Member of EVRS

Saturday, 24 September 2011

Chombo cha Utafiti wa Anga cha NASA Hakijulikani Kimeangukia Wapi

mchoro wa kuigiza wa chombo kinapolipuka moto mara kiingiapo katika anga ya Duni
Chombo cha angani (Satellite) kinachomilikiwa na NASA, ambacho kilikuwa anagani kwa zaidi ya miaka 20 kikifanya utafiti wa hali ya hewa, kwa sasa kinasemekana kimekwisha rejea duniani, inasemekana wamiliki wa chombo hicho (NASA) wanahisi kwa kiasi kikubwa kimekwisha anguka duniani, japo hawajui ni sehemu gani kimeangukia.  
   
Awali walitegemea kingeanguka katika bahari ya Pacific, lakini katika hali isiyokuwa ya kutarajiwa, kilipoingia kwenye anga ya dunia (Earth atmosphere) kilionekana kama kimepunguza kasi ya kuanguka, hivyo badala ya kutarajiwa kuanguka siku ya ijumaa, NASA ilikadiria kitaanguka jumamosi usiku au jumapili alfajiri. 
  
Chombo hicho chenye ukubwa kama wa basi kubwa, na kinachokadiriwa kuwa na uzito wa tani 6, mpaka sasa hakijulikani kilipo, na wala hakuna mtu aliyekwisha kutoa taarifa kama wameona mabaki yake. Na kwa kuwa mpaka sasa hivi NASA haijapokea taarifa yoyote ya majeruhi au madhara ya aina yoyote, wanaamini chombo hiki kimeanguka baharini, lakini hawajui ni sehemu gani.  

Bado wantafuta habari ya wapi mabaki ya chombo hiki yataonekana ili wawe na uhakika ya kuwa ni kweli kimekwisha anguka kwenye uso wa dunia. 
  
Pata habari zaidi hapa

Friday, 23 September 2011

Chama cha Upinzani Chashinda Uchaguzi Mkuu wa Zambia

Chama cha Upinzani  nchini Zambia, Patritic Front kimefanikiwa kupata ushindi wa urais pale bwana Michael Chilufya Sata (Miaka 73) alipotangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo.
Ukiwa ni msimu wake wa nne kwa bwana Sata kugombea nafasi hiyo, safari hii amefanikiwa kumshinda bwana Rupiah Banda, ambaye ndiye alikuwa anashikilia wadhifa huo.  
  
Uchaguzi huu kwa mara ya kwanza ulileta tafrani ambayo ilisababisha Tanzania, ambao ni nchi jirani na Zambia kwa upande wa kaskazini, kufunga mpaka wake na Zambia kuepusha wimbi la wakimbizi na waleta fujo kuingia Tanzania bila mpangilio. 
 
Sata amepata jumla ya 43% ya kura zote halali zilizopigwa, akifuatiwa na Bwana Banda aliyepata 36% ya kura zote halali zilizopigwa. 
  
Ninahisi ya kuwa uchaguzi huu wa Zambia utakuwa umetoa funzo fulani kwa siasa za kiafrika na hasa nyumbani kwetu Tz na nchi nyingine kama Zimbabwe na Uganda.  

Wednesday, 21 September 2011

Life is Full of Challenges! Python Hunting

How can you get hold of python without causing harm to it and yourself!

Follow very few and courageous steps like these gentlemen!

 Ensure security for your hand skin, because this will be hand python will try to attack or swallow. Animal skin is the best fooling instrument for the python, It smell like its favourable food eeeh!
Aye, also you avoid to go to hospital for unnecessary anti-tetanus vaccinations.

 Somebody waiting should have very good ears and strong to pull you when the time is due to do so...


 You see good source of natural light which is somehow fearful for the python
But, of course will make you see better...

 Be alerted, very sharp and each hand ready for action...

 Hurrraaaaah!..... Then shout to be pulled out


 Proud python catcher

They consider very well animal rights!! Where are they heading to? May be to a zoo, or return it to the thick forest to protect their domestic animals which are favourite meal for the "stranger" or to sell it to mafisadi!!

I wish I could have known the source of this....., but thanks Mdau for reviving photos.

RwandAir Promotes its Services by Cutting down Fares

Passengers, over the weekend, cashed in on RwandAir’s new promotional fares as charges for the Kigali-Entebbe were slashed to US$100 and US$200 for the economy and business class, respectively.
Usually, fares on the same route range between US$320 and US$450, depending on departure time.
John Mirenge, the national carrier’s CEO, on Sunday said feed-back from their customers ‘has been great.”
“It is part of our scheme to make flying affordable to people in the region, to make sure that more people are attracted to flying other than the usual road transport,” Mirenge said.

“They [passengers] are really excited about it! Feed-back is great. Time and again, we do it. We want more people to fly.”
RwandAir’s new promotional fares are also in celebration of the inaugural flight of the new Boeing 737-800NG.
On last Saturday, fares for the Kigali-Johannesburg were pegged at US$200 and US$400, for the economy and business classes, respectively.
On monday, passengers on the Kigali-Kilimanjaro/Dar es Salaam route cashed US$180 and US$320, for the economy and business classes, respectively.
Yesterday, Tuesday, the Kigali - Libreville/Brazzaville route cost US$$200 and US$500, for the economy and business classes, respectively, while the Libreville-Brazzaville will be set at US$$250 and US$$350.
Next Saturday, for the popular Kigali-Nairobi route, passengers will pay US$ 150, and USD 300 for Business class.

Source: New Times

Friday, 16 September 2011

Hatimaye! Tanzania yapata medali yake Mashindano ya Afrika

Timu ya taifa ya mpira wa pete, Taifa Queens, hapo juzi iliipatia medali Tanzania kutoka katika mashindano ya Afrika, baada ya kuifunga timu ya akina dada wa Botswana kwa 43 - 35 na hivyo kuchukua medali ya fedha katika mashindano hayo.
Waliochukua medali ya dhahabu ni Uganda, na ya shaba ni Zambia.

Timu ya Tanzania, ilipoteza michezo 2 kati ya 8 iliyocheza, na ilifungwa na timu za Uganda 52-41 na Zambia 46-42 pekee, ambazo zote hizi ndio zilizofanikiwa kutwaa medali katika mchezo huu.

Hata hivyo Tanzania waliwazidi Zambia kwa idadi ya magoli, kwani walikuwa waanalingana kwa alama.

Michezo waliyocheza:

Waliwafunga
Kenya 36 - 35
Ghana 94 - 24
Mozambique 92 - 8
Zimbabwe 38 - 27
South Africa 32 - 29
Botswana 43 - 35

Tunaipongeza timu ya Taifa Queens kwa kutuondolea fedheha ya muda mrefu.

Picha kutoka Star Africa

Thursday, 15 September 2011

Mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa Tanzania Bara Septemba 2011

Ifuatayo ni orodha ya wakuu wapya wa mikoa, na kituo walichotoka

1. Bw. Saidi Mecki Sadiki DAR ES SALAAM  Kutoka RC - Lindi

2. Bw. John Gabriel Tupa MARA Kutoka DC - Dodoma

3. Bw. Saidi Thabit Mwambungu RUVUMA Kutoka DC - Morogoro

4. Kanali Joseph Simbakalia MTWARA Kutoka RC Kigoma

5. Bi. Chiku S. Gallawa TANGA Kutoka DC - Temeke

6. Bw. Abbas Kandoro MBEYA Kutoka RC Mwanza

7. Bw. Leonidas T. Gama KILIMANJAROKutoka  DC – Ilala

8. Dkt. Parseko Ole Kone SINGIDA Kutoka RC Singida

9. Eng. Stella Manyanya RUKWA Kutoka Mbunge Viti Maalum

10. Bibi Christine Ishengoma IRINGA Kutoka RC Ruvuma

11. Dk. Rehema Nchimbi DODOMA Kutoka DC - Newala

12. Bw. Elaston John Mbwillo MANYARA Kutoka DC – Mtwara

13. Col. Fabian I. Massawe KAGERA Kutoka DC - Karagwe

14. Bibi. Mwantumu Mahiza PWANI Kutoka Mbunge/Naibu Waziri Mstaafu

15. Bibi. Fatma A. Mwassa TABORA Kutoka DC - Mvomero

16. Bw. Ali Nassoro Rufunga LINDI Kutoka DC - Manyoni

17. Eng. Ernest Welle Ndikillo MWANZA Kutoka DC - Kilombero

18. Lt. Col. Issa Machibya KIGOMA Kutoka RC Morogoro

19. Bw. Magesa S. Mulongo ARUSHA Kutoka  DC - Bagamoyo

20. Bw. Joel Nkaya Bendera MOROGORO Kutoka Mbunge/Naibu Waziri Mstaafu

21. Bw. Ludovick Mwananzila SHINYANGA Kutoka Mbunge/Naibu Waziri Mstaafu


Waliostaafu ni
Bw. Mohammed Babu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera;
Bw. Isidore Shirima aliyekuwa Arusha;
Kanali (mst.) Anatory Tarimo aliyekuwa Mtwara;
Bw. John Mwakipesile, aliyekuwa Mbeya.
Kanali Enos Mfuru aliyekuwa Mara;
Brig. Jen. Dk. Johanes Balele aliyekuwa Shinyanga;
Meja Jen. Mst. Said S. Kalembo aliyekuwa Tanga.
Wakuu wa Mikoa wanne waliostaafu ambao watapangiwa vituo vingine vya kazi ni
Bibi Amina Mrisho aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani;
Dk. James Msekela aliyekuwa Dodoma;
Bw. Abeid Mwinyimusa aliyekuwa Tabora
Bw. Daniel Ole Njoolay aliyekuwa Rukwa.

Taarifa kutoka blogu ya Ikulu-Tanzania

Tuesday, 13 September 2011

Miss Universe 2011 is Miss Angola

Katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa... hata sijui niiteje kwa kiswahili, yaliyofanyika Sao Paulo, nchini Brazil masaa machache yaliyopita, Mrembo kutoka Angola, Lopes, mwenye asili ya Cape Verde, amefanikiwa kushinda mashindano hayo kwa mwaka huu na hivyo kuwa miss Universe 2011.

After being crowned as Miss Universe 2011

She could not believe her ears!


When she was announced among the top 16. On her right background, is Tanzanian model
 
Top 10
 Kwa habari zaidi just click here

Monday, 12 September 2011

Sad News: Fire Tragedy in Nairobi, Kenya

East Africa has faced another bad traged within few daysy. This time has occurred in Nairobi slums along the Lunga lunga road named Sinai. The fire, erupted today 12th September 2011 in the morning hours.  

 
More than 100 Sinai residents have been confirmed dead and nearly 120 have been admitted in Kenyatta National hospital in Nairobi for emergency treatment, some of them have serious burns where they requires fluid and blood transfusion immediately. 
  
The source of the fire has not been identified yet, however there is a rumour that it was started by a Sinai resident who was trying to siphon petroleum from the pipeline, and during the course of drilling, the fire erupted with thunderous bang and huge flames scattered all around. 
  
The damage of slums is unexplained as most of the houses were gutted down to thrashes and ashes.

This is the second tragedy in east Africa for the past 2 days, as in earl hours of Saturday, a ferry carrying more than 800 passengers and overloaded with goods capsized in Zanzibar water, as she was heading to Pemba Island. The accident took away life of more than 200 people, most of them being women and children, and about 610 were rescued. 
 
The normal capacity of capsized ship was 645 passengers and 45 crews. 
 
In both tragedies, the respective Governments have promised to be responsible for treatment and burial ceremonies for deceased.

Sunday, 11 September 2011

Miss Tanzania 2011 ni Huyu Hapa

Shindano la kumpata mlimbwende atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya warembo duniani amepatikana mwanzoni mwa siku ya leo, yaani usiku wa manane pale Salha Israel kutokea Ilala (pichani chini, samahani kwa picha kutokuwa na muonekano mzuri.... si unajua tena!) kuwashinda warembo wengine 29.
Kwa ushindi huu, mrembo huyu amejipatia zawadi ya gari aina ya JEEP jipya lenye thamani ya TZS milioni 70 na kifuta jasho cha TZS milioni 8.
Pia ana zawadi kem kem ambazo zinafuatia ushindi huo.

 Wakati alipokuwa akijibu swali kabla kwenye kipindi cha maswali na majibu

Salha akiwa na washindi wa pili na tatu. 
  
Nashukuru kwa kuweza kunielewa, kwani hizi ni habari za chap chap, na picha nzuri bado hazijapatikana

Tuesday, 6 September 2011

Muwasho wa WikiLeaks ni wa Kuaibisha!

Jana, Kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, ililazimika kukana tuhuma zilizotolewa na mtandao wa WikiLeaks kuhusiana na taarifa iliyotolewa na aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Tz Bwana Michael Retzer na baadaye kunaswa na mtandao huu wa wikileaks. 
  
Inadaiwa ya kuwa wakati Mhesh Rais alipokuwa waziri wa mambo ya nchi za nje, aliwahi kupokea zawadi mbalimbali zikiwamo suti 4 na Chama chake kupewa dola za kimarekani milioni 1 ili kumsaidia katika kampeni za urais mwaka 2005. Na kama haitoshi, mtandao huo ulikuwa na habari zilizotumwa na aliyekuwa balozi huyo wa Marekani nchini Tz, ya kuwa aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Tz alilipiwa nauli kwenda London kwa ajili ya kwenda kupewa zawadi mbali mbali na mmiliki wa hoteli za Kempinski akiwa na matumaini ya kupewa haki ya kujenga hoteli  katika hifadhi za mbuga za wanyama za Ngorongoro na Serengeti. 
   
Jambo ambalo mimi binafsi ninajiuliza, ni kwa nini hili limepingwa haraka sana na kwa hisia za hasira. Angalau Rais wetu ana jukwaa la kumsemea, je na wale ambao hawana jukwaa la kuwasemea inakuwaje? 
 
Je, ni kweli hawa mabalozi huwa wanatuma taarifa za uzushi au ni kweli baadhi ya watu huwaambia taarifa nyeti, kama alivyofanya mkurugenzi wa Takukuru aliposema kuhusiana na wanaohusika na rushwa kubwa ambapo hata RA na EL walitajwa kuwa wamo!

Yote kwa yote, doa limeshapakwa, hata kama ni uwongo au ukweli, tayari Rais wetu na chama chake vimeaibishwa na kutiwa fedheha kubwa. 
 
Pata taarifa ya kukana kutoka Kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu hapa

Friday, 2 September 2011