Member of EVRS

Thursday, 4 November 2010

Rwandair !!!

Hivi utasijiakiaje pale shirika la ndege linapokupatia tiketi ambayo unalazimika kutumia ndege nyingine kabla ya kuunganisha na ndege yao. Halafu tarehe ya ndege yao, wanakupa siku na saa ambayo hawana safari ya kwenda huko uendako.

Shirika jingine wanapokueleza ya kuwa connection yako haiwezekani, kwani shirika waliokupa tiketi hiyo,   hawana safari muda huo!!    
Unapowarudia ofisini kwao na kuwaambia wakupe ratiba ya safari zao, wanakuambia hapo customer care, kuwa hawana ratiba ofisini, na wakati huo huo wana mtandao wanaotumia kufanya booking!! Yaani hawatanii, ndio wanakwambia ukweli.... 
  
Ukiwa bado umeduwaa, wanakuja abiria wengine wawili, tayari wametahayari na kulalalama, ya kuwa walipofika uwanja wa ndege siku 3 zilizopita, waliambiwa safari ya ndege yao imefutwa, na hivyo wakaambiwa waje leo saa 4 asubuhi, kwani ndege itaondoka saa 8 mchana. Na wakawaandikia kwenye tiketi KABISA kwa elektroniki. Alipofika saa 4 asubuhi wakafika kwa bashasha, ndio wakakuta ndege inakaribia kugusa mawingu, yaani ilipaa kama dakika 1 hivi tangu wafike. Huwezi kuamini safari zote hizo ni za kimataifa.  
  
Mimi ambaye nilikuwa nasubiri kukata tiketi, nayo ya safari ya kimataifa nikabaki mdomo wazi. Mwisho wa yote, nilipomaliza kulipa, nikapewa karatasi yangu niliyokuwa nimewapa ya maelezo yote ya abiria, na wao walikuwa wameandika kwa mkono nyuma ya maelezo yangu wakiwa wameweka na namba ya elektroniki ya tiketi yangu, wakadai printer haifanyi kazi, kwa hiyo nije uwanjani na kikaratasi hicho!!!!!!!!!!  
  
Nikaomba nitumiwe kwa barua pepe, maana niliona hicho ni kiini macho.....sasa saa 8 zimekwisha pita, bado sijapokea barua pepe yoyote, na namba za simu zetu wanazo!!!

Upo hapo, kumbe sio Bongo tu kwenye mitkas viza ..............

5 comments:

EDNA said...

Inakera kweli,Kaka CHIB ungewachapa vibao washike adabu zao.

emu-three said...

Sio bongo tu, hili ni swala la `nchi za kimasikini' umasikini unapokithiri, utendaji unapungua! Pole sana, najiuliza hata ndege mnapigwa kalenda, je mkiwa hewani mara mnasikia uwanja wa kutua hauna nafasi, saa mliyopangiwa kutua imeshikwa na mtu mwingine!

SIMON KITURURU said...

Afrika yetu mambo yake yanavyoendeshwa ajuaye ni MUNGU tu !Kuna wakati hata kujitetea mtu unapata taabu ikitokea unapigwa maswali fulani ya jinsi ya maswala yanavyoendeshwa na hapa sizungumzii Air Tanzania wal Air Rwanda tu.:-(

Hivi kwanza katika ratiba Tanzania tulitakiwa tutangaziwe Rais lini vile?

chib said...

@ Edna, ni kweli inakera, maana leo nilipoenda, nikakuta hata jina nililowaandikia wamelikosea!!!!!

@ Emu 3, hayo yalinikuta London(Heathrow), tulizunguka hewani kama dk 45 tunasubiri kutua, sababu uwanja ulikuwa busy na ndege zituazo na kuondoka, na sio kushikiliwa na ka-fisadi :-), saa ya kuondoka tulisubiri kwa dk 50 ndio tukapewa go ahead

@ Simon.... :-)

Upepo Mwanana said...

Ndio maana mashirika yetu hayaendelei!