Member of EVRS

Thursday, 12 August 2010

Rwanda Vipi tena?!! Grenade attack!

You can get info in English here

Wakati watu wakianza kusheherekea ushindi wa Kagame, mara baada ya tume ya taifa ya uchaguzi kutangaza ushindi wa Kagame wa asilimia 93 hapo jana. Kufika saa moja jioni .. mara BOOOOOOM

Yaani watu wakarusha gruneti katika mtaa na nyakati ambapo watu huwa wanakuwa wengi wakitokea kazini kuelekea nyumbani, tena kwenye kituo cha mabasi ya usafiri wa jiji la Kigali, nikilinganisha na mabasi ya daladala labda katika kituo cha Kariakoo muda wa jioni.

Mlipuko ulikuwa mdogo, lakini ulijeruhi watu zaidi ya 7 na wengine kadhaa kupata majeraha madogo madogo.

Watu wengi hawakuwa na habari ya tukio hili, mimi nikiwa mmoja wapo, kwani nakaa mbali kiasi na mjini, na pia nimefunga matembezi ya jioni sana na usiku hasa sehemu za misongamano.

Kwa leo mji umetulia kabisa, huwezi kujua hata kama kulikuwa na tukio lolote. Maisha yanaendelea kama kawaida.

5 comments:

Anonymous said...

Hello!

I am new to this forum and look forward to making some new friends

big respect, Dennis from [url=http://www.myonlinepayday.com]Payday Loans[/url] website!

Maisara Wastara said...

Kwa mafanikio aliyoyafikia Rais Kagame, Wanyarwanda watajuta kurejea vitani......

Hizo chokochoko watakuja zijutia kwani hazina mwisho mzuri

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

unajua inashangaza wakati mwingine kwamba mtu anashinda kwa asilimia 90?? ikiwa ina maana kuwa watu wote wanafikiri sawa, kama wavisitors wa blogu ya chib ambao woote hufikiri sawa isiokuwa mimi mwenye maoni tofauti kidogo. naonekana mpiznzani

SIMON KITURURU said...

@Komandoo Kamala: :-)

Fadhy Mtanga said...

kusema ukweli huwa siielewi Rwanda kabisa...