Member of EVRS

Friday, 28 January 2011

Tanzania: Matokeo Kidato cha Nne 2010 ni Aibu Tupu!

Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2010 kusema ukweli ni ya aibu tupu!
Kiwango cha kufaulu na kufeli vimekaribia kulingana, kwani si kitu cha kujivunia hata kidogo iwapo karibu nusu ya watahiniwa wanaambulia daraja ziro (division zero)

Kilichochangia zaidi ni kuanzisha shule kisiasa bila kuandaa waalimu wa kufundisha katika shule hizo. Ndio maana tumeshuhudia matokeo mabovu kabisa.

Hii ni changamoto kwa watu wote, na pia kwa wale watu ambao wamekubali shule zitumie majina yao, wana wajibu wa kuzisaidia shule hizo kupambana na matatizo wanayokutana nayo.

Ifuatayo, ni baadhi ya mifano ya shule zilizochemsha kama nilivyonukuu kutoka kwenye tovuti ya baraza la mitihani kwa matokeo ya kidato cha nne 2010:

Shule        Daraja 1 - 2 - 3  -  4  - 0  
  
Anna Mkapa                      0 - 3 - 11 - 69 - 109 
Karamagi                           0 - 0 - 0 - 11 -
Celina Kombani               0 - 0 - 1 - 21 - 44 
Mary Nagu                        0 - 0 - 0 - 18 - 36 
Felix Mrema                     0 - 0 - 4 - 38 - 118 
Prof Philemon Sarungi    0 - 0 - 0 - 19 - 52 
Balozi Mshangama          0 - 0 - 0 - 8 - 33 
Kabwe                              0 - 0 - 1 - 18 - 23 
J. M. Kikwete                  0 - 4 - 2 - 29 - 52 
Mwanamwema Shein      0 - 0 - 4 - 27 - 66 
Salma Kikwete                3 - 8 - 27 - 119 - 150 
Mwapachu                       0 - 0 - 1 - 27 - 171 
Monica Mbega                0 - 0 - 0 - 3 - 31 
Nyamoko                         0 - 0 - 2 - 51 - 52 
Chokocho                        0 - 0 - 0 - 13 - 42 
Ukonda Moyo                 0 - 0 - 1 - 9 - 31 
Mswaki                            0 - 0 - 2 - 10 - 27 
Kilamacho                       0 - 0 - 2 - 35 - 89 
Mabwerebwere                0 - 1 - 1 - 7 - 56 
Ukata                               0 - 0 - 0 - 9 - 54 
Mtumba                           0 - 1 - 0 - 18 - 60 
Shume                             0 - 0 - 5 - 39 - 102 
Dindira                            0 - 0 - 0 - 21 - 84 
Mwisho wa Shamba       0 - 0 - 0 - 28 - 97 
Zuzu                               0 - 0 - 0 - 3 - 19 

Napenda kuishia hapa, kwani orodha ni ndefu, na inaweza kukufanya ukapata ugonjwa wa moyo!

Wednesday, 26 January 2011

Wimbi la Kuondoa Marais Waliokaa Muda Mrefu Afrika

Kumekuwa na wimbi jipya la kung'oa utawala wa kiarabu uliodumu kwa muda mrefu. 
  
Lilianzia Tunisia, na tukashuhudia rais wa nchi hiyo akikimbilia Saudia kujificha mara baada ya kuzidiwa na "hoja ya nguvu".  
    
Upepo ukavuma mpaka huko Yemen na baadaye kuhamia Misri ambako unaelekea kupamba moto.  
Raia wa Misri wamemkamia rais wao Hosni Mubarak ambaye ameiongoza nchi hiyo kuanzia tarehe 14 oktoba 1981 hadi leo hii  kuondoka madarakani.
Kabla ya hapo Mubarak alikuwa makamu wa rais kwenye uongozi wa Anwar El-Sadat kuanzia tarehe 16 Aprili 1975 hadi oktoba 1981 ambapo rais wa Misri aliyekuwapo kuuawa kwenye gwaride.  
  
Mubarak ni mmoja wa viongozi wa nchi za kiafrika aliyedumu kwa muda mrefu sana, kwani inazidi miaka 29 tangu aingie madarakani wakati huo akiwa na nguvu, lakini kwa sasa uzee unamnyemelea, ukizingatia ya kuwa alizaliwa tarehe 4 Mei 1928.

Kwa sasa kumekuwa na maandamano makubwa yakimtaka aachie ngazi kiasi cha kusababisha mauaji ya watu kadhaa. 
 
Inafikia wakati, wale viongozi waliokaa muda mrefu madarakani kama Mugabe, Gadhaffi, Al-Bashir, Museveni, Dos Santos na wengine kuachia ngazi na kuacha watu wengine waongoze.

Nina imani kukaa muda mrefu madarakani hakuongezi tija, bali humfanya mtu atawale kwa mazoea na kujisahau.

Monday, 24 January 2011

Kila Mtu na Kazi Yake

Hakuna kuchekana jamani.
Pale unapoona ya kuwa kazi yako ni hovyo na ya kuchosha sana.... Labda inawezakuwa sio kweli.  
 
Unaweza kuwa kati ya watu waliobahatika kupata kazi nzuri. 
 
Ukijaribu kufanya utafiti kwa watu wanaong'ang'ania kubaki kwenye nafasi ya urais wa nchi kama ni kweli wanaifurahia sana kazi yao, nahisi wengi watakuambia ni kazi ya utumwa, isiyo na uhuru wa kweli na kuishi kwa wasiwasi muda wote. Lakini utashangaa watu wanagombea na kujenga uadui na wapinzani au washindani wao ili kupata nafasi hiyo hiyo ya urais!!!.  
 
Basi, nami nimeamua kuipenda kazi yangu, japo watu wakiniangalia hapo juu watafikiri naunda bomu la nyukilia ilhali nipo kazini natengenea kiungo muhimu cha binadamu ili arudie tena kama alivyokuwa zamani.
Hapo nilikuwa nyumbani Bongo wakati wa "likizo"

Friday, 21 January 2011

Weekend wishes To You!


I just wanna say... Have a lovely weekend.  
   
Huku nikiwa nasubiri kwa hamu kubwa mazao yangu yakomae hapa kibandani kwangu ili nipate japo ya kuchoma na kufaidi jasho la mikono yangu!! 
 
Be blessed

Tuesday, 18 January 2011

Tanzania Yageuka Shamba la Bibi

Sina mengi ya kusema... Lakini bado nipo kwenye mshangao kwa jinsi ninavyo ona Tanzania inavyochumwa na kila mtu mwenye nafasi yake tena kuchuma usichopanda, na kuwanyima wenye njaa ambao ndio mali yao.

Wakati bado tupo kwenye kelel za kwa nini Tanzania iilipe kampuni ya kitapeli ya Dowans mabilioni ya pesa ambayo serikali yetu tukutu iliamua kupunguza kwa kuwahadaa watanzania kuwa ni tubilioni tisini na badala ya mamia... Sasa kuna uzushi mwingine kuwa Tanzania inatakiwa kuwalipa .... hawa kampuni kutoka India iliyoingia ubia na serikali wa kuendesha reli ya kati kiasi cha shilingi bilioni 21 kwa kuvunja mkataba tata ambao kampuni ya India ilishindwa kabisa kuendesha reli ya kati.

Najua watu wakipiga kelele utasikia tunatakiwa kulipa bilioni 12 tu, kama vile hayo mabilioni ni vijisenti tu!!

Sijasikia hata mara moja hiyo inayojiita serikali kusema ni hatua gani itawachukulia walio sababisha hasara na kututaka tulipe mabilioni ya fidia kwa kutokuwa na huduma ya aina yoyote!!

Kwa sasa nimeanza kuwa na wasiwasi haya mabilioni hayalipwi kwa kampuni yoyote ya nje, bali yanaenda kwa watanzania hao hao ambao ni makuwadi wakubwa wa ufisadi, na ndio maana kuna kuwa kama kuna haraka vile ya kutaka kulipa kabla ya bunge kuanza.

Hivi tumefumba macho au tumekaangwa akili.
Hakika mganga huyu ni mkali sana, sasa tusemeje, maana tumelala na lazima tutafute visingizio kama vile kilichotokea ni bahati mbaya.  
  
Hata wezi wa EPA waliambiwa warudishe taratibu tu, hawatachukuliwa hatua, na hakuna anayejua ni kiasi gani kilisha rejeshwa iwapo ni kweli.  
  
Wale watuhumiwa wa ujambazi kama akina AM walishikwa na baadaye wakaachiwa kwa kuambiwa ati wasifanye matukio ya uhalifu kwa angalau miaka miwili.   
 
Vinara wa madawa ya kulevya, orodha iliandaliwa, mwendesha mashtaka akatamka kuwa orodha inatisha, kuna jamaa fulani alikabidhiwa naye kaimeza kimyaaa, sijui anasubiri wikileaks tena!!!!!   

Shule zetu, watoto wanakaa kwenye vigunia, hospitali hakuna dawa wala wataalamu, maji hakuna, umeme sina la kusema, maana kuna jamaa yangu alisema ati Tanesco ni kampuni pekee duniani iliyoweza kufanikisha kupandisha gharama za kuuza umeme kwa kuongeza muda wa kuwaweka watu gizani badala ya kuwapa umeme!!!  
     
Hivi hawa watanzania siku wakifumuka, patatosha????  
   
Shamba la Bibi linavunwa tuuu, hivi haliishi hilo?

Monday, 17 January 2011

Twin Baby Boys Laughing at Each OtherDid you had a lovely weekend?

If not, then Have a blessed and laughing monday!!

Thursday, 13 January 2011

Which One is a Fake Product!!

Someone alerted me that one of these Santa Lucia spaghetti is a fake product!!

I am not sure which one, can you spot or suggest from this appearances.
Just look this below too......
NB. For below photos, On left is 450g and right is 500 gr which is opposite from the above photo

Tuesday, 11 January 2011

Kuuliza sio Werevu!

Nahisi nilikuwa nimepotea au.....  
Happy New Yeaaaaaaaar 2011, sasa sijui ni kufurahi au kuandika maumivu!!
  
Baada ya kupigwa na baridi sana....then jooooto....Nina swali la kizushi.....
Hivi Uchumi wa Tanzania unaposemwa kwamba unakuwa ..... yaani wana maana gani, yaani kwenda kwenye hasi au chanya? 
 
Au ni kimtizamo tu kwa upande mmoja wa sarafu?