Member of EVRS

Thursday, 3 March 2011

Uongo wa Waziri Mkuu Pinda Bungeni!!

Kwa wale wanaokumbuka katika kikao cha Bunge la Tanzania kilichopita, Spika Makinda alimwagiza Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kuwasilisha ushahidi kimaandishi kuthibitisha ya kuwa Mhesh Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda alitoa taarifa ya uongo bungeni kuhusiana na mauaji yaliyotokea Arusha mara baada ya polisi kuzuia kufanyika kwa maandamano hayo.

Itakumbukwa ya kuwa Spika Makinda alikataa ushahidi huo kutolewa bungeni na kufafanua ya kuwa aliagiza uletwe kwa maandishi tu.

Godbless Lema aliwasilisha ushahidi wake akibainisha kwa ujumla uongo 10 ambao Pinda aliutoa katika bunge.

Soma hapa kwenye blog ya Mnyonge... upate ushahidi wote wa Mhesh Lema

1 comment:

Upepo Mwanana said...

Hakika ushahidi huo unatisha, kama viongozi wetu wamekuwa waongo kiasi hicho... Tutafika kweli!