Member of EVRS

Wednesday 30 March 2011

Sherehe za Kumuaga Josephine Ulimwengu - Rwanda

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Umoja wa Watanzania wanaoishi Rwanda - UTARWA - Ulifanya sherehe fupi ya kumuaga aliyekuwa mwenyekiti wa umoja huo Mama Josephine Marealle- Ulimwengu ambaye amepata kazi mpya ambayo inashughulikia masuala ya watoto kwa nchi sita zilizo katika ukanda wa Afrika ya Kati.
Ofisi yake itakuwa Addis Ababa, Ethiopia.
Kabla ya kupata kazi hiyo mpya, Josephine alikuwa mwakilishi mkazi wa shirika la CARE International kwa hapa Rwanda.

Katika mambo aliyowaasa watanzania wanaoishi Rwanda, aliwasihi kujituma, kufanya kazi kwa malengo ya kujiendeleza kitaaluma na kiutendaji na pia kusisitiza kukumbuka na kufanya shughuli za maendeleo nyumbani Tanzania.
Na mwisho alisisitiza, ya kuwa wasiwe waoga kufanya maamuzi ambayo wanahisi yatawaletea maendeleo kimaisha na kiutendaji.

Mwisho wa kauli mbali mbali za viongozi wa UTARWA akiwepo pia balozi wetu nchini Rwanda, Watanzania waliburudika kwa vyakula, vinywaji na muziki mwororo wa nyumbani ukichagizwa na utani wa makabila mbalimbali ya Tanzania.

Pata habari picha hapo chini!



Mwenyekiti Mpya wa UTARWA Bw,. Thambikeni akisoma risala kwa niaba ya wana-UTARWA

Mlezi wa UTARWA Mhesh. Balozi wa Tanzania nchini Rwanda akitoa wosia

Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Mama Josephine Ulimwengu akipokea zawadi ya UTARWA kutoka kwa Balozi Dk Matiko

Josephine akiifurahia kwa moyo wote zawadi aliyopewa

Kauli ya kuwaasa wana UTARWA


Wana UTARWA wanabadilishana hili na lile huku wakisubiri "Ndafu"

2 comments:

malkiory said...

Tutaufanyia kazi ushauri wake juu ya watu kujiendeleza. Hongera Josephine, tuwakilishe vema huko kwa Wahabeshi.

Simon Kitururu said...

Mbona sioni MSOSI? Unajua tena siye Wabongo kwa kubania bajeti kwenye sherehe za watu!:-(