Member of EVRS

Monday, 24 January 2011

Kila Mtu na Kazi Yake

Hakuna kuchekana jamani.
Pale unapoona ya kuwa kazi yako ni hovyo na ya kuchosha sana.... Labda inawezakuwa sio kweli.  
 
Unaweza kuwa kati ya watu waliobahatika kupata kazi nzuri. 
 
Ukijaribu kufanya utafiti kwa watu wanaong'ang'ania kubaki kwenye nafasi ya urais wa nchi kama ni kweli wanaifurahia sana kazi yao, nahisi wengi watakuambia ni kazi ya utumwa, isiyo na uhuru wa kweli na kuishi kwa wasiwasi muda wote. Lakini utashangaa watu wanagombea na kujenga uadui na wapinzani au washindani wao ili kupata nafasi hiyo hiyo ya urais!!!.  
 
Basi, nami nimeamua kuipenda kazi yangu, japo watu wakiniangalia hapo juu watafikiri naunda bomu la nyukilia ilhali nipo kazini natengenea kiungo muhimu cha binadamu ili arudie tena kama alivyokuwa zamani.
Hapo nilikuwa nyumbani Bongo wakati wa "likizo"

10 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kwanza tuwe na furaha kuwa na kazi maana wapo wengi pia wanaitafuta kazi hiyo hiyo ambayo wewe/mimi tunasema inachosha. Na kazi uliyonayo kaka Chib ni muhimu kwani bila wewe kuipenda kazi yako basi wengi wangekuwa hawana maana. TUZIPENDE KAZI ZETU...PAMOJA DAIMA

emu-three said...

Hongera mkuu, nyie ndio watu muhimu sana katika maisha yetu, kama ningeliambiwa watu gani wawe wanapewa mishahara mikubwa sana, mimi ningewataja nyie na walimu...!

chib said...

Swadakta emu-three

EVARIST said...

Hongera sana mkuu

chib said...

Shukran Evarist!

SIMON KITURURU said...

DUH!


FASHENI zenu kimavazi na MAPADRE zinatisha Mkuu!:-)

Bwaya said...

Hongera sana daktari.

Upepo Mwanana said...

I see, sasa nimeelewa...
Nyumba hiyo inatisha, hakuna tofauti na wana anga wa mbali!

Koero Mkundi said...

Sikujua kama wewe ni Tabibu.....
Nakutakia kila la kweri kaka katika kazi yako hiyo ya kuokoa roho za watu na kuahirisha vifo vyao.....LOL

chib said...

Upepo- Hakuna cha kutisha, kama unaweza kupanda ndege na kumuamini rubani, basi yote ni kama sisi
Koero- Ni njia ya kubangaiza tu na kutuwezesha kuishi mjini!