Member of EVRS

Wednesday, 23 March 2011

Rais wa Guatemala kumtaliki mkewe Sababu ya Mkewe Kutaka Urais!

Siasa.... kweli ni mchezo usio na maadili wala staha.  
  
Rais wa sasa wa Guatemala anayemaliza muda wake, Alvaro Colom, anatarajiwa kumpa talaka mkewe Sandra Torres de Colom kwa kile kinachodaiwa ya kuwa mkewe anataka kumrithi kiti cha urais.  
  
Mchakato wa kutengua ndoa hiyo umekwisha anza kwenye mahakama ya Guatemala na utachukua kama mwezi mmoja kukamilika.  
  
Katiba ya Guatemala, hairuhusu mtu yeyote aliye karibu kiundugu au ki-uwenza na rais aliyepo madarakani kugombea kiti cha urais baada ya muda wa rais aliyepo madarakani kumalizika kikatiba. 

Guatemala itafanya uchaguzi wake mwezi septemba mwaka huu.

Habari zaid kwa kiingereza, soma hapa

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kupeana TALAKA kwababu ya siasa mweh! hii sasa kali kwelikweli....

Malkiory Matiya said...

Watu kwa madili, kwahiyo asiposhinda! ndiyo imetoka. Hawa wamepanga dili la ulaji tu wala si lolote. Ingekuwa Tanzania rais bila mume ingekuwaje!

Fadhy Mtanga said...

kaaaaazi kweli kweli. Ina maana kuwa hawapeani talaka kwa kushindwana bali kusaidiana ili kushinda urais. Kwa maana hiyo mapennzi yapo pale pale.

Kweli dunia ina mambo!

chib said...

Hawa walikuwa na mkataba tu, maana wameishi kwenye ndoa miaka 8 tu baada ya kukutana miezi 6 kabla.
@ Malkiory, na mimi ndio nilikuwa najiuliza, akishindwa ndio inakuwaje, au akishinda, atakuwa na gari dogo aka nyumba ndogo ya aliyekuwa rais?!!