Kampuni ya huduma za mawasiliano kwa njia ya simu ya Airtel inayomilikiwa na Bharti ya India, leo imezindua huduma zake nchini Rwanda na hivyo kuongeza idadi ya nchi ambazo Airtel inatoa huduma zilizopo barani Afrika kufikia 17.
Nchi ambazo kwa sasa zinafikiwa na huduma za Airtel katika bara la Afrika ni Burkina Faso, Niger, Nigeria, Zambia, Kenya, Tanzania, Uganda, Chad, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Congo Brazaville, Sierra Leone, Madagascar, Ushelisheli (Seychelles), Ghana na Gabon.
Bharti Airtel Ltd, ina mpango wa kuwekeza kiasi cha dola za Kimarekani milioni 100 katika kipindi cha miaka 3 ijayo. Kati ya hizo, dola milioni 30 zitatumika katika kupata leseni ya uendeshaji!
Pia, kampuni hii inatarajia kutoa zaidi ya ajira 300 kwa wananchi wa Rwanda, nyingine zikiwa ni za moja kwa moja na nyingine si za moja kwa moja.
Inatarajiwa gharama za kutumia simu zitapungua kwa sababu nguvu ya ushindani kwa sasa itaongezeka baada ya makampuni yanayotoa huduma hizo kwa sasa kufikia matatu. Mengine ni TIGO na MTN.
Showing posts with label Rwanda. Show all posts
Showing posts with label Rwanda. Show all posts
Friday, 30 March 2012
Thursday, 19 January 2012
Rwanda Yapunguza Kodi ya Nishati ya Mafuta Kupunguza Makali ya Mfumuko wa Bei
Wakati mfumuko wa bei unaelekea kupanda hapa Rwanda, na hivyo kuelekea kupandisha bei za bidhaa mbalimbali za vyakula na matumizi mengine. Serikali ya Rwanda imeamua kupunguza tozo ya kodi kwa mafuta kwa asilimia 6% . Taarifa hii ya punguzo ilitolewa na wazara ya Biashara na Viwanda.
Hali hii imesababisha kushuka mara moja kwa bei ya mafuta kutoka Faranga za Rwanda 1,000 kwa lita moja ya mafuta ya petroli na dizeli hadi Faranga 940. Hii ni sawa na punguzo la asilimia 6% kwa kila lita inayonunuliwa. Bei elekezi ilitolewa na wizara hiyo ikitegemea bei ya mafuta ya rejareja haitazidi Faranga za Rwanda 940 kwa lita.
Baada ya kutangazwa bei hii mpya, vituo vyote vilishusha bei na hakukuwa na tatizo lolote la vituo kuacha kuuza mafuta kama inavyokuwa Kenya na Tanzania.
Hii ndio serikali inayojali mustakabali na uchumi wa wananchi wake.

Thursday, 7 April 2011
Rwanda Leo Yaadhimisha Miaka 17 ya Mauaji ya Kimbari Dhidi ya Watutsi
Leo imetimia miaka 17 tangu mauaji ya Kimbari ya Rwanda kutokea.
Kwa miaka yote tangu mauaji hayo ya kikatili dhidi ya Watutsi yafanyike, tarehe kama ya leo watu hukumbuka matukio ya mwaka 1994 kwa hotuba na baadhi ya watu kutoa ushuhuda wa matukio ya wakati huo. Kwa ujumla huamsha hisia na uchungu kwa manusura, baadhi yao hupata mfadhaiko wa akili kiasi cha baadhi yao kulazimika kupelekwa hospitali kwa matibabu.
Katika hotuba ya kitaifa siku ya leo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, katika machache aliyozungumza, hakuficha hisia zake na hasira kwa wale wanaoendelea kupinga mauaji hayo ya kimbari dhidi ya watutsi (Genocide against Tutsis), na pia aliyashutumu mataifa yanayoendelea kuwaficha watuhumiwa wakuu wa mauaji hayo ambao wamejificha katika baadhi ya nchi hususan za Ulaya, na kukataa kata kata kuwatoa kwa ajili ya kushitakiwa kisheria. Alitoa hisia yake ya kuwa nchi hizo zinaogopa kuwatoa kwa sababu zinaogopa ushahidi utakaotolewa na hao watuhumiwa, utadhihirisha ni jinsi gani nchi hizo zilishiriki katika kufanikisha mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi wa Rwanda.
Siku kama ya leo huwa ni mapumziko ya kitaifa, na shughuli zote za kikazi husimamishwa ikiwa ni pamoja na maduka kufungwa na shughuli zote za kibiashara kusimamishwa.
Jinsi nilivyoiona siku ya leo, sikuona tofauti na siku nyingine za maadhimisho ya mauaji hayo hasa nikilinganisha na maadhimisho ya miaka iliyopita, kwani jiji la Kigali limepooza sana, na watu wachache wanaotembea barabarani, sura zao zinaonyesha huzuni kubwa.
Nakubaliana na msemo wao NEVER, NEVER... IT WILL NEVER HAPPEN..... NEVER AGAIN

Sunday, 3 October 2010
Tanzanian Festival - Kigali, Rwanda
Siku ya jumamosi, tarehe 2 oktoba 2010, umoja wa wanawake wa kitanzania waishio Rwanda, waliandaa vyakula vya asili ya Kitanzania ili kutunisha mfuko wao wa maendeleo. Shughuli hii ilifanyika kwenye hoteli mpya inaoendeshwa na Mtanzania kwa ubia iitwayo FOEYES PREMIER eneo la Bibare, jijini Kigali.
Kulisheheni vyakula mbalimbali ikiwepo supu ya makongoro, mtori, pilau la kibongo, vitumbua, samaki wa mpako, maandazi, chapati, aina zote za nyama choma isipokuwa kitimoto!, mihogo ya kuchemsha, kisamvu nk nk nk

Kwa wale wapenzi wa kinywaji, walifurahia bia za Tanzania, ambazo zimeanza kupatikana Kigali baada ya ufunguzi wa hoteli hii, na hakuna sehemu nyingine yoyote hapa Kigali unaweza kuzipata.
Mimi nilifunga kwa siku moja mahsusi ili niweze kufaidi Tanzanians Festival, lakini.... nafikiri walitayarisha double share, maana ... kilibaki ndugu.
Baada ya watu kushiba, ilikuwa ni saa ya kufukuza gout, kwa wale walioshindilia mbuzi huku wakiwa na matatizo ya gout!!!
Watu waliburudika na mduara na taarabu.
Kitu cha kufurahisha hapa, kila kitu kilikuwa kwenye utamaduni wa kitanzania, wafanyakazi karibu wote ni wanyarwanda, lakini walikuwa wanazungumza kiswahili vizuri, ikiwa ni pamoja na walinzi wa kampuni rasmi, wote waliokuwepo, yaani unajisikia kama upo nyumbani.
Home sweet hooooooome!
Thursday, 12 August 2010
Rwanda Vipi tena?!! Grenade attack!
You can get info in English here
Wakati watu wakianza kusheherekea ushindi wa Kagame, mara baada ya tume ya taifa ya uchaguzi kutangaza ushindi wa Kagame wa asilimia 93 hapo jana. Kufika saa moja jioni .. mara BOOOOOOM
Yaani watu wakarusha gruneti katika mtaa na nyakati ambapo watu huwa wanakuwa wengi wakitokea kazini kuelekea nyumbani, tena kwenye kituo cha mabasi ya usafiri wa jiji la Kigali, nikilinganisha na mabasi ya daladala labda katika kituo cha Kariakoo muda wa jioni.
Mlipuko ulikuwa mdogo, lakini ulijeruhi watu zaidi ya 7 na wengine kadhaa kupata majeraha madogo madogo.
Watu wengi hawakuwa na habari ya tukio hili, mimi nikiwa mmoja wapo, kwani nakaa mbali kiasi na mjini, na pia nimefunga matembezi ya jioni sana na usiku hasa sehemu za misongamano.
Kwa leo mji umetulia kabisa, huwezi kujua hata kama kulikuwa na tukio lolote. Maisha yanaendelea kama kawaida.

Wednesday, 9 June 2010
Rwanda Kuanza kutumia Bangi katika Matibabu. (Rwanda to Use Marijuana for Treatment Purposes)
The Rwanda Ministry of Health has forwarded a bill to parliament that seeks to legalize the use of marijuana and other narcotics to be used strictly for medical purposes.The minister, Dr. Richard Sezibera promised MPs that: “The medicine will thus be available and correctly utilised" as pain relievers, especially in treating the problems related to the behavioural problems.
Members of Parliament unanimously endorsed the bill without any objection
Huo ndio ukweli, Bangi imeidhinishwa kutumika kwa shughuli za matibabu hasa ya kutuliza maumivu kwa watu walioshindikana kitabia, na sio kwa ajili nyingine yeyote.
Hapa nawakumbuka ndugu zangu wa Iringa ambao hula bangi kama mboga ya majani ya kawaida, lakini sihusishi ulaji wa bangi hii na tabia ya kujinyonga..... :-(
Na pia nawakumbuka ndugu zetu wa Mara ambao ni maarufu kwa kulima bangi, ila sijui wao huwa wanaitumia kwa shughuli gani, ingawa na ukanda huo kwa kupenda kuuana kwa sababu za ki.#*.. :-((
Tuesday, 25 May 2010
Umoja Wa Watanzania Wanaoishi Rwanda: UTARWA wapata Viongozi
Takribani wiki 2 zilizopita, Watanzania waishio Rwanda tumeweza kufanikisha kuunda umoja wetu ambao unajulikana kwa kifupi kama UTARWA.
Jumuiya hii iko chini ya ulezi wa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda. Jumuiya hii au umoja huu uko mbioni kusajiliwa na una madhumuni makuu ya kuwakutanisha Watanzania waishio Rwanda, na pia kupeana taarifa na kusaidiana pindi Mwanachama anapopata tatizo lolote.
Zoezi la kuandikisha wanachama likiendelea kabla ya kuanza mkutano

Wajumbe wakipitia rasimu ya katiba ya jumuiya kabla ya kuifanyia marekebisho ya mwisho na kuipitisha
Wajumbe wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Dr Matiko Chacha Marwa ambayo aliitoa baada ya kupata viongozi wa Jumuiya.
Jumuiya hii iko chini ya ulezi wa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda. Jumuiya hii au umoja huu uko mbioni kusajiliwa na una madhumuni makuu ya kuwakutanisha Watanzania waishio Rwanda, na pia kupeana taarifa na kusaidiana pindi Mwanachama anapopata tatizo lolote.
Wajumbe wakipitia rasimu ya katiba ya jumuiya kabla ya kuifanyia marekebisho ya mwisho na kuipitisha
Katika mambo aliyoyasisitiza ni kuwasihi Watanzania kuchangamkia fursa ya kufanya biashara Rwanda ambako kuna soko kubwa la bidhaa za Tanzania kwani zina viwango vya ubora wa hali ya juu kuliko bidhaa nyingi hapa.
Balozi Marwa Alitoa ushauri kwa watu wajihamasishe na kusambaza taarifa za kuja Rwanda kufanya biashara, na pia alisisitiza ya kuwa Serikali ya Rwanda imefungua milango kwa wanajumuiya ya Afrika Mashariki kuingia Rwanda na kufanya shughuli halali bila kulipia viza.
Subscribe to:
Posts (Atom)