Member of EVRS

Sunday 30 September 2012

Adha na Raha ya Kazi ya Huduma kwa Jamii

Kazi zinahusiana na kutoa huduma kwa jamii zina raha zake na karaha zake.
Kazi hizi ni kama vile za siasa, sekta ya afya, polisi, huduma za hoteli na migahawa, benki na kadhalika.

Wakati wote unahitaji kuwa mchangamfu na unayejali.

Hata pale anapokuja mtumishi wako wa nyumbani, ule ukali wako wooote, unayeyuka anapokuja ofisini kwako kwa ajili ya kupata huduma.

Lakini sina hakika kama watu wote wanakuwa hivi....
Nilikuwa nawatakia wikend njema tu!

Wednesday 12 September 2012

Mfanyakazi Takukuru - Ngara Ajiua kwa Kujipiga Risasi

Mfanyakazi mmoja wa TAKUKURU wilaya ya Ngara, siku chache zilizopita alijiftyatulia risasi na kufa papo hapo kwa sababu ambazo bado hazijafahamika. 
  
Mfanyakazi huyo kazi yake kubwa ilkuwa ni ya masuala ya usalama na utunzaji wa zana za moto (silaha), ambaye pia ni mwenyeji wa mkoa mmojawapo wa nyanda za juu kusini magharibi mwa Tanzania, ambapo mkoa huo hapo awali ulikuwa na sifa ya wenyeji wake kujiua pale wanapoudhiwa kupita kiasi.    
  
Chanzo cha mtu huyo kufikia uamuzi mgumu kama huo hakijajulikana wazi, japo inasemekana alitakiwa kutoka kwenye kikao ambacho kinahisiwa kilitakiwa kukaa na kumjadili yeye. 
  
Alipotoka nje ya kikao, muda mfupi baadaye ulisikika mlio wa risasi, jambo ambalo lilizua taharuki kutoka kwa wajumbe waliokuwa kwenye kikao cha kazi na kuwafanya wakimbie hovyo huku wakisigana kupita kwa kasi ya ajabu kwenye mlango wa kuingilia kwenye chumba hicho cha mkutano.  
  
Habari zaidi zinadai ya kuwa funguo za chumba cha silaha alikuwa amekwisha kuzikabidhi kwa mamlaka husika kazini kwake, na kuna hisia labda alikuwa amekwisha itoa silaha iiyomuua, au alikuwa janja na kutoa nakala ya ufunguo  wa chumba cha kuhifadhia silaha za moto. 
 

Saturday 8 September 2012

Dedicated to You!

Masseter Muscles!