Member of EVRS

Wednesday, 20 October 2010

Here and There, Chicago

Eye Industry exhibition booths


This week, we had a meeting attended by more than 30,000 eye care teams from all over the world at Chicago, IL. It was an interesting experience! Something terrible to us was cold. ...
Green market at the heart of Chicago, masoko haya ni kama magulio ya huko kwetu nyumbani, kwani wakulima wanaleta mazao yao na kuyauza, wanayakuza bila kutumia mbolea wala virutubisho vya bandia. Lakini ... nyumbani si ndio muda wote tunatumia mbolea asili.....

Mihangaiko ya mitaani tu, usishangae mitaa kuwa mitupu, kibaridi si mchezo.


 Nilipita pita maeneo ya Cook County, ambapo Barack Obama alikuwa anaishi, na mtaa katika picha hii ya chini unaoitwa Ellis, kwa mbele kidogo, ndio kuna nyumba aliyokuwa anaishi Obama, kuna ulinzi mkali japo hauna mtu anayeishi katika nyumba hiyo, ilikuwa imepambwa na masanamu ya haloween!!
Sehemu hii ndio pekee nilipokuta walinzi wa jadi, au ukipenda community security, ambao walikuwa wapo wengi mtaa wa 51 ambako ndipo kuna nyumba ya Obama. Maeneo haya wanaishi watu wengi wenye asili ya Uafrika, ila .. duh, kuna sehemu nyingine, watu kaustaraabu wamekasahau.....
Bustani ya kupumzika Cook County, nje kidogo ya katikati ya jiji la Chicago, IL.

1 comment:

emu-three said...

Nimevutiwa na kausemi kako, umesema, kuna sehemu nyingine `kaustaarabu kamewashinda, kaustaraabu gani hako?
Tunashukuru kwa kutupa haya, twaomba utupe zaidi na hata maisha yao ya ndani, hakuna visa, visa huko?