Member of EVRS

Monday, 11 April 2011

Mukama ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Mpya wa CCM

Hatimaye jina la mrithi wa Yusuph Makamba kama katibu mkuu wa CCM limetangazwa na mwenyekiti wa CCM, naye si mwingine bali ni Wilson Mukama (Pichani juu)
Jina lake limepitishwa na Kikao cha halmashauri kuu ya CCM huko Dodoma, na muda mfupi uliopita ndio jina hili likatangazwa rasmi.   
   
Naibu wake kwa upande wa Bara ni John Chiligati na kwa upande wa Visiwani ni Ali Vuai Ali.

5 comments:

Malkiory Matiya said...

January Makamba na Mnauye ndani ya nyumba! CCM kazi ni kulipa fadhali na kurithishana madaraka kifamilia, kutoka kwa baba kwenda kwa mwana. Utawala wa kifalme.

chib said...

Ni hapo sasa!

Malkiory Matiya said...

Rekebisho: fadhila na siyo fadhali!

Anya said...

Congratulations to Mukama :-)

emu-three said...

Heko chama chetu, CCM chama chetu, uendeleze juhudi chama zilifanywa na wazazi wako, ...wimbo huu naukumbuka, kipindi CCM, NI CCM KWELI, USIPOKUWA NA KADI HUPATII SHULE! unga sukari, mkate kwa mgawo...tumetoka mbali