Member of EVRS

Monday, 5 July 2010

Polisi wa Tanzania Wajilipua na Kufa....Kulikoni?!!!!!

Hivi karibuni kumekuwa na matukio kadhaa ya polisi wa Tanzania kujiua kwa kujipiga risasi!

Matukio matatu Yamekwisha ripotiwa kwa siku za hivi karibuni, Kwa kuanzia huko Kigoma, wikiendi tukasikia mwingine huko Dar es Salaam, ambaye aliacha ujumbe kwenye kitabu cha taarifa za kipolisi kwamba mtu yeyote asisumbuliwe kwa maamuzi yake hayo, na inasemekana aliwapigia simu baadhi ya jamaa zake kuwaaga kabla ya kuzima simu na kujilipua kichwani..... na leo tumesikia huko mkoani Mara kwa polisi mwingine kujilipua na bunduki ikidaiwa alifanya kitendo hicho baada ya kunyakua bunduki kwenye kituo cha polisi alipokuwa amewekwa kwa mahojiano, na alifanikiwa kukimbilia ofisi ya kamanda wake na kujifungia.

Mkuu wa polisi Tanzania, Saidi Mwema, alisema baadaye ilisikika milio ya risasi kutoka katika ofisi askari huyo alipokuwa amejifungia, na baadaye alikutwa si yeye tena!

Chanzo cha askari huyo kuhojiwa, inadaiwa kwamba aliuelekeza vibaya msafara wa Rais Kikwete, na kusababisha msafara huo kugawanyika.

Bado natafakari kwa sauti... Kuna tatizo gani katika jeshi letu la polisi?
Mafunzo ya ujasiri na kukabiliana na vikwazo kweli wanapata hawa walinda usalama wetu?
Je, mazingira ya kazi yanawachanganya mpaka wanafikia uamuzi mbaya kwa muda mfupi sana tu!

Nafikiri jeshi la polisi lisipuuzie matukio kama haya, linapaswa kujichunguza kwanza katika sekta zote zikiwa pamoja na utawala, maadili, mishahara, haki za polisi, sifa za mtu kujiunga na jeshi la polisi na wakufunzi wa mafunzo ya upolisi.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mungu ibariki Tanzania yetu Hata mie nimeanza kuogopa pia kuwaza kwa sauti kuna nini tena?

Upepo Mwanana said...

Watu wamechoka na maisha, hali ngumu sana