Member of EVRS

Saturday, 24 September 2011

Chombo cha Utafiti wa Anga cha NASA Hakijulikani Kimeangukia Wapi

mchoro wa kuigiza wa chombo kinapolipuka moto mara kiingiapo katika anga ya Duni
Chombo cha angani (Satellite) kinachomilikiwa na NASA, ambacho kilikuwa anagani kwa zaidi ya miaka 20 kikifanya utafiti wa hali ya hewa, kwa sasa kinasemekana kimekwisha rejea duniani, inasemekana wamiliki wa chombo hicho (NASA) wanahisi kwa kiasi kikubwa kimekwisha anguka duniani, japo hawajui ni sehemu gani kimeangukia.  
   
Awali walitegemea kingeanguka katika bahari ya Pacific, lakini katika hali isiyokuwa ya kutarajiwa, kilipoingia kwenye anga ya dunia (Earth atmosphere) kilionekana kama kimepunguza kasi ya kuanguka, hivyo badala ya kutarajiwa kuanguka siku ya ijumaa, NASA ilikadiria kitaanguka jumamosi usiku au jumapili alfajiri. 
  
Chombo hicho chenye ukubwa kama wa basi kubwa, na kinachokadiriwa kuwa na uzito wa tani 6, mpaka sasa hakijulikani kilipo, na wala hakuna mtu aliyekwisha kutoa taarifa kama wameona mabaki yake. Na kwa kuwa mpaka sasa hivi NASA haijapokea taarifa yoyote ya majeruhi au madhara ya aina yoyote, wanaamini chombo hiki kimeanguka baharini, lakini hawajui ni sehemu gani.  

Bado wantafuta habari ya wapi mabaki ya chombo hiki yataonekana ili wawe na uhakika ya kuwa ni kweli kimekwisha anguka kwenye uso wa dunia. 
  
Pata habari zaidi hapa

5 comments:

Anya said...

Hi Chib

Yes it sounds vey scary
and
they predicted that it could collapse in Western Europe :(
Thats where I live !!have a nice sunday
:-)

emu-three said...

Oh juhudi yote ya miaka 2 !

alp said...

vaya foto,,,un abrazo..desde Murcia...

Amin said...

Anya or where I live...

nyahbingi worrior. said...

Habari za siku.
Kama mwanablogu kutoka Tanzania,nakuomba kushiriki kuchangia Mchakato wa KUFUFUA JUMUWATA(Jumuiya ya Wanablogu Tanzania).

Tafadhali naomba ufungue hii kurasa ya
http://blogutanzania.blogspot.com/
kisha upendekeze jinsi ya kufufua JUMUWATA.

Ahsante

Luiham Ringo.