Member of EVRS

Friday, 16 September 2011

Hatimaye! Tanzania yapata medali yake Mashindano ya Afrika

Timu ya taifa ya mpira wa pete, Taifa Queens, hapo juzi iliipatia medali Tanzania kutoka katika mashindano ya Afrika, baada ya kuifunga timu ya akina dada wa Botswana kwa 43 - 35 na hivyo kuchukua medali ya fedha katika mashindano hayo.
Waliochukua medali ya dhahabu ni Uganda, na ya shaba ni Zambia.

Timu ya Tanzania, ilipoteza michezo 2 kati ya 8 iliyocheza, na ilifungwa na timu za Uganda 52-41 na Zambia 46-42 pekee, ambazo zote hizi ndio zilizofanikiwa kutwaa medali katika mchezo huu.

Hata hivyo Tanzania waliwazidi Zambia kwa idadi ya magoli, kwani walikuwa waanalingana kwa alama.

Michezo waliyocheza:

Waliwafunga
Kenya 36 - 35
Ghana 94 - 24
Mozambique 92 - 8
Zimbabwe 38 - 27
South Africa 32 - 29
Botswana 43 - 35

Tunaipongeza timu ya Taifa Queens kwa kutuondolea fedheha ya muda mrefu.

Picha kutoka Star Africa

3 comments:

emuthree said...

Twawapa pongezi sana

Ivo Serenthà said...

The sport has always united the peoples, long live the sport.

Good new week

Simon Kitururu said...

Tanzania oyeee!
Hongereni jamani ! Huwa inatia moyo kweli angalau mara moja moja tukisikia vitu CHANYA kuhusu TZ aka Bongo Nyoso!

Vitu HASi kwenye vyombo vya habari ni kiburungutu yani!:-(