Member of EVRS

Wednesday 26 January 2011

Wimbi la Kuondoa Marais Waliokaa Muda Mrefu Afrika

Kumekuwa na wimbi jipya la kung'oa utawala wa kiarabu uliodumu kwa muda mrefu. 
  
Lilianzia Tunisia, na tukashuhudia rais wa nchi hiyo akikimbilia Saudia kujificha mara baada ya kuzidiwa na "hoja ya nguvu".  
    
Upepo ukavuma mpaka huko Yemen na baadaye kuhamia Misri ambako unaelekea kupamba moto.  
Raia wa Misri wamemkamia rais wao Hosni Mubarak ambaye ameiongoza nchi hiyo kuanzia tarehe 14 oktoba 1981 hadi leo hii  kuondoka madarakani.
Kabla ya hapo Mubarak alikuwa makamu wa rais kwenye uongozi wa Anwar El-Sadat kuanzia tarehe 16 Aprili 1975 hadi oktoba 1981 ambapo rais wa Misri aliyekuwapo kuuawa kwenye gwaride.  
  
Mubarak ni mmoja wa viongozi wa nchi za kiafrika aliyedumu kwa muda mrefu sana, kwani inazidi miaka 29 tangu aingie madarakani wakati huo akiwa na nguvu, lakini kwa sasa uzee unamnyemelea, ukizingatia ya kuwa alizaliwa tarehe 4 Mei 1928.

Kwa sasa kumekuwa na maandamano makubwa yakimtaka aachie ngazi kiasi cha kusababisha mauaji ya watu kadhaa. 
 
Inafikia wakati, wale viongozi waliokaa muda mrefu madarakani kama Mugabe, Gadhaffi, Al-Bashir, Museveni, Dos Santos na wengine kuachia ngazi na kuacha watu wengine waongoze.

Nina imani kukaa muda mrefu madarakani hakuongezi tija, bali humfanya mtu atawale kwa mazoea na kujisahau.

2 comments:

Simon Kitururu said...

Nahisi kuna viongozi UONGOZI hugeuka kuwa ndio identity yao na wanaogopa kutoka kwakuwa wakiacha kuitwa VIONGOZI inakuwa ndio basi tena hata umuhimu wa maisha yao hupotea.


Tatizo hili naliona sana hata kwa waachishwao kazi ghafla ambao hawaachi kuondoka majumbani mwao asubuhi na kujifanya wameenda ofisini au hata wale wafikiao KURITAYA ambao unakuta nyumbani hapakaliki kwa kuwa hawajui hata nini wafanye nyumbani.


NI mtazamo tu!

emu-three said...

Lakini kazi kama uraisi, utakuwaje hujui nini la kufanya nyumbani, nafikiri hata akistaafu bado marupurupu yatakuwawepo...labda wenzangu na sie ambao ukistaafu ujue unakwenda kujifia, maana huna akiba, huna kigango wala dungu...utakuwa nalo vipi wakati mshahara ulikuwa `haujai kiganja...mmmh
Mabadiliko ni lazima, na vuguvugu hili, kama viongozi wenye busara watalielewa ni heri waache ngazi mapema, wkani sasa `uongozi utakuwa kiti cha moto'