Member of EVRS

Monday, 21 March 2011

Healing by Believing: Kupona kwa Imani

Makala hii aliyoitoa Subi kwenye WAVUTI imenivutia sana.

Hii inatokana na wananchi wa kawaida, viongozi wa kiserikali na kidini, matajiri na raia wa kigeni waliokulia kwenye dawa zilizohakikiwa, kusahau yote na kwenda Loliondo kwa Babu kupata kikombe cha dawa ya aina moja ambayo inatibu maradhi ya aina yoyote. 
  
Na pia dawa hii imeleta chuki kwa baadhi ya watu wanaojiita ni mitume wa Mungu au Manabii na kufikia hata kumlaani Babu wa Loliondo kwa kumuhusisha na wale wahubiri wa uongo walioandikwa katika Biblia takatifu, lakini baadaye ilikuja kugundulika ya kuwa hao manabii na wahubiri wa neno la uzima wameanza kupoteza waumini katika makanisa yao, na kuna uwezekano mkubwa ndio sababu ya wao kumpigia kelele Babu wa Loliondo!

Kutokana na wimbi kubwa la watu kukimbilia kwa Babu, serikali ya mkoa wa Arusha imelazimika kutoa vibali vya usafirishaji vya muda kwa baadhi ya magari, ili kuwezesha kupungua kwa nauli inayotozwa kwa sasa kwa wagonjwa kuelekea Loliondo.

Bofya hapa kwa Subi upate habari picha.

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwa hiyo hapa inamaana hii imani imekuja sasa tu?

Malkiory Matiya said...

Mimi raha yangu ni kuona baba na wananchi wa eneo lile wanafaidika kiuchumi. Babu angeishi kwenye umasini hadi lini! sasa hivi anatafuna hata vijisenti vya mafisadi.

emu-three said...

Kweli mkuu kufa-kufaana, unajua riziki hutolewa na mungu, hili linajionyesha hapa, lini huyu mzee angelipata hela ya waziri au nani vile?....lao anafikiwa na watu ambao kama angeliondoka siku moja kuwatembelea angeswekwa ndani...ajabu kabisa hii! Miujuza ya yule tusiyemwamini lakini yupo na ataendeela kuwepo! Hafi, hafanani na chochote unachokiwaza, ...!

Anya said...

Thank you very much
for your birthday wishes :-)

Hugs from us all
:))