Member of EVRS

Tuesday, 29 March 2011

Sababu ya Watu Wengi Kuwahi Kwa Babu wa Loliondo

Kama inavyojulikana... watu wengi wanaenda kijiji cha Samunge kwa "Babu" pichani hapo juu, kupata tiba mbadala ya magonjwa sugu na yasiyotibika katika hospitali za kawaida.  
  
Mbali ya sababu hiyo kuu, kuna baadhi ya watu, labda wengi wanataka kuwahi hasa kwa kuzingatia umri wa Mchungaji mstaafu Ambilikile au maarufu kama "Babu". Kwani watu wengine wamekuwa na wasiwasi ya kuwa ni mzee sana, na kazi anayofanya sasa kuanzia asubuhi hadi usiku inamchosha sana. Hivyo, wamekuwa na wasiwasi labda siku zake za kuishi duniani zipo ukingoni, na hivyo wanataka kumuwahi kabla hajaitwa kwenye hukumu ya haki na ya mwisho!!!!! 
 
Nimekwisha pata habari kwa watu watatu walionithibitishia nia yao ya kuwahi huko Loliondo kuwa sababu nyingine ya muhimu kwa wao kwenda mapema ni huo umri wa Babu!!.
  
Hapa Rwanda, kuna watu wanajiandaa kukodi gari hadi kwa Babu huko Loliondo. 
 
Picha kutoka Bongocelebrity

4 comments:

emu-three said...

Aisee...! Mkuu tupo pamoja, nimetingwa kidogo, lakini siachi kukutembelea

Anya said...

He is looking not happy :(

Swahili na Waswahili said...

Maisha ni gharama sana!!!kuna wanowahi kabla ya Babu kufa wawe ameshatibiwa,lakini wanaweza kutangulia wao kwa sababu nyingi tuu!!.

leo nimepita hapa kukumbuka siku nyingi sana tulikuwa tunakutana kuleeeeeeee kwa BABU!!!!!!

ohhhh si Loliondo ni Fotobalaza!!.

NN Mhango said...

Mambo yameziku kuzua mambo! Mbeya na Tabora nako kuna kaka na dada. Bado mama. Uzuri au tuseme ubaya wa watanzania ni mabingwa wa kuigiza. Kila mkoa hata wilaya utastukia kuna mtoa kikombe na baada ya watu kugutuka wote wanatokomea walikoibukia.