Member of EVRS

Sunday, 11 September 2011

Miss Tanzania 2011 ni Huyu Hapa

Shindano la kumpata mlimbwende atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya warembo duniani amepatikana mwanzoni mwa siku ya leo, yaani usiku wa manane pale Salha Israel kutokea Ilala (pichani chini, samahani kwa picha kutokuwa na muonekano mzuri.... si unajua tena!) kuwashinda warembo wengine 29.
Kwa ushindi huu, mrembo huyu amejipatia zawadi ya gari aina ya JEEP jipya lenye thamani ya TZS milioni 70 na kifuta jasho cha TZS milioni 8.
Pia ana zawadi kem kem ambazo zinafuatia ushindi huo.

 Wakati alipokuwa akijibu swali kabla kwenye kipindi cha maswali na majibu

Salha akiwa na washindi wa pili na tatu. 
  
Nashukuru kwa kuweza kunielewa, kwani hizi ni habari za chap chap, na picha nzuri bado hazijapatikana

No comments: