Member of EVRS

Tuesday, 6 September 2011

Muwasho wa WikiLeaks ni wa Kuaibisha!

Jana, Kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, ililazimika kukana tuhuma zilizotolewa na mtandao wa WikiLeaks kuhusiana na taarifa iliyotolewa na aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Tz Bwana Michael Retzer na baadaye kunaswa na mtandao huu wa wikileaks. 
  
Inadaiwa ya kuwa wakati Mhesh Rais alipokuwa waziri wa mambo ya nchi za nje, aliwahi kupokea zawadi mbalimbali zikiwamo suti 4 na Chama chake kupewa dola za kimarekani milioni 1 ili kumsaidia katika kampeni za urais mwaka 2005. Na kama haitoshi, mtandao huo ulikuwa na habari zilizotumwa na aliyekuwa balozi huyo wa Marekani nchini Tz, ya kuwa aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Tz alilipiwa nauli kwenda London kwa ajili ya kwenda kupewa zawadi mbali mbali na mmiliki wa hoteli za Kempinski akiwa na matumaini ya kupewa haki ya kujenga hoteli  katika hifadhi za mbuga za wanyama za Ngorongoro na Serengeti. 
   
Jambo ambalo mimi binafsi ninajiuliza, ni kwa nini hili limepingwa haraka sana na kwa hisia za hasira. Angalau Rais wetu ana jukwaa la kumsemea, je na wale ambao hawana jukwaa la kuwasemea inakuwaje? 
 
Je, ni kweli hawa mabalozi huwa wanatuma taarifa za uzushi au ni kweli baadhi ya watu huwaambia taarifa nyeti, kama alivyofanya mkurugenzi wa Takukuru aliposema kuhusiana na wanaohusika na rushwa kubwa ambapo hata RA na EL walitajwa kuwa wamo!

Yote kwa yote, doa limeshapakwa, hata kama ni uwongo au ukweli, tayari Rais wetu na chama chake vimeaibishwa na kutiwa fedheha kubwa. 
 
Pata taarifa ya kukana kutoka Kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu hapa

1 comment:

Goodman Manyanya Phiri said...

Ukweli ni kwamba "penye moshi lazima moto upo". Hata Afrika Kusini hapa Wikileaks imeshatupatia mawazo kwamba eti "Raisi wetu ni kibaraka wake Obama" alietumwa kuyiangusha serekali yasasa huko Zimbabwe badala ya kusikiliza maamuzi ya SADEC.

Inaelekea utawala wa Mugabe umezifurahi habari hizo. Kicheko ni kwamba ilipogeuka Wikileaks na kusema Raisi Mugabe anaumwa ugonjwa wa PROSTATE, wakaanza kukana ile mbaya!

Mimi binafsi yote haya siyajali kama ni ukweli au uzushi. Bali najifunza kitu kimoja tu KAMPYUTA NDIE MTAWALA WA DUNIA SASA kwakuwa Wikileaks inatumia utaalam wa kikampyuta kueneza habari zake inaozipata kwa WHISTLEBLOWERS wake.