Member of EVRS

Tuesday, 21 December 2010

Hukumu ya BAE SYSTEMS Kutolewa Leo

Hukumu kesi ya shirika kubwa la kuuza silaha la Uingereza (BAE Systems) itatolewa kesho na Jaji Bean anayesikiliza madai ya kampuni hiyo kujihusisha na rushwa kubwa kwa kuiuzia Tanzania radar ya kijeshi ambayo iliigharimu nchi maskini ya Tanzania zaidi pauni za Uingereza milioni 28 ( Zaidi ya sh.billioni 70 za kitanzania)

Hakimu huyo aliihoji kampuni hiyo kuhusu madai ya kumlipa mfanyabiashara Sailesh Vithlani kiasi cha kama pauni millioni 7.7, katika kujitetea kampuni hiyo ilidai ilitoa pesa kumpa Vithlani kwani walimtumia kama papa mdogo kupenyeza ili waweze kushinda zabuni ya kuiuzia Tanzania rada hiyo kwa bei ya kuruka.
Kampuni ilikiri kuwa na kosa dogo la kuweka vizuri kumbukumbu za mahesabu kwa kudai walimlipa Vithlani kama mshauri wa kiufundi wakati Vithlani mwenyewe hakuwa na ujuzi wowote katika masuala hayo ya ununuzi wa rada.

Jaji hakuridhika na maelezo hayo, na akaendelea kusisistiza kuna kila dalili ya rushwa kwani alihoji kwa nini zaidi ya 97% ya malipo ilipitia  kwenye mikono ya Vithlani!, kiasi kwamba alitaka kutoa uamuzi wa kuita mashahidi kueleza ni vipi pesa alizopewa Vithlani zilivyotumika kabla ya kutoa hukumu yake, lakini baadaye alibadili mawazo yake na kuahidi kutoa ya hukumu dhidi ya BAE System leo siku ya Jumanne.
 
Hapo awali, kampuni hii ilikiri kuwa na makosa ya kuweka vibaya kumbukumbu za pesa, na ilikubali kulipa pauni milioni 3 kama fidia kwa Tanzania na pesa hizo kutumika nchini Tanzania kwa ajili ya shughuli za maendeleo. Lakini ikawa inasisitiza haikutoa mlungula wowote.

Pata maelezo zaidi kwa mwanzilishi wa mjadala huu wa uuzwaji wa rada hii kwa bei isiyo na tija

1 comment:

emu-three said...

Haya ngoja tusubiri hiyo hukumu