Member of EVRS

Thursday, 14 April 2011

Anne Makinda: Bado Kanuni za Bunge Zinamkanganya

Kwa wale wanaofuatilia mijadala ya Binge la Tanzania kwenye runinga moja kwa moja, watakubaliana nami ya kuwa Bunge la sasa la Tanzania linaelekea kuyumba na kuendeshwa ndivyo sivyo. 
   
Chanzo kilichopo ni pamoja na Spika Anne Makinda kutokufahamu vizuri baadhi ya kanuni za uendeshaji wa Bunge la Tanzania, na wakati mwingine kuendesha mambo kwa "mazoea". 
Katika kikao cha Bunge kilichopita, kuna siku alikiri ya kuwa kuna baadhi ya kanuni hakuwa anazijua, hadi wabunge walipokuwa wananukuu vifungu fulani fulani, akajikuta kuwa naye alikuwa havijui.
Hayo ni matunda ya kuendesha Bunge kwa mazoea, ndio maana hata na yeye baada ya kukaa bungeni kwa zaidi ya miaka 30, bado hajui baadhi ya kanuni, achilia mbali ya kuwa alishawahi kuwa naibu spika! 
  
Jana wakati wa kikao cha Bunge aling'aka pale mbunge mmoja alipotaka mwongozo wa uteuzi wa wenyeviti wa Bunge, baada ya Bunge kukiuka uteuzi wa wagombea.
Mwishoni Spika ilibidi akubali kutengua kanuni hiyo iliyokiukwa ili wenyeviti hao waweze kuteuliwa na kufanya kazi baada ya kuonekana upungufu/ uvunjaji wa kanuni ya Bunge.

Pia kulikuwa na vurugu nyingine
Nisikumalizie uhondo, ingia hapa kwa Subi upate video ya vurugu Bungeni. Utabofya kwenye link aliyo onyesha, nina hakika utabaki mdomo wazi!!!

3 comments:

Malkiory Matiya said...

Huyu mama yatakuja kumshinda asipojirekebisha, kila kukicha lazima mzozo kwenye vikao vya bunge. Hizi ni dalili za wazi kuwa anashindwa kuimudu kazi yake vema.

chib said...

Kweli kabisa Malkiory. Hii ni Dalili mbaya, halafu amekuwa akitumia jazba, anashindwa kutofautisha ukali na jazba!

Goodman Manyanya Phiri said...

Hajui kanuni? Kisingizio tu!

Njoo Afrika Kusini uone vichekesho vinaosababishwa na SPEAKER. Mara wabunge kufukuzwa; mara mbunge kuambiwa aombe msamaha.

Ukichunguza kwa undani, sababu ni kwamba mbunge mhusika ni wachama cha upinzani!