Member of EVRS

Friday 23 July 2010

Rwanda: Kampeni za Uchaguzi wa Rais 2010

Rwanda inatarajia kufanya uchaguzi wa rais mwezi ujao katikati.
Kampeni zimeanza rasmi wiki hii na itachukua majuma sita tu kumaliza kampeni na wananchi kuchagua Kiongozi atakayewafaa kwa miaka mingione saba (7).

Rais wa sasa, Paul Kagame anatarajiwa kushinda uchaguzi huo kwa kuwa wananchi wengi bado wanamkubali sana, japo wapo wachache wasiomkubali, ndio demokrasia hiyo.

Kampeni zinaendeshwa kwa amani na utulivu, hakuna fujo, na wala sijaona polisi wakikimbizana na watu au kuvuruga mikutano.

Sijasikia madai ya rushwa wala hisia ya rushwa, japo yapo manung'uniko kidogo kwa wale walioshindwa kusajiri vyama vyao vya siasa kabla ya uchaguzi.

Pichani chini ni kampeni za chama kinachotawala cha Paul Kagame katika jimbo la Kaskazini, unaweza kushuhudia umatu wa watu unaokiunga mkono chama hiki ambao ulijitokeza kutoa mshikamano kwa mgombea wao Na hawa wa kijani chini ni wanachama na wapenzi wa Liberal Party wakiwa katika kampeni zao pia. Nao wana matumaini ya kushinda na kuweka historia kwa kuwa na rais wa kwanza kutoka katika chama chao.


Na wao wanatumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua kiongozi wanayeona atawafaa
Linganisha tena hapa, yaani siasa inataka moyo bwana...



No comments: