Member of EVRS

Friday 30 March 2012

Airtel: Yazindua Huduma zake Rwanda

Kampuni ya huduma za mawasiliano kwa njia ya simu ya Airtel inayomilikiwa na Bharti ya India, leo imezindua huduma zake nchini Rwanda na hivyo kuongeza idadi ya nchi ambazo Airtel inatoa huduma zilizopo barani Afrika kufikia 17. 
  
Nchi ambazo kwa sasa zinafikiwa na huduma za Airtel katika bara la Afrika ni Burkina Faso, Niger, Nigeria, Zambia, Kenya, Tanzania, Uganda, Chad, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Congo Brazaville, Sierra Leone, Madagascar, Ushelisheli (Seychelles), Ghana na Gabon. 
  
Bharti Airtel Ltd, ina mpango wa kuwekeza kiasi cha dola za Kimarekani milioni 100 katika kipindi cha miaka 3 ijayo. Kati ya hizo, dola milioni 30 zitatumika katika kupata leseni ya uendeshaji!  
  
Pia, kampuni hii inatarajia kutoa zaidi ya ajira 300 kwa wananchi wa Rwanda, nyingine zikiwa ni za moja kwa moja na nyingine si za moja kwa moja.  
 
Inatarajiwa gharama za kutumia simu zitapungua kwa sababu nguvu ya ushindani kwa sasa itaongezeka baada ya makampuni yanayotoa huduma hizo kwa sasa kufikia matatu. Mengine ni TIGO na MTN. 

No comments: