Member of EVRS

Tuesday, 15 March 2011

Kona ya Siasa: CCM Waanza Kudonoana

Katika kile kinachoonekana fukuto la moto ndani ya chama tawala cha Tanzania (CCM), kumeanza kutokea shutuma za kulaumiana ndani ya chama hicho.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, mkutano wa UVCCM ambao ulifanyika  Kibaha, mkoa wa Pwani, ulihitimisha kikao chao kwa kutoa kauli kali kwa mawaziri wakuu waliopita, mmoja akiwa kamaliza muda wake wakati wa awamu ya tatu, na mwingine muda wake ulichakachuliwa mapema na kulazimika kujiuzulu. 
  
Shutuma zililengwa kwao ati kwa sababu waliishauri ama serikali au Chama Chao kuhusu masuala ya nchi na wanachi au kurekebisha mfumo wa utendaji na kujibu hoja za baadhi ya wapinzani kupitia kwenye vyombo vya habari badala ya kutoa ushauri kwenye vikao vya Chama hicho au kumshauri mwenyekiti wao kwa faragha!  
   
Vijana hao walidiriki kumshauri ati mwenyekiti wao awatose hao mawaziri wakuu wastaafu ambao ni wajumbe wa Halmashauri kuu ya chama hicho ili kukinusuru chama hicho, kwani wastaafu hao wana nia ya kuwania urais 2015 kwa staili ya kukichafua chama au mwenyekiti wao......
Si hapo tu, tumesikia pia kuna baadhi ya mawaziri wamezuiliwa kuendelea na utendaji wa kazi zao kwa kuzingatia sheria, ati kwa sababu kasi yao ni kubwa mno na inahatarisha amani! 
  
Mimi binafsi sioni tatizo lolote kwa mtu kusema ukweli kutokana na hali halisi, sipendi kuwasemea chochote hao wanaotishiwa kutoswa, kwani wanasema msema kweli ni mpenzi wa MUNGU! 
   
Pia ina ashiria ya kuwa kuna kikundi kinachotaka kuendesha Chama hicho, kwani suala la kumuambia mwenyekiti wao awatose, ni kukiuka demokrasia ndani ya chama hicho kwa kumfanya mtu mmoja kuwa na maamuzi ndani ya chama hicho, kwangu mimi naona huo ni ubabe zaidi kuliko busara. 
  
Mimi ningependa kusikia watu wanajadili namna ya kutatua matatizo yaliyopo Tanzania na sio kuanza kuwauma wale wanaosema ukweli au kuweka wazi matatizo yaliyopo nchini.  
 
Maendeleo ni kwa watanzania wote na sio ya mtu binafsi, tabaka la watu au chama fulani!
Nawashauri baadhi ya wanasiasa wetu waende Loliondo kwa Babu kupata tiba ya fikra na vitendo!!. :-(

6 comments:

Malkiory Matiya said...
This comment has been removed by the author.
Malkiory Matiya said...

Ipo siku CCM itagawanyika na kufa kifo cha mende. Hizi ni dalili tu za mwanzo.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

tatizo ni kubwa, wako kimaslahi kaa wewe (CHIB) ulivyoko nje ya nchi kimaslahi.

wasingekuwa kimaslahi mambo yangeeleweka.

hamna anayeweza kuisafisha kwani wote ni maslahi zaidi

Chib said...

Kamala, Kila mtu yupo kimaslahi kwa ajili ya kujiboresha mwenyewe na watu anao wahudumia. Lakini maslahi binafsi ndio ugomvi upo hapo!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sipo na sitakuwepo. we unaona nipo kweli???

hata wewe uliko ni kimaslahi binafsi, ungeambiwa uwe huko kwa maslahi yangu kwa mfano, unafikiri ungekupo bado?

SIMON KITURURU said...

Mmmmh!