Member of EVRS

Sunday 4 March 2012

Chelsea: Yamtimua Kocha Wake Andre Villas-Boas

Klabu ya mpira wa miguu ya Chelsea ya jijini London, leo imemfutia kazi ya kuifunza timu hiyo kocha Andre Villas-Boas baada ya kutetereka katika michezo ya ligi kuu ya England na pia mashindano ya Ubingwa wa ulaya. 
  
Kufuatia kupoteza mechi ya jana dhidi ya timu ya West Bromwich Albion kwa bao 1 - 0 wakiwa ugenini kulihamasisha uamuzi wa uongozi wa Chelsea kumuondoa kocha huyo mwenye umri wa miaka 34.
 
Kupoteza mechi hiyo ya jana kuliweka rekodi ya Chelsea kushinda mechi 3 tu kati ya 12 za mwisho za ligi kuu ilizocheza. 
 
Andre amedumu kwa siku 257 tu ndani ya Chelsea tangu alipoanza kazi ya kuifundisha Chelsea kuanzia tarehe 22 Juni 2011. Katika kipindi chote alichokuwa Chelsea, kocha huyu amekuwa akidaiwa ya kuwa alikuwa na migongano na wachezaji "wazee" ndani ya Chelsea, lakini haijathibitishwa ya kuwa ndio chanzo cha Chelsea kufanya vibaya msimu huu.
 
Kwa muda wa siku 10 zijazo, Chelsea itakuwa na kazi kubwa ya kuishinda timu ya Napoli ya Italia katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kupoteza mechi ya awali nchini Italia kwa kufungwa magoli 3 - 1.
Kabla ya hapo watalazimika kucheza mechi ya ugenini dhidi ya timu ya Birmingham kwenye mashindano ya kushindania kutwaa Kombe la chama cha soka cha Uingereza (FA Cup). Itakumbukwa ya kuwa mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge, timu hizo zilitoka sare ya bao 1 - 1 huku Chelsea ikitoka nyuma na kusawazisha bao hilo. Kwa sasa, timu ya Birmingham ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo.

1 comment:

Simon Kitururu said...

Chelsea na timu nzima ya Uingereza ni kama tu Timu ya Taifa Bongo,... NIVIGUMU sana kuwa KOCHA katika timu hizo!

Na hisi kocha wa Asernal hawezi kukaa wiki Chelsea bila kutimuliwa!
My 2 cents!