Member of EVRS

Saturday, 4 December 2010

Vituko vya Marais wa Afrika: Ivory Coast Presidential Results Controversy

I hate people who thinks they were created to be leaders for life, look this man from Ivory Coast!
  
Marais wengi wa Afrika wana kasumba ya kujiona kuwa wao ndio pekee wanaofaa kuongoza nchi kama wafalme, yaani kifo tu ndicho kinaweza kuwaondoa madarakani.

Mifano michache ya ving'ang'anizi ni kama Museveni (Uganda), Mugabe (Zimbabwe), Mubarak (Misri), na hata huyu jamaa wa Angola ambaye kaamua kuwa rais anachaguliwa na wabunge walioshinda katika uchaguzi na sio wananchi tena.

Nguli mwingine ni Laurent Gbagbo wa Ivory Coast (pichani juu) ambaye ametia mpya hivi karibuni ktika uchaguzi huru uliofanyika nchini Ivory Coast. Katika raundi ya mwisho alipokuwa anashindana na mpinzani wake mkuu Allasane Ouattara (pichani chini), alihisi kuelemewa na hivyo kuamuru matokeo yasitishwe kutangazwa, na sehemu iliyokuwa bado kumaliza kutolewa matokeo ilikuwa ni ngome ya mpinzani wake
Hii ilisababisha kuchelewa kutolewa matokeo kwa siku mmoja, hata hivyo tume ya uchaguzi ilimtangaza Ouattara kama mshindi  kwa kupata  54%, na miongoni mwa watu wa kwanza kumpongeza alikuwa Rais Obama wa Marekani.
    
Cha kushangaza, baraza la katiba ambalo ndicho chombo kikuu cha mwisho kuidhinisha matokeo kilipinga matokeo ya tume na kusema tume ilichelewesha kutoa matokeo, na hivyo baraza hili likachakachua matokeo na kumtangaza Gbagbo kuwa kashinda kwa 51.45%.

Kwa sasa jeshi limefunga mipaka yote ya Ivory Coast, na kuzuia vyombo vya habari vya kimataifa kuchukua na kurusha habari zozote za uchaguzi huo.

Ufaransa na Umoja wa Mataifa umekataa kutambua matokeo ya pili ambayo yalimwengua Ouattara kwenye nafasi ya ushindi.

Ndugu yangu, utajiju na maswali yatakayokujaa kichwani mwako!!

3 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

marais wetu wengi wana tabia na hulka kama yako ya kujiona kuwa wewe ndiye mwenye haki pekee ya kushea kitanda na mkeo na usitake wengine wainjoy!!!!!

SIMON KITURURU said...

Ndio viongozi wetu hao! Matumbo yao muhimu kuliko jamii waiongozayo!

chib said...

Kamala naona hauna sera za kuuza :-)