Jumuiya hii iko chini ya ulezi wa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda. Jumuiya hii au umoja huu uko mbioni kusajiliwa na una madhumuni makuu ya kuwakutanisha Watanzania waishio Rwanda, na pia kupeana taarifa na kusaidiana pindi Mwanachama anapopata tatizo lolote.
Zoezi la kuandikisha wanachama likiendelea kabla ya kuanza mkutano
Wajumbe wakipitia rasimu ya katiba ya jumuiya kabla ya kuifanyia marekebisho ya mwisho na kuipitisha
Wajumbe wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Dr Matiko Chacha Marwa ambayo aliitoa baada ya kupata viongozi wa Jumuiya.
Katika mambo aliyoyasisitiza ni kuwasihi Watanzania kuchangamkia fursa ya kufanya biashara Rwanda ambako kuna soko kubwa la bidhaa za Tanzania kwani zina viwango vya ubora wa hali ya juu kuliko bidhaa nyingi hapa.
Balozi Marwa Alitoa ushauri kwa watu wajihamasishe na kusambaza taarifa za kuja Rwanda kufanya biashara, na pia alisisitiza ya kuwa Serikali ya Rwanda imefungua milango kwa wanajumuiya ya Afrika Mashariki kuingia Rwanda na kufanya shughuli halali bila kulipia viza.
11 comments:
kusaidiana wakati wa matatizo!! mna matatizo sana huko ehe??
Hongereni kwa kupata uongozi mpya.
Kumradhi: Ni Kusaidiana kwa mambo yote..
Hongereni sana kusaidiana ni maja ya maisha hapa duniani na pia hongera kwa kupata uongozi mpya.
Hongereni sana kwa kuunda umoja na kupata viongozi, nawatakia kila yalio mema
Hivi kwa Makisio Rwanda kuna kama Watanzania wangapi?
Hongereni kwa kujipanga!
mwanzo mzuri, tunwaombea kila la kheri
mambo gani?? ngoja niishie hapa maana!! kuna mambo ambayo hamwezi kusaidiana tusidanganyanye!!
Hongereni sana.
Kamala tukuzoea.. Mr Controversial, he he hee
Hongereni sana! Mama Ulimwengu ni kiongozi mahiri. Mpeni sapoti.
Post a Comment