Member of EVRS

Sunday 15 August 2010

Orodha ya Wagombea Ubunge wa CCM - 2010

Orodha ya wana CCM walioteuliwa kugombea ubunge mwaka 2010 bofya hapa kwa Subi uipate yote.

Kilichonishangaza ni mchanganuo wa elimu zao, wengine wameandkiwa elimu ya msingi, wengine darasa la saba. Wengine sekondari, wengine kidato cha tatu, nne, sita nk. Sikuelewa mantiki hii.

Tofauti ya darasa la saba na elimu ya msingi?!!!

Kazi kwako

3 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kuna mengi huyaelewi labda umwombe mungu ataakusaidia.. elimu ya msingi ni ile ya kujua kwenda chooni, kuchamba vyema na kuosha mikono baada ya hapo

ila ya darasa la saba ni ile ya kuhesabu kwa vijiti, kujua kuandika jina lako na la babako nk

na kidato cha nne au form four inafuatana na unavyojua kiingereza au ulipata div. gani

UNABISHI??

chib said...

Kamala, ha ha haaa, you made my day

Upepo Mwanana said...

Karne hii ya sayansi na teknolojia.. bado tunang'ang'ana na darasa la saba! Sasa hii ndio itatia uvivu watu kwenda shule.
Yaani hiyo website wamechemsha kisomo na miaka ya watu...