdau from Mexico for the link.
Pata zaidi hapaMonday, 19 July 2010

Vuvuzela Zaendelea Kuwa Maarufu

Kwa wale waliokuwa wanazichukia vuvuzela za Afrika Kusini itabidi wabadili mtazamo wao... Kwani inaelekea zinaweza kutumika kama alama ya upenzi wa mpira wa miguu au timu ya mpira wa miguu.


Ujerumani ambayo ilikuwa maarufu kupitia pweza wake waliyempachika jina la Paul, inaendelea kuwa maarufu zaidi bada ya kampuni moja huko kutaka kutengenezewa vuvuzela kwa makadirio ya awali waweke oda ya vuvuzela milioni 5 (5,000,000). Kwa sasa bado wapo kwenye mchakato mkubwa wa kuweza kubuni vuvuzela ambayo itakubalika kwenye soko lao.


Inapenda kufanya mabadiliko kidogo kutokana na vuvuzela za Afrika kusini, kwani inadaiwa zile za Sauzi, zimetengenezwa kwa plastic hafifu (cheap plastic), na wao hawawezi kuzipata hizo. Pia za kwao wanataka ziwe na uwezo wa kutokuharibu mazingira (environmental friendly).


Pia inapenda vuvuzela zao ziwe na rangi 3 kama ilivo bendera ya nchi yao, yaani nyeusi, manjano na nyekundu, na pia iwe nyepesi zaidi ambayo itapunguza gharama za usafiri.


Kwa kuzingatia malalamiko ya wanachi wa Ujerumani, ya kuwa walipokuwa wanaangalia runinga wakati wa kombe la dunia, vuvuzela zilikuwa zinavuma kama vile jamii fulani ya nyuki... kampuni hiyo inataka kubuni vuvuzela ambayo itakuwa na kipunguza sauti (Silencer) ili isiwe kero kwa mashabiki watakaokuwa karibu na hiyo vuvuzela.


Wataalamu wa vuvuzela wa Sauzi wamekuwa wakisisitiza kuwa vuvuzela nzuri ni ile kubwa, lakini wajua ukubwa wa vuvuzela, maana yake sauti yake nayo inakuwa kubwa, nafikiri ndio maana hao jamaa wanataka kipunguza sauti....


Namkumbuka rafiki yangu Fadhy amabye ana matumaini makubwa sana kwamba vuvuzela zitakuja kuwa maarufu sana, hasa kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Sunday, 18 July 2010

Kazi ya Kisiasa ndio Kwanza Inaanza

Mchakato wa kuwania nafasi za kisiasa unaanza rasmi kesho.


Wale wenye homa za uchaguzi, na hasa wale wanaowania kurudisha tena nafasi zao kisiasa zitaongezeka pale watakapojikuta wanapambana na watu mahiri zaidi yao.


Nawatakia mafanikio mema wote wale wenye nia thabiti ya kuchukua fursa ya kuwawakilisha vyema wananchi wao, na wale wanaofikiria kupata neema binafsi, na washindwe vibaya sana.


Tunaomba hekima za mwenye haki, kutuongoza tuweze kuchagua watu wanaotufaa na sio wanaojifaa.

Na pia tunawaasa hao wanasiasa ya kuwa, kuwania nafasi moja, sio tiketi ya kununiana na kuzusha ugomvi, mshindi ni mmoja tu hata kama wote ni wazuri kupindukia. Msianze kutafutiana Sangoma...


Good luck! - Kila la heri wanasiasa wote wenye mapenzi mema.

Friday, 16 July 2010

Enjoy your Weekend

Let's forget the hard times we had during the week long-days, and now let's focus on the most enjoyable coming weekend.

Nawatakia mapumziko mema ya mwisho wa wiki kwenu nyote!

Photo from techie.com.ph

Tuesday, 13 July 2010

FIFA 2010 World Cup Teams Ranked

FIFA had put a list of ranking for all 32 teams participated in 2010 world cup in South Africa.


Spain topping the list as the World cup champions followed by Netherlands and Germany


Ghana is the highest in Africa, and 7th overall. Followed by Ivory Coast as the second in Africa and 18th Overall and South Africa in 20th position.


The last world Cup Champions, Italy, has been ranked 26th and France is the worst by holding the 32nd position which is the last in this year's ranking. France were even beaten by North Korea who tailed on top of France at 31st position.


See the full list of FIFA WC 2010 ranking here

Friday, 9 July 2010

Octopus Paul: Pweza Maarufu Kuliko Wote Duniani

Pweza (pichani juu) ambaye anatunzwa kwenye nyumba maalumu ya viumbe maji (aquarium) huko Oberhausen, Ujerumani amejizolea umaarufu mkubwa kwa watu wa Ujerumani na kwingineko duniani mara baada ya kufanikiwa kubashiri matokeo ya timu ya Ujerumani kwenye kombe la dunia huko Afrika Kusini kwa kupatia kwa asilimia 100 ya matokeo yote ya Ujerumani.


Habari iliharibika pale alipobashiri kuwa Hispania itashinda dhidi ya Ujerumani, kwa mara ya kwanza aliwakasirisha wapenzi wa soka wa Ujerumani kwani hawakufurahia kushindwa kuingia fainali ya kombe la dunia. Na ni kweli usiku huo Ujertumani ilifungwa na Hispania.


Kwa sasa kuna washabii walikuwa wanataka huyo pweza achinjwe na wamle kabisa. Kwani hakutarajia awaangushe. Lakini wao si wa kwanza kudai achinjwe na kuliwa, walioanza ni wale wa Argentina, pale alipobashiri kushindwa kwa Argentina na kweli wakafungwa mabao mengi tu.


Kwa sasa washabiki wa Hispania wanaomba huyo pweza apewe ulinzi wa kutosha ili asiuwawe, kiasi kwamba na Kiongozia wa Hispania amemtumia Kansela wa Ujerumani, Angela Merkert kuongeza ulinzi kwa Pweza huyo ambaye amebatizwa jina la Pweza Paulo (Octopus Paul).


Leo anangojewa kutoa utabiri wa fainali kati ya Hispania na Uholanzi.


Sijui itakuwaje akitabili Uholanzi kushinda, wahispania nao wataomba achinjwe? Ikumbukwe kuwa wahispania wanapenda saaaaaaaaaana nyama ya pweza.

Kuna washabiki wanaomba atunzwe mpaka kombe la dunia la 2014!
Wamiliki wa pweza huyo wameshasema watamtunza kabisa


Yangu ni masikio na macho tuuuu.


Photo from Telegraph.co.uk

Wednesday, 7 July 2010

Netherlands Win For WC Finals Cheered by Many Africans


Netherlands qualified for the WC 2010 In South Africa over a narrow edge advantage over Uruguay, this has given some Africans fans big relief from the pain they suffered when Ghana was defeated by Uruguay in a controversial game through penalty shoot-out.
Many African fans were not happy when they saw Uruguay players lifts up Suarez in cheers after the penalt shoot-out, who apparently was red carded by handling the jabulani ball, which was heading into his team net, which eventually diminishes Ghana's hope to advance into semi-finals.
This was different as compared to Thierry Henry goal to lift up France to the WC, where French players sympathises somehow for the faulty action leading to exit of their opponent.

The memmory of South Africa to be defeated 3 - 0 by Uruguay had an added effect on South African fans.

Many South Africans whites also had a big smile for the same factors as other African football fans, but for them, it was more than that...., some of them, their ancestors originates from Netherlands, so it was big cheers for them after South African team earl elimination and the last hope for Africa continent... Ghana exit.
It was agreat celebrations too for Dutch people all over the world.
German team is a favourite to win today for the second semi-final game, however, I prefer Spain to qualify for this year Finals!!
Photo by BBC

Monday, 5 July 2010

Polisi wa Tanzania Wajilipua na Kufa....Kulikoni?!!!!!

Hivi karibuni kumekuwa na matukio kadhaa ya polisi wa Tanzania kujiua kwa kujipiga risasi!

Matukio matatu Yamekwisha ripotiwa kwa siku za hivi karibuni, Kwa kuanzia huko Kigoma, wikiendi tukasikia mwingine huko Dar es Salaam, ambaye aliacha ujumbe kwenye kitabu cha taarifa za kipolisi kwamba mtu yeyote asisumbuliwe kwa maamuzi yake hayo, na inasemekana aliwapigia simu baadhi ya jamaa zake kuwaaga kabla ya kuzima simu na kujilipua kichwani..... na leo tumesikia huko mkoani Mara kwa polisi mwingine kujilipua na bunduki ikidaiwa alifanya kitendo hicho baada ya kunyakua bunduki kwenye kituo cha polisi alipokuwa amewekwa kwa mahojiano, na alifanikiwa kukimbilia ofisi ya kamanda wake na kujifungia.

Mkuu wa polisi Tanzania, Saidi Mwema, alisema baadaye ilisikika milio ya risasi kutoka katika ofisi askari huyo alipokuwa amejifungia, na baadaye alikutwa si yeye tena!

Chanzo cha askari huyo kuhojiwa, inadaiwa kwamba aliuelekeza vibaya msafara wa Rais Kikwete, na kusababisha msafara huo kugawanyika.

Bado natafakari kwa sauti... Kuna tatizo gani katika jeshi letu la polisi?
Mafunzo ya ujasiri na kukabiliana na vikwazo kweli wanapata hawa walinda usalama wetu?
Je, mazingira ya kazi yanawachanganya mpaka wanafikia uamuzi mbaya kwa muda mfupi sana tu!

Nafikiri jeshi la polisi lisipuuzie matukio kama haya, linapaswa kujichunguza kwanza katika sekta zote zikiwa pamoja na utawala, maadili, mishahara, haki za polisi, sifa za mtu kujiunga na jeshi la polisi na wakufunzi wa mafunzo ya upolisi.

Saturday, 3 July 2010

Company Names!


I have no comment regarding the name of insurance Brokers