Member of EVRS

Friday 1 April 2011

Dawa za "Vikombe" Si Lolote si Chochote

Wimbi la dawa za "vikombe" inasemekana si lolote si chochote, bali ni njia mojawapo za kujikwamua kimaisha na kukabiliana na ukata uliopo kwa sasa Bongo.

Watu werevu wametumia mbinu ya matatizo ya wananchi na ukomo wa fikra zao, na kutumia njia hiyo kuwahadaa ya kuwa wanatibu magonjwa sugu ambayo madaktari wamesema hayatibiki hadi kupona kabisa. 
  
Maneno haya yamebainishwa na mchungaji mstaafu wa Loliondo, na ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kwa kuacha kunywa dawa zao za hospitali baada ya "vikombe", amekuwa akisisitiza waendelee kunywa dawa zao hata baada ya "vikombe" 
  
Itakumbukwa ya kuwa siku zote huwa anawaambia wateja wake ya kuwa, kupona kwao ni kwa imani, na kama huna imani, basi hautapona.
Hii ni kama vile watu wanavyo amini ya kuwa Mungu yupo, japo hawajawahi kumuona wala kusikia sauti yake achana na harufu yake tu. Lakini watu kwa imani yao, inapotokea mtu akamkashifu huyo Mungu ambaye hawajamuona na wanayemuamini, kunaweza kukatokea vita na maangamizi! 
  
Tahadhari: Leo ni siku ya wajinga!

1 comment:

Rachel Siwa said...

Taifa lina teketea kwa mambo ya mazingaombwe,hakuna cha kikombe wala nini ujanja mpya tuu umezuka!Mwisho wake ni mbaya sana tena ni aibu kwa Taifa kuungana na kiini macho.