Member of EVRS

Sunday, 3 October 2010

Tanzanian Festival - Kigali, Rwanda

Siku ya jumamosi, tarehe 2 oktoba 2010, umoja wa wanawake wa kitanzania waishio Rwanda, waliandaa vyakula vya asili ya Kitanzania ili kutunisha mfuko wao wa maendeleo. Shughuli hii ilifanyika kwenye hoteli mpya inaoendeshwa na Mtanzania kwa ubia iitwayo FOEYES PREMIER eneo la Bibare, jijini Kigali.
Kulisheheni vyakula mbalimbali ikiwepo supu ya makongoro, mtori, pilau la kibongo, vitumbua, samaki wa mpako, maandazi, chapati, aina zote za nyama choma isipokuwa kitimoto!, mihogo ya kuchemsha, kisamvu nk nk nk
Kwa wale wapenzi wa kinywaji, walifurahia bia za Tanzania, ambazo zimeanza kupatikana Kigali baada ya ufunguzi wa hoteli hii, na hakuna sehemu nyingine yoyote hapa Kigali unaweza kuzipata.
Mimi nilifunga kwa siku moja mahsusi ili niweze kufaidi Tanzanians Festival, lakini.... nafikiri walitayarisha double share, maana ... kilibaki ndugu.


Baada ya watu kushiba, ilikuwa ni saa ya kufukuza gout, kwa wale walioshindilia mbuzi huku wakiwa na matatizo ya gout!!!
Watu waliburudika na mduara na taarabu.

Kitu cha kufurahisha hapa, kila kitu kilikuwa kwenye utamaduni wa kitanzania, wafanyakazi karibu wote ni wanyarwanda, lakini walikuwa wanazungumza kiswahili vizuri, ikiwa ni pamoja na walinzi wa kampuni rasmi, wote waliokuwepo,   yaani unajisikia kama upo nyumbani.

Home sweet hooooooome!

1 comment:

LNFAW said...

visit here http://lnfaw.blogspot.com